ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 13, 2015

MKAZI WA KOROGWE, TANGA AIBUKA MSHINDI WA MTOKO WA MBUGANI KWENYE FAINALI YA TUTOKE NA SERENGETI

Meneja chapa wa bia ya Serengeti Premium, Bw.Rugambo Rodney, wa pili kulia, akionyesha namba ya simu ya mshindi wa mwisho wa shindano la Tutoke na Serengeti, ambapo Bw. Robert Gabriel mkazi wa Korogwe, Tanga aliibuka mshindi.Msimamizi toka PWC, Golder Kamuzora na (wa pili kulia), Afisa mwandamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha,Bw. Jehud Ngolo (wa kwanza kushoto) Afisa Mauzo toka SBL, Anitha Moshi, (wa kwanza kulia). Droo hiyo iliyofanyika katika baa ya Hongera jijini Dar es salaam.
Mmoja wa washiriki wa droo ya mwisho ya “Tutoke na Serengeti,” Morris Maro wa pili toka kulia akibonyeza kitufe cha laptop kuchezesha droo hiyo wakati wa kumtafuta mshindi wa mwisho wa "Mtoko wa mbugani" katika kampeni ya Tutoke na Serengeti. Droo hiyo ilifanyika Hongera baa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es salaam amapo Bw. Robert Gabriel mkazi wa Korogwe,Tanga aliibuka mshindi. Kwenye picha ni Meneja chapa bia ya Serengeti premium Bw. Rugambo Rodney (wa pili  kushoto), Afisa mwandamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha, Jehud Ngolo (wa kwanza kushoto), na Getrud Mzava*mteja) aliyeitwa kushuhudia, droo hiyo ikichezeshwa kwa haki ndani ya ukumbi wa Hongera baa-Kijitonyama jijini Dar es salaam.
Mateja wa Serengeti Premium Lager, Getrud Mzava ,akitaja namba za simu za mshindi wa mwisho katika droo ya Tutoke na Serengeti wakati wa kumtafuta mshindi wa mwisho wa Mtoko wa mbugani, ambapo mkazi wa Korogwe,Tanga,Bw.Robert Gabriel aliibuka mshindi wa Mtoko wa Mbugani. Droo hiyo ilichezeshwa ndani ya ukumbi wa Hongera-Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Bia chapa ya Serengeti Premium Lager, Bw. Rugambo Rodney, (wa pili kushoto) akiongea kwa njia ya simu na mshindi wa mtoko wa mbugani, Bw. Robert Gabriel mkazi wa Korogwe-Tanga, baada ya kuibuka mshindi wa mwisho wa shindano la Tutoke na Serengeti katika droo iliyochezeshwa ndani ya ukumbi wa Hongera baa-Kijitonyama jijini Dar es salaam.Kulia ni Afisa mwandamizi toka Bodi ya michezo ya kubahatisha, Jehud Ngolo.
Kaimu Meneja chapa wa bia ya Serengeti Premium Bw. Elihuruma Ngowi akiwahudumia baadhi ya wateja walioshiriki wakati wa kumtafuta mshindi wa mwisho  wa Mtoko wa Mbugani wakati droo hiyo ilipochezeshwa ambapo mkazi wa Korogwe-Tanga,Bw. Robert Gabriel aliibuka mshindi wa mwisho wa shindano hilo,lililofanyika katika Baa ya Hongera-Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Wasanii toka SBL wakikonga nyoyo za  washiriki wa Droo ya Tutoke na Serengeti wakati wa kumtafuta mshindi wa mwisho wa “Mtoko wa Mbugani” ambapo Bw.Robert Gabriel toka Korogwe-Tanga aliibuka mshindi wa droo hiyo iliyochezeshwa jana katika Baa ya Hongera iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa washindi wa shindano la Tutoke na Serengeti, Bw.Godfrey Mpiruka aliyeibuka na zawadi ya Limo Bajaji siku za nyuma akiteta jambo na afisa toka SBL wakati wa kuchezeshwa kwa droo ya mwisho ya shindano hilo, lililofanyika katika baa ya Hongera iliyopo-Kijitonyama jijini Dar es salaam.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.