ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 18, 2015

TEMEKE WATINGA NUSU FAINALI

Mchezaji wa timu ya Ilala Rukia Annaph (kushoto) akichuana vikali na mchezaji wa timu ya Temeke Christina Daudi katika mchezo wa nusu fainali ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi September 17. Temeke ilishinda 2-1
Mchezaji wa timu ya Ilala Tumaini Michael (Kulia) akimtoka mchezaji wa timu ya Temeke Shamimu Hamis katika mchezo wa nusu fainali ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi September 17). Temeke iliibukana na ushindi wa magoli 2-1.
Mchezaji wa timu ya Ilala Jackline Albert (Kushoto) akimtoka mchezaji wa timu ya Temeke Shamimu Hamis katika mchezo wa nusu fainali ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi September 17. Temeke ilishinda 2-1.

Temeke watinga fainali ARS.
Temeke girls jana walifanikiwa kutinga hatua ya fainali, baada ya kuwagaragaza majirani zao wa Ilala kwa kuwafunga mabao 2-1 katika muendelezo wa michuano ya U-17 ya Airtel Rising Stars, mchezo uliofanyika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.

Ilala ambao walionekana kuumiliki mpira kwa kiasi kikubwa sana katika kipindi cha kwanza walifanikiwa kuandika bao lao mnamo dakika ya 1 baada ya Tumaini Michael kuachiashuti na kutinga wavuni huku kipa wa Temeke akiwahana la kufanya.

Alamanusra Ilala wapate bao la pili manmo dakika ya 20 baada ya Tumaini Michael tena kupiga mpira wa kichwa ambao ulipaa kidogo langoni mwa Temeke.

Katika kipindi cha pili, Temeke walionekana kucharuka huku wakicheza kwa kasi kubwa, na ndipo mshambuliaji wa timu hiyo, Shamimu Hamisi mnamo dakika ya 40, alipomalizia kwa umaridadi mpira uliotemwa na kipa wa Ilala na kuukwamisha moja kwa mojawavuni na kusawazisha goli.

Temeke waliofanikiwa kuandika goli la pili mnamo dakika ya 61 kupitia kwa Asia Juma na kudidimiza matumaini ya Ilala kutinga hatua ya fainali.

Baada ya mchezo huo kocha wa Ilala Omari Bwezi alisema: “Tumekubali matokeo, wachezaji wangu walicheza vizuri kipindi cha kwanza lakini walionekana kuchoka sana kipindi cha pili na kuwapa nafasi ya kutawala wenzetu na ndio maana tukafungwa”.


Naye kocha wa Temeke Daudi Siang’a alisema: “Vijana wangu walifuata niliyowalekeza wakati wa mapumziko na waliporudi uwanjani walifanya nilicho waeleza na hatimaye tukapata matokeo”.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.