ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 6, 2015

WANAKIJIJI CHA OLOLOSOKWAN WAIPA AIRTEL HEKO/SHUKRANI

Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto), akizungumza na viongozi wa Kata ya Ololosokwan, wilaya ya Ngorongoro (kutoka kulia), Diwani wa kata hiyo, Yannick Ndoinyo, Mwenyekiti wa kijiji cha Ololosokwan, Kerry Dukunyi na Mjumbe wa Baraza la kijiji hicho, Norkishili Naing’isa, walipomtembelea ofisini kwake katika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kutoa shukrani zao baada ya kampuni hiyo kufunga mnara katika eneo lao na kupelekea urahisi wa mawasiliano ikilinganishwa na hapo awali.
Diwani wa Kata ya Ololosokwan, wilaya ya Ngorongoro, Yannick Ndoinyo, (kulia), akifafanua jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto), wakati baadhi ya viongozi wa kata hiyo, walipomtembelea ofisini kwake katika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kutoa shukrani zao baada ya kampuni hiyo kufunga mnara katika eneo lao na kupelekea urahisi wa mawasiliano ikilinganishwa na hapo awali. Wa (wa pili kulia) ni Mwenyekiti wa kijiji cha Ololosokwan, Kerry Dukunyi na Mjumbe wa Baraza la kijiji hicho, Norkishili Naing’isa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto), akizungumza na viongozi wa Kata ya Ololosokwan, wilaya ya Ngorongoro, walipomtembelea ofisini kwake katika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kutoa shukrani zao baada ya kampuni hiyo kufunga mnara katika eneo lao na kupelekea urahisi wa mawasiliano ikilinganishwa na hapo awali. Wa (pili kushoto) ni Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto), akipata ufafanuzi wa jambo kutoka kwa Mtaalamu wa Mawasiliano wa UNESCO, Al-Amin Yusuph (wa pili kulia), aliyeongozana na baadhi ya viongozi wa Kata ya Ololosokwan, wilaya ya Ngorongoro, walipomtembelea ofisini kwake katika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kutoa shukrani zao baada ya kampuni hiyo kufunga mnara katika eneo lao na kupelekea urahisi wa mawasiliano ikilinganishwa na hapo awali. 

Wengine ni Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), Mwenyekiti wa kijiji cha Ololosokwan, Kerry Dukunyi (wa tatu kulia) na Mjumbe wa Baraza la kijiji hicho, Norkishili Naing’isa

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.