ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 3, 2015

JEMBE FM YAPANIA KUWA SEHEMU YA UCHANGIAJI KATIKA UKUAJI WA MAENDELEO YA JIJI LA MWANZA

Mkurugenzi wa Mtedaji wa Jembe ni Jembe ambaye ni mmiliki wa Jembe FM Radio, Dr. Sebastian Ndege, kwa mara ya kwanza hii leo amezungumza na wakazi wa mkoa wa Mwanza kupitia masafa mapya ya 93.7 Jembe FM kuwakaribisha kuwa sehemu ya familia ya redio hiyo sanjari na kuelezea mipango na mikakati ya kituo hicho. 
Dr. Ndege amesema kuwa Jembe FM imepania kuwa sehemu ya uchangiaji wa ukuaji wa maendeleo ya jiji la Mwanza lenye hazina za kitalii, uvuvi, madini na sekta mbalimbali za uchumi, viwanda biashara kwa kuhakikisha inapenya kihabari na kuainisha changamoto mbalimbali za jamii husika ikiwa ni sambamba na kutoa ushauri kwa nini kifanyike. ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA YALIYOJIRI TANGU AWALI KUPITIA JEMBE FM.

Mkurugenzi wa Mtendaji wa Jembe ni Jembe ambaye ni mmiliki wa Jembe FM Radio, Dr. Sebastian Ndege (kulia) akitambulishwa hewani na moja kati ya watangazaji wa kituo hicho Timoth Ngalula (kushoto). 
Mtangazaji Timoth Ngalula akiendelea kufanya yake at the same time 'Casmir Jembe' akiiba upicture ndani ya 93.7
Kutoka Jembe DjZ ni Dj K-Flip ndiye aliyekuwa akifanya makamuzi. 
Jembe na producer Okeleky.
Kutoka Jembe DjZ ni 
Mikakati mipango na mifano yenye uhalisia.....Dah... watu kwi-kwi-kwi...
Very interesting.....ingawa picha za tukio hili zilipigwa kwa kutumia kamera zisizo na sauti.
Mfano kwa dhati...
Jembe DjZ wamekubali mada.
Wasikilizaji wa kwanza kupiga simukupitia 93.7 Jembe Fm Mwanza ambao walijizawadia zawadi mbalimbali ikiwemo Tshirt za JEMBEKA complimentary za kutinga Jembe Beach katika kusherehekea sikukuu ya Pasaka ambapo msanii wa Bongo Fleva Young Dee sanjari na JJ Band watakisanukisha siku hiyo. Kutoka kushoto ni Alex Richard mkazi wa Kirumba Mwanza, baada ya Dr. Jembe ni Regan Regan Robert mkazi wa Kabuholo Kirumba Mwanza na George Lucas mkazi wa Nyamanolo Mwanza.
Sasa ni wakati wa kula bata @jembenijembe Instagram.
Washkaji wametoka Arusha hadi Mwanza 'KUJEMBEKA' kutoka kushoto ni Fredy Materu, George Albert, Ray, na Bonny wakiwa na rubani wao 'Casmir Jembe' pale kati.
Another one.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.