ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 21, 2015

'KING CLASS MAWE' APOTEZA MCHEZO WA KWANZA NAMIBIA

BONDIA IBRAHIMU CLASS ;King Class Mawe' mwenye rekodi ya namba moja nchini Tanzania na ni namba 216 kwa Dunia  amepoteza mpambano wake wa kwanza nchini namibia kwa kupigwa kwa pointi na bondia Julius Indongomwenye rekodi ya Namibia na namba moja na duiani ni namba 76 kwa ubora.
 Mpambano uho uliofanyika march 20 Windhoek Country Club Resort, Windhoek, Namibia
ulianza kwa kasi ya ajabu ambapo bondia Class alimkalisha chini Indongo na kuhesabiwa na mpambano kuendelea kwa mashambulizi ya zamu kwa zamu kila upande
hata hivyo mpaka mwisho wa mchezo Class alipoteza mpambano uho kwa point

Mpambano huu ni wa pili kwa Class kucheza nje ya nchi baada ya ule wa kwanza kupigana nchini Zambia mwaka jana na kurudi na ubingwa wa WPBF Africa

Kabla ya kuchaguliwa kwenda kupigana nchini Namibia Class alimdunda bondia Cosmas Cheka na kunyakuwa mkanda wa U.B.O Africa na kumfanya amiliki mikanda miwili ya Africa mpaka sasa 

Mpambano huu anaupoteza baada ya miaka mitano iliyopita kuwapiga mabondia mbalimbali Class anaenolewa na jopo la makocha linalongozwa na Habibu Kinyogoli 'Masta' Kondo Nassoro pamoja na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye umpa ushauli anapokuwa uringoni jinsi ya kukabiliana na mpinzani anaecheza nae

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.