ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, March 26, 2015

WAKAZI ZAIDI 48,100 WAKOSA MAJI SAFI NA SALAMA KWA UZEMBE WA HALMASHAURI KUTONUNUA LUKU YA UMEME.


NA PETER FABIAN, NANSIO.
HALMASHAURI imeshindwa kunua luku ya umeme kwa ajiri ya kuendeshwea mtambo wa kusukuma maji safi na salama na kusababisha wananchina wakazi wa mji wa Nansio wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza kupata adha ya kukosa maji kwa miezi sita sasa.

Hayo yalibainshwa katika taarifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyosomwa kwa Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezwaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia ilani ya uchaguzi 2010 hadi 2015 pamoja na uhai wa chama.

Mtaturu alisema kuwa kutokana na taarifa za kuwepo baadhi ya watendaji wa halmashauri wasio waaminifu a mbao wamekuwa wakitumia nafasi zao kukwamisha utekelezwaji huo ni vyema vikao vya chama vikakaa na kuwaita kisha kuwajadiri na kuwasilisha mapendekezo yao Mkoani.

Awali alipotembelea chanzo cha maji mjini Nansio akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Joseph Mkirikiti na viongozi wa chama hicho ili kujionea tatizo linalosababisha mitambo kushindwa kusukuma maji, ambapo alipewa taarifa fupi na meneja wa Mamlka ya Maji Safi na Salama Edward Joseph aliyeonyesha kushitukizwa na kutakiwa kutoa taarifa na viongozi hao.


 “ tatizo hili limesababishwa na kukosekana kwa umeme wa luku na mamlaka kushindwa kukusanya fedha kutoka kwa wateja jambo ambalo limesababisha kusuasua utolewaji wa huduma ya maji safi katika mji wa Nansio pia wananchi hawana mwamko wa kulipia bili kwa wakati.” Joseph.

Baada ya taarifa hiyo Katibu Mtaturu aliuagiza uongozi wa Mamlaka ya Maji Safi na Halmashauri hiyo kuhakikisha inalekebisha kasoro zilizopo haraka ili wananchi waweze kupata huduma ya maji safi na kuweka mipango mizuri ya ukusanyaji fedha ili kuwezesha uendeshaji wa Mamlaka hiyo.

. Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Mkirikiti, licha ya kuletewa mita za kufungia wateja ili walipe
maji wanayotumia, mamlaka hiyo imeshindwa kufunga mita hizo na kukusanya ankara za maji, hivyo kukosa pesa za kununua umeme na wananchi kubaki wakisotea maji kwa baadhi yao kununua maji shilingi 3,000 kutoka kwenye mkokoteni wenye madumu kumi.

Pia Mkirikiti aliwaagiza Mameneja wa Mamlaka ya Maji Nansio, Tanesco na Mkurugenzi wa halmashauri kukutana naye na kumueleza mikakati ya kutatua kero ya maji haraka iwezekanvyo ili wananchi wa mji huo waanze kupata huduma ya maji safi na salama ndani ya muda uliotolewa na Katibu wa CCM na sitowavumilia watendaji wa serikali watakaoshindwa kutekeleza wajibu wao kwa nafasi zao hapa wiliayani.

Hivi sasa mji wa Nansio wenye wakazi 48,100 wanaopata huduma maji ya bomba ni wakazi 919 tu hali ambayo imelalamikiwa na wananchi wakazi wa Nansio katika mkutano wa hadhara na viongozi hao wa chama na serikali uliofanyika katika viwanja vya stendi ya zamani mjini humo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.