ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 12, 2015

UNFPA-TANZANIA KWA KUSHIRIKIANA NA TUME YA MIPANGO YAENDESHA WARSHA MKOA WA MARA

Mgeni Rasmi Bw. Ibrahim D. Kalengo, Mtakwimu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ambae anamwakilisha Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, akitoa neno kwa ajili ya warsha hiyo kufunguliwa rasmi.

 SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA IDADI YA WATU (UNFPA) TANZANIA
KWA KUSHIRIKIANA NA OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO YAENDESHA
WARSHA KATIKA HOTEL YA AFRILUX MJINI MUSOMA

Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, wameandaa warsha kwa ajili ya kuhamasisha na kuwajengea uwezo watumishi wa Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu kujumuisha masuala ya vijana katika mipango ya Mkoa na wilaya.

Warsha hiyo inafanyika katika vituo vya Mwanza na Musoma. Katika kituo cha Musoma warsha inafanyika katika ukumbi wa Afrilux Hotel tarehe 11 na 12 Juni 2015. Kituo hiki kinajumuisha Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za mkoa wa Mara na Simiyu.

Washiriki wa warsha ni Makatibu Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya.
Mwezeshaji Dr. Deograsias P. Mushi ambae pia ni Mchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mtafiti wa Ecom Research Group akishusha nondo kwa wanawarsha juu ya mambo mbalimbali yanayohusu ujumuishaji wa masuala ya vijana katika mipango ya maendeleo ya mkoa na wilaya.
Afisa kutoka UNFPA anaeshughulikia maswala ya vijana Bi. Tausi Hassan, akisisitiza jambo kwa washiriki wa warsha kuhusu program za vijana katika shirika la UNFPA.
Washiriki wa warsha kutoka Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za mkoa wa Mara na Simiyu ambao ni Makatibu Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya wakimsiliza kwa makini mwezeshaji.
Washiriki wa warsha kutoka Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za mkoa wa Mara na Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa warsha hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.