ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 4, 2015

MVUA YASABABISHA KUAHIRISHWA KWA MECHI YA KAGERA Vs SIMBA DIMBA LA CCM KAMBARAGE

 NA ALBERT G SENGO: SHINYANGA

Kufuatia mvua kubwa kunyesha kwa takribani siku mbili mchezo wa Ligi Kuu soka Tanzania bara baina ya Kagera Sugar dhidi ya Simba Sports Club uliokuwa uchezwe kwenye dimba la CCM Kambarage mjini Shinyanga umeahirishwa hadi siku ya jumatatu. BOFYA PLAY KUJUA KILICHOJIRI
Kutuama kwa maji hasa katika maeneo muhimu kwenye magoli ya pande zote mbili ndiyo sababu kuu kwa mwamuzi aliyepangwa kwa mchezo huo Erick Anock kutoka Arusha kusimamisha mchezo huo na kushauriana na kamati husika kisha mchezo kuahirishwa.
Hali katika moja ya lango uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga kufuatia mvua zilizonyesha kwa takriban siku mbili na leo siku iliyopangwa kwa kipute..
Hata mzunguko wa uwanja uko katika hali tete ya tope.
Hata mzunguko wa uwanja uko katika hali tete ya tope.
Kutoka jukwaa kuu na eneo la katikati ya uwanja.
Lango la kaskazini.
Hali halisi dimbani.
Benchi la Simba liko nusu wengine wakitafakari kujumuika.
Kutoka jukwaa kuu muonekano wa uwanja wa Kambarage.
Kufuatia kufariki kwenye ajali ya basi iliyotokea katika eneo la Mkundi nje kidogo ya mji wa Morogoro mnamo April 3 mwaka huu (2015), wanachama saba (7) wa Klabu ya Simba ya Dar es salaam kutoka tawi la Mpira na Maendeleo maarufu kama Simba UKAWA ambalo limewahi kutangazwa kufutwa wakafariki dunia, huu ndiyo ujumbe wa mashabiki wenzao wa Simba tawi la Terminal.
Mashabiki wa Simba tawi la Terminal katika picha ya pamoja ndani ya dimba la CCM Kambarage mara baada ya mchezo kuahirishwa leo.
Mazingira ya nje ya uwanja wa CCM Kambarage hii leo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.