ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 25, 2015

CHANGAMOTO ZA JIMBO LA ULYANKULU WANANCHI WATAKA MBUNGE AJAYE AZIMALIZE

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ulyankulu wilayani Kailiua mkoani Tabora akiomba kura ili kumaliza changamoto ya maji safi, barabara, umeme, elimu na afya zinazolikabili jimbo hilo wakati wa mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika Kata ya Kashishi mpakani mwa Mji wa Kahama mkoani Shinyanga na jimbo hilo jana Picha Na Peter Fabian.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ulyankulu wilayani Kailiua mkoani Tabora akiomba kura ili kumaliza changamoto ya maji safi, barabara, umeme, elimu na afya zinazolikabili jimbo hilo wakati wa mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika Kata ya Kashishi mpakani mwa Mji wa Kahama mkoani Shinyanga na jimbo hilo jana Picha Na Peter Fabian.

NA PETER FABIAN, ULYANKULU.

WANANCHI wa Jimbo jipya la Ulyankulu Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora wametakiwa kuvumilia hadi kumalizika kwa uchaguzi ili Mbunge watakayemchagua John Kadutu wa Chama Cha Mapinduzi aweze kuanza kazi ya kuibana serikali juu ya kero na matatizo yanayolikabili jimbo hilo kwa sasa.

Kauli hiyo imetolewa jana na Kadutu (CCM) anayewania kuchagulilwa na wananchi mwezi Oktoba mwaka huu ili awe Mbunge wa Jimbo hilo atakayetekeleza wajibu wake kwa vitendo katika kuwaletea maendeleo wananchi, alipofanya mikutano ya kampeni kwa nyakati tofauti katika vijiji vya Kata ya Kashishi iliyoko mpakani na Mji wa Kahama (Shinyanga) kwa na lengo la kujinadi na kuomba kura.


Kadutu aliwaeleza wananchi hao kwamba baada ya serikali kukubali kuligawanya jimbo la Urambo Magharibi na kuzaliwa majimbo mawili la Kaliua na Ulyankulu kutasaidia kufikisha huduma za kijamii na maendeleo haraka kwa serikali ya awamu ya tano kuwapatia Wilaya na Halmashauri, lakini pia wakimchagua atapigania uboreshaji wa miundombinu ambayo ni kero kubwa.

“Barabara hazipo na zilizopo hazina ubora katika maeneo mbalimbali kutokana na kutopitika kilahisi, jingine ntakalo lisimamia kuomba serikali itusaidie kwa haraka ni miundombinu ya shule za msingi na sekondari kukabiliwa na changamoto ya upungufu mkubwa wa majengo na nyumba za walimu ikiwemo vyoo kutokuwepo na kupelekea wanafunzi kujisaidia kwenye machaka,”alisema.

Aidha alisema kwamba changamoto nyingine atakayoisumbua serikali akiwa Mbunge ni jimbo hilo kutokuwa Hospitali ya Wilaya kutokana na iliyopo kubaki jimbo la Kaliua, kupigania serikali iendelee kumbana Mkandarasi wa usambazaji umeme vijijini kutoka Grid ya Taifa kwenye maeneo yote ya vijijini ambapo kwa sasa sehemu kubwa wananchi wanatumia umeme wa Nishati ya  jua (Sorla).

“Kata hii ipo jirani na Mji wa Kahama ambapo ni kilomita 80 mkinichagua tu mtanisikia nikimbana Rais na Waziri wa Wizara ya  Maji ili tupate mradi mkubwa wa maji safi kutokea Ziwa Victoria yaliyokwisha fika Mji wa Kahama yafike hadi Ulyankulu kabla ya kuanza kupeleka Mjini Tabora (zaidi kilomita 200),  Mji wa Nzega na Igunga ili kuondoa kero hii,”alisisitiza.

Kadutu aliwahidi wananchi hao kuibana Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika juu ya makato ya fedha za ruzuku ya zao la Tumbaku ili kuwezesha kujiunga na Mfuko wa Bima  ya Afya pamoja na kucheleweshwa kwa fedha za wakulima pamoja na fedha za ruzuku ya serikali ya vijiji na kusababisha kuwepo malalamiko ya wakulima kwa Makampuni ya ununuzi wa zao hilo.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ulyankulu wilayani Kaliua mkoani Tabora, John Kadutu (kulia) akimkabizi Ilani ya Uchaguzi mgombea Udiwani wa Kata ya Kashishi  Silas Masanja (kushoto) mbele ya wananchi na kuomba wamchague ili kurahishisha utakelezaji wake na kumshirikisha katika kumaliza kero na changamoto zinazoikabili Kata hiyo na Jimbo hilo kwa ujumla kwenye mkutano wa kampeni jana Picha Na Peter Fabian.
“Kwa hili wakulima nitapambana kuhakikisha mnalipwa masilahi ya jasho lenu pamoja na kuhakikisha makubaliano ya fedha za makato ili Halmashauri itekeleze kuwaingiza kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya muweze kupata matibabu ikiwemo wazee kupata huduma hiyo bure na wanawake wakati wa kujifungua, lakini pia muweze kunufaika na kukomesha makampuni kuwatapeli wakulima,”alisisitiza.

Kadutu aliwaomba wananchi wamchague mgombea Dk John Magufuli kuwa Rais wa awamu ya tano, yeye pamoja na Madiwani wanaotokana na CCM ili kuyatekeleza yaliyopo kwenye Ilani ya uchaguzi aliyowaahidi huku akiwahasa wananchi kutokubali kudanganywa na wagombea wa vyama vya upinzani kwani wengi wao hawana dhamira njema ya kuwatumikia bali kuwagawa na kuwabagua kwa manufaa yao binafsi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.