ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 15, 2015

SHIRIKA LA UMEME TANESCO PWANI LATOA TAHADHARI KWA WANANACHI WANAOFANYA BIASHARA CHINI YA NGUZO ZA UMEME.

NA VICTOR MASANGU, PWANI 
 
SHIRIKA la ugavi wa umeme Tanesco Mkoa wa Pwani  limewataka wananchi na wafanyabiashara ambao kwa sasa wanaoendeshea shughuli zao mbali mbali chini ya nguzo   za umeme kuondoka mara moja kutokana na kuwepo kwa hali ya hewa ya mvua kubwa ambayo inaweza kuhatarisha maisha yao.
 
 Hayo yamebainshwa na Afisa usalama wa Tanesco Mkoa wa Pwani Hery Byarugaba wakati wa zoezi la kufanya ukaguzi  wa miundombinu ya umeme ya shirika hilo  ikiwemo mita, nyaya,  transfoma, nguzo pamoja na mingineyo ili kuweza kuifanyia matengenezo.
 
 Afisa huyo alibanisha  kwamba kwa sasa wananchi wanatakiwa kuwa makini kutokana na kuharibika kwa miundombinu ya umeme kutokana na mvua ambayo inaendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali.
 
Byarugaba alisema kwamba kutokana na kuwepo kwa mvua hizo sambamba na upepo mkali umesababisha kuwepo kwa uharibifu mkubwa wa miundombinu ya umeme ikiwemo kudondoka kwa nguzo zaidi ya nane hivi karibuni hali ambayo inaweza kuleta madhara makubwa kwa wananchi hivyo wanatakiwa wasiwe chini ya nyaya za umeme.
 
“Kwa sasa kitu kikubwa tunachokifanya kama tanesco ni kuhakikisha tunafanua jitihada za hali na  mali katika kukagua miundombinu yetu ya umeme ili kama kuna tattizo lolote la kiufundi tuweze kuikarabatiharaka iwezekanavyo na kuweza kuwapatia huduma wateja wetu ambayo inasatili,”alisema Byarugaba.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Enarist Ndikilo amewaomba wazazi na walezi katika Mkoa wa Pwani kuwa makini na watoto wao na kuachana na kuwatuma katika maeneo ya mbali huku wakiwa peke yao na badala yake wawalinde kwani wanaweza kusombwa na maji.
 
“Nadhani mamlaka husika ya hali ya hewa tayari imeshatoa taadhari kuwa mvua bado inaendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Pwani na maeneo mengine hivyo kitu kikubwa ninachowaomba wazazi na walezi kuwa makini na watoto wao, kwani wanaweza kupoteza maisha kutokana na mvua hizi,”alisema Ndikilo.
 
Aidha Injia Ndikilo amewataka wavuzi katika maeneo ambayo yapo kando kando ya  bahari ya hindi kutoendelea na shughuli zao za ufuaji wa samaki kwani kwa sasa bahari imechafuka hivyo lolote linaweza likajitokeza kutokana na kuwepo kwa mvua kubwa kunyesha ambazo zinaambatana na upepo mkali ambozo zinaweza kuleta madhara makubwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.