ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, April 1, 2015

RC PWANI AWASHUKIA WATUMISHI WA UMMA NA WATENDAJI WA SERIKALI KWA KUENDEKEZA USHABIKI WA SIASA

NA VICTOR MASANGU,MKURANGA  PWANI   APRIL 1  .. 20 15

MKUU wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo amewataka watumishi wa  umma pamoja na watendaji wa halmashauri  kuachana na tabia ya kuwa na itikadi ya vyama vya siasa ambayo wakati mwingine yanaleta migogoro na badala yake wajikite zaidi katika kuwatumikia wananchi wao pamoja na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kuleta maendeleo na sio vinginevyo.
Injinia Ndikilo ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na watumishi  wa umma pamoja na madiwani wakati alipofanya ziara yake ya kikazi ya siku moja  katika Wilaya ya Mkuranga  yanye lengo la kuweza kubaini cangamoto zinazowakabili pamoja na akukagua miradi mbali mbali ya maendeleo.
Mkuu huyo amesema kwamba watumishi wa umma wamekuwa wakilipwa mshahara kutokana na kufanya kazi, hivyo wanapaswa kuwatumikia wananchi wao kwa nguvu zote na sio kutumia muda mwingi katika kubishana katika mambo hayana msingi wowote na kina.
BOFYA PLAY MSIKILIZE RC NDIKILO

Aidha Ndikilo ametoa muda wa siku tatu kwa wazazi na walezi wenye watoto ambao wamefaulu kuingia kidato cha kwanza lakini  hadi sasa bado wapo majumbani kwao kuwapeleka haraka iwezekanavyo lasi hivyo atawachukulia hatua kali za kisheria kwa kuwakamata na kuwapeleka kaatika vyombo vya dola.
MSIKILIZE INJINIA

Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa halmashauri  ya Mkuranga Juma Abeid ambaye akusita kumweleza Mkuu wa Mkoa wa Pwani kilio chao pamoja na  changamoto ambazo zinawakwamisha katika kutekeleza kwa wakati miradi  mbali mbali ya maendeleo.
MSIKILIZE MAKAMU ABEID

 Naye Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Abdalah Kiato awali akisoma ripoti ya utekelezaji kwa Mkuu wa Mkoa naye alikuwa na haya ya kusema, sambamba na kubainisha changamoto walizonazo.
MSIKILIZE DC NDIKILO

Wilaya ya Mkuranga ambayo kwa sasa ina idadi ya watu zaidi ya laki mbili bado inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo kutokamilisha ujenzi wa maabara katika shule za sekondari, wazazi kutowapeleka watoto  wao shule, miundombinu ya barabara kuwa mibovu pamoja na hali ya kuwepo kwa wimbi la kuwepo kwa bandari bubu ambazo zimekuwa ni kikwazo cha muda mrefu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.