ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 11, 2015

NIA YA UDIWANI KATA YA SEGEREA NUSURA UMTOE ROHO MTOTO WA MASSABURI

Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya Segerea,  Steve Massaburi akiwa Hospitali ya Aga-khan leo akiendelea na matibabu.
Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya Segerea,  Steve Massaburi akiwa Hospitali ya Aga-khan leo akiendelea kuuguza majeraha baada ya kujeruhiwa kwa mapanga nyumbani kwake Segerea jijini Dar es Salaam jana na watu wasiojulikana. Kushoto anayemuhudumia ni jamaa yake Martin Pemba.

Na Dotto Mwaibale

WATU wasiojulikana wamejeruhi kwa mapanga Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya Segerea Steve Massaburi usiku wa kuamkia juzi nje ya nyumba yake alipokua akirejea kutoka matembezini.

Kwa mujibu wa Steve aliyelazwa katika Hospitali ya Aga khan, watu hao wapatao wanne wakiwa na Pikipiki, walimvamia majira ya saa tatu usiku nje ya geti la nyumba anayoishi na kuanza kumshambulia huku yeye akijaribu kupambana nao.

Steve ambaye ni mtoto wa Meya wa Jiji la Dar es salaam Dk. Didas Massaburi, alisema wakati watu hao wakimshambulia walikuwa wakisema wazi wazi kuwa lengo lao ni kumuona hagombei nafasi ya udiwani katika Kata hiyo ya Segerea baada ya yeye kuonyesha nia ya kutaka kugombea nafasi hiyo.

“Walikuwa wakiniambia kuwa wewe si unautaka udiwani sasa utaugombea ukiwa kitandani au kaburini, hapa hakuna na umaharufu wa mtu kwa kuwa kila mtu anaitaka nafasi hiyo” alisema Massaburi.

Alisema wakati akiendelea kupambana na watu hao alikuwa akipiga kelele jambo lililowafanya watu hao kumuacha na kasha kukimbia huku yeye akiwa amelala chini damu zikimtoka sehemu za shavuni kutokana na panga alilopigwa.

Pamoja na sehemu ya shavuni, watu hao pia wamemjeruhi sehemu mbalimbali za mkono wake wa kushoto alipokuwa akijaribu kuzuia panga kumdhuru sehemu za usoni.

“Kelele nilizopiga ndizo zilizonisaidia kwa kuwa ziliwafanya watu watoke katika majumba yao kuja kunisaidia wakati huo huo watu hao wakikimbia kwa kutumia pikipiki zao mbili walizokuwa wamekuja nao” aliongeza.

Alisema kwa sasa hali yake inaendelea vizuri  tangu alipofikishwa hospitalini hapo jana huku akishonwa nyuzi zaidi ya ishirini katika taya lilipigwa na panga na watu hao. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.