ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, February 19, 2015

AIRTEL YAMKABIDHI MKAZI WA KYELA MBEYA BWANA EDOM MWANSASU GARI LAKE

Kamanda mkuu wa polisi wa Mkoa wa Mbeya Bwana Hemed Msangi (wa pili kulia)  akimkabithi mshindi wa gari aina ya Toyota IST bwana Edom Dickson Mwansasu  mkazi wa Kyela Mbeya baada ya kuibuka moja kati ya washindi wa wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi. pichani kushoto ni mke wa Edom Mwansasu na kulia ni Meneja biashara wa Airtel  Nyanda za juu kusini Bwana Straton Mushi.
Mshindi wa gari aina ya Toyota IST bwana Edom Dickson Mwansasu  akiwasha gari mara baada ya kukabithiwa gari lake baada ya kuibuka moja kati ya washindi wa wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi.

mshindi wa gari aina ya Toyota IST bwana Edom Dickson Mwansasu  akiwa ndani ya gari pamoja na mke wake baada ya kukabithiwa gari lake kufatia kuibuka kuwa mshindi wa wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi katika droo iliyofanyika ijumaa iliyopita.

Airtel yamkabithi Mkazi wa Kyela Mbeya Bwana Edom Mwansasu gari Lake
·         Baada ya kuibuka kuwa moja kati ya washindi wa wiki ya pili ya Airtel Yatosha Zaidi
Mkazi wa kyela mkoani Mbeya Bwana Edom Dickson Mwansasu amekabithiwa gari aina ya Toyota IST na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel mara baada ya kuibuka mshindi kupitia droo ya wiki ya pili ya promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi iliyofanyika siku ya ijumaa iliyopita
Bwana Edom Mwansasu mwenye umri wa miaka 40 anajishughulisha na shughuli za kilimo huko Ngonga Kyela  Mkoani Mbeya  ameibuka mshindi baada ya kununua na kujiunga na  vifurushi vya siku vya huduma ya Airtel yatosha kila siku.
Akiongea baada ya kukabithiwa gari bwana Edom Mwansasu alisema ninafuraha sana kuwa mshindi  na kutumiza ndoto yangu ya kumiliki gari.  Nilipopigiwa simu sikuamini kuwa nimeshinda gari , nilifurahi sana nakupasha habari kwa familia yangu. Sijawahi kumiliki gari hivyo najisikia furaha sana Airtel kunizawadia mimi hii gari kupitia hii promosheni ya Airtel yatosha. Kwa kupitia gari hili sasa na uhakika wa usafiri mimi pamoja na familia yangu lakini pia litanisaidia katika kazi yangu ya kilimo na kuniwezesha kusafirisha mazao yangu kirahisi ukilinganisha na  awali nilikuwa natumia baskeli au kukodi gari.
‘Nawapongeza sana Airtel na nawashauri watanzania kuendelea kutumia huduma ya Airtel yatosha na kuamini kuwa nao wanaweza kubahatika na kushinda kama mimi” aliongeza Mwansasu
Kwa upande wake Kamanda mkuu wa polisi wa Mkoa wa Mbeya Bwana Hemed Msangi alisema”  kwanza kabisa napenda kuwapongeza Airtel kwa kuanzisha promosheni hii kabambe inayowawezesha watanzania kutoka sehemu mbalimbali kujishindia magari.  Naamini kwa kupitia promosheni hii mtawawezesha watanzania wengi kujikwamua kiuchumi na kuwawezesha kufanya shughuli zao za kijamii na kiuchumi kirahisi na kwa ufanisi zaidi. Nawapongeza washindi wote waliopatikana mpaka sasa.  Lakini natumia fulsa hii kuwaomba wananchi wadumishe amani maana kama sio amani tulionayo basi promosheni kama hizi zisingeweza kufanyika”
Akiongea kwa niaba ya Airtel Meneja biashara wa Nyanda za juu kusini Bwana Straton Mushi Alisema”  promosheni hii ya Airtel yatosha zaidi ni mahususi kwa wateja wetu Tanzania nzima wanaotumia huduma hii ya Airtel Yatosha kuweza kujishindia gari aina ya Toyota IST kila siku .  kujiunga na vifurushi vya Airtel yatosha mteja anatakiwa kupiga *149*99# au kwa kununua vocha vya Airtel yatosha au kununua kupitia huduma ya Airtel Money na kuunganishwa moja kwa moja kwenye droo itakayomwezesha kushinda.
Mpaka sasa washindi 10 wamepatika ambapo kati yao wawili wanatoka kanda ya nyanda za juu kusini na leo tunamkabithi mshindi wetu wa Mbeya Bwana Edom Mwansansu gari lake na kisha tutamkabithi mshindi wa mkoa wa sumbawanga bwana Saidi Mashiko ambaye ni mganga wa tiba za jadi na mkazi wa Katavi hivi karibuni”
“Natoa wito kwa watanzania na wateja wetu kujiunga na vifurushi hivi vya Airtel yatosha na kupata nafasi ya kujishindia gari aina ya Toyota IST kila siku”. Aliongeza Mushi
Washinde wengine waliojishindia Toyota IST toka promosheni hii ianze ni pamoja na Ramadhani Dilunga mkazi wa Pwani, Namtapika Kilumba Mkazi wa Mtwara, said Mashiko mkazi wa katavi, Hamim Yoyo mkazi wa Korogwe Tanga, Esther Mashauri Mkazi wa Mwanza, Ibrahim Kimondo mkazi wa Kondoa pamoja na Mwajabu Churian, Sakina Libwana na Justin Wilium wote wakazi wa Dar

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.