ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 20, 2015

AIRTEL YAMTANGAZA BINGWA WA AIRTEL TRACE MUSIC YAMZAWADIA MILIONI 50TZS

Meneja Masoko wa Airtel Aneth Muga (kushoto) akimkabidhi mshindi wa Airtel Trace Music Stars Nalimi Mayunga hundi ya mfano yenye dhamani ya sh. 50mil baada ya kuibuka mshindi wa mashindano ya Airtel Trace Music Stars, pia atapata fursa ya kwenda kuiwakilisha nchi yetu katika mashindano ya Airtel Trace Stars ya Afrika yatakayofanyika Mjini Nairobi Kenya mwezi machi, anaeshuhudia ni Afisa Uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki.
Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Nalimi Mayunga akifurahia zawadi yake baada ya kuibuka mshindi wa mashindano hayo yaliyofanyika hivi karibuni. Mshindi huyo pia atapata fursa ya kwenda kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Airtel Trace Stars ya Afrika yatakayofanyika Mjini Nairobi Kenya mwezi machi,
Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Nalimi Mayunga (kati) akiwaimbia waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika hafla ya makabidhiano ya zawadi yake hundi ya sh. Milioni 50 kushoto yake ni Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki (kushoto) na Meneja Masoko wa Airtel Aneth Muga (kulia). Press Release Airtel yamtangaza Bingwa wa Airtel Trace Music, yamzawadia milioni 50TZS

* Nyota wa Airtel Trace Music Stars apatikana Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel leo imemtangaza rasmi mshindi wa shindano la Airtel Trace Music star, shindano lilidumu kwa muda wa miezi mitatu maalum kwa wasanii chipukizi kuweza kuimba na kutuma nyimbo zao kwa kutumia simu zao za mkononi kama studio kwa lengo la kusaka na kuibua vipaji kwa wanamuziki chipukizi nchini.

Akiongea na waandishi wa habari Meneja Masoko wa Airtel Aneth Muga alisema"Leo tunayofuraha kubwa kumtangaza mshindi wetu wa shindano la Airtel Trace Music Stars mara baada ya kuchaguliwa na majaji na kupigiwa kura na watanzania "Washiriki watano ni kati ya wengi waliothubutu kuonyesha uwezo wao wa kushiriki kwa kupiga simu, kuimba na kutuma nyimbo zao na hatimae majaji wamesikiliza vipaji vyao kama walivyoimba na kuwachagua kuingia tano bora (top 5)" alifafanua Muga.

Washiriki waliokuwa wamebahatika kuingia tano bora ni Nalimi Mayunga mwenye namba ya ushiriki (55100182), Christopher Kihwele (5510050), Tracy Eminence (55100420), Beautus Henry (55100106) na Rose Mbuya (55100366) Mshindi wetu ni Nalimi Mayunga mwenye namba ya ushiriki (55100182) ambae amechaguliwa na majaji wetu pamoja na kupigiwa kura nyingi na wananchi Zawadi yake ni milioni Tshs 50mil, na pia atapata fursa ya kwenda kuiwakilisha nchi yetu katika mashindano ya Airtel Trace Stars ya Afrika Nairobi Kenya yanayoshirikisha nchi 13 barani Afrika ambapo pia mshindi atakaepatikana atarekodiwa nyimbo zake katika studio za kimataifa nchini uingereza, na kupewa mafunzo toka kwa msanii nguli wa Afrika Akon.

Nchi nyingine zinazoshiriki mashindano haya na zitakazotoa jumla ya vijana 13 barani Afrika ni pamoja na Kenya, Uganda Zambia, Madagascar, Malawi, Nigeria, Ghana, Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, The Democratic Republic of Congo (DRC), na Gabon

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.