ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 21, 2015

KENYA AIRWAYS YAPUNGUZA SAFARI ZAKE TZ

CHANZO/BBC SWAHILI
Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways leo limeanza rasmi kupunguza safiri zake katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam kufuatia agizo la mamlaka ya anga ya Tanzania kuamuru shirika hilo kupunguza safari zake kutoka 42 kwa wiki hadi 14.
Serikali ya Tanzania inasema huo ndio mkataba wa tangu awali na kulaumu mamlaka ya anga nchini Kenya kwa kushindwa kuafikia maelewano na mamlaka ya Tanzania kuhusu jambo hilo.
Tayari baadhi ya wasafiri wanaotumia ndege za shirika hilo wameanza kuathirika kufuatia shirika hilo kufuta baadhi ya safari kutoka Dar es Salaam

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.