ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 14, 2015

KOCHA SYLVESTER MASH AFARIKI DUNIA

Enzi za uhai wake Marehemu Syvester Mash (kushoto) akipewa maelekezo toka kwa aliyekuwa kocha wa timu ya Tanzania Taifa Stars Kim Poulsen 
Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Sylvester Marsh amefariki dunia alfajiri ya leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako ndiko alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu. 

Kwa mujibu wa Katibu mkuu wa Chama cha soka mkoawa Mwanza MZFA Nasib Mabrouk amethibitisha kutokea kwa msiba huo akisema kuwa ni kipindi zaidi ya mwaka sasa kocha Marsh amekuwa akiugulia na sasa Mwenyezi Mungu ameamua kumpumzisha hivyo amewataka wapenzi wa soka kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu huku akisema kuwa wasubiri taratibu za mazishi na harakati mbalimbali ambazo zitatangazwa baadaye leo mara baada ya kukamilika kwa taarifa kamili.

Zaidi tukutane ndani ya Sports Xtra Clouds Fm kwa taarifa kamili.


R.I.P SYLVESTER MASH

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.