ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, March 5, 2015

ALBINO WAZUSHA VURUGU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

Viongozi wa Chama Cha Albino Tanzania wakiwasili Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 5, 2015 kuonana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliyewakaribisha ili kuwasikiliaza matatizo yao na kujadiliana nao mikakati ya namna ya kukomesha ukatili na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini​. Hata hivyo mkutano huo baadaye uliingia dosari. 
CHANZO:BBC SWAHILI
Vurugu zilizofanywa na baadhi ya walemavu wa ngozi Albino katika Ikulu ya Tanzania zimesababisha kuahirishwa kwa kikao kati ya viongozi wao na Rais Jakaya Kikwete.
Rais Kikwete alikuwa akitarajiwa kufanya mkutano na viongozi wa Albino Tanzania TAS aliowaalika kuzungumzia hoja zao kutokana na mauaji ya walemavu hao yanayoendelea nchini humo.
Lakini heka heka iliyotokea katika eneo la mapokezi iliwalazimu maafisa wa Ikulu kuwatawanya walemavu hao.
Ni muda mfupi baada ya ukaguzi kuanza kufanyika katika moja ya lango la kuingilia Ikulu,kundi moja la walemavu hao waliokuwa katika moja ya chumba wakaanzisha malalamiko kwa sauti huku viongozi wao wakiwa wanajiandaa kuruhusiwa na kuingia ndani.
Kelele hizo na mabishano hayo miongoni mwa walemavu hao kwa mbali ikaanza kuonekana ni dosari namba moja hasa baada ya kupandisha mori na kila mtu kuanza kusema lake kupinga ushiriki wa viongozi hao
Kutokana na vurugu hizo maafisa wa Ikulu waliwatawanya Walemavu hao kutoka nje ya Geti , na hapo ikawa mwanzo wa sakata jipya baada ya kuanza kulumbana na viongozi wao na hatimaye kuanza kupigana na mambo yakawa hivi.Baada ya kutulizwa ugomvi kilichofuata ni nyimbo za kupinga uhalali wa viongozi wao
Hata hivyi vurugu hizi zinatazamwa tofauti na baadhi ya walemavu hao,ambao wanasema ni vurugu hizo zimepoteza fursa ya kuwasilisha matatizo yao kwa Rais.
RAIS AKUTANA NA UONGOZI WA CHAMA CHA ALBINO TANZANIA
 IKULU JIJINI DAR 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na viongozi wa Chama Cha Albino Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo. Walioketi kushoto ni Waziri wa Sheria na Katiba Dkt Asha Rose Migiro, Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Mathias Chikawe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe George Mcheche Masaju Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabirika Mushi na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bw. Emmanuel Achayo 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifafanua jambo wakati akiongea na viongozi Wa Chama Cha Albino Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na viongozi Wa Chama Cha Albino Tanzania baad ya kukutana nao pamoja na Waziri wa Sheria na Katiba Dkt Asha Rose Migiro, Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Mathias Chikawe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe George Mcheche Masaju Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabirika Mushi na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bw. Emmanuel Achayo Ikulu jijini Dar es salaam leo. PICHA NA IKULU

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.