ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 6, 2015

HALMASHAURI YA USHETU KUGAWA PEMBEJEO KWA WAKULIMA

Na Emmanuel Mlelekwa
Novemba 6,2015.
KAHAMA

Kuelekea msimu mpya wa kilimo Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga imewataka wakulima kutumia Pembejeo zinazosambazwa na Mawakala waliothibitishwa na Serikali badala ya kununua  mtaani.

Akizungumza na Jembe Fm Kaimu Afisa Kilimo wa Halmashauri hiyo Mshana Wilson amesema kuwa Serikali imepanga kuboresha kilimo cha Wakulima kwa kuleta Pembejeo bora ambazo zitakuwa na tija kwa wakulima.

Mshana amesema kuwa Wakulima wanatakiwa kutumia Pembejeo  zinazosambazwa na serikali kwa mfumo wa Vocha na tayari usambazwaji wake umeanza kwa utaratibu maalum  kupitia ofisi za kata.

Ameongeza kuwa Halmashauri hiyo  imepata Vocha ya Pembejeo za  Mahindi na Mpunga kwa upande wa mazao ya Chakula, Pamba na Tumbaku kwa upande wa  Biashara pamoja na Mbolea na Madawa ambazo zitagawiwa kwa wakulima.

Hata hivyo takwimu sahihi ya idadi ya wakulima watakaopatiwa Pembejeo hizo bado haijafahamika sanjari na gharama ya vocha ya Pembejeo hhizo kutokana na Mawakala wa usambazaji kutowasilisha nakala  hadi sasa kwa Mkurugenzi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.