ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, January 29, 2015

ALI KIBA AMTAMBULISHWA RASMI SAUTI ZA BUSARA

Mwenyekiti wa Bodi wa Busara Promotions, wandaaji wa tamasha la Sauti za Busara, Simai Mohammed (katikati) akiongea na wandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wanahabari Jijini Dar es Salaam, juu ya tamasha la 12 la Sauti za Busara, litakalofanyika, Februari 12 hadi 15, mwaka huu, Ngome Kongwe, Zanzibar. Wengine (kushoto) ni Meneja wa tamasha hilo, Journey Ramadhani. na upande wa kulia ni Mkurugenzi wa tamasha hilo, Yusuf Mahmoud 'Dj Yusuf, akifuatiwa na msanii wa bongo fleva nchini, Ali Kiba (kulia).
Simai, Dj Yusuf na Kiba wakiwa wameunganisha mikono kwa kusalimiana ikiwa ni ishara ya Umoja na Amani, kama Kauli mbiu ya mwaka huu ya tamasha hilo inavyohimiza amani.
Ali Kiba katika 'Selfie' na Mwenyekiti wa Bodi ya Busara Promotions, Simai Mohammed, muda mfupi baada ya utambulisho wa msanii huyo juu ya kupiga shoo kwenye tamasha la 12 la Sauti za Busara, litakalofanyika Februari 12 hadi 15, Zanzibar.

Ali Kiba ahidi makubwa Sauti za Busara Februari 12
Ali Kiba atamba kufanya kweli Sauti za Busara mwaka huu
Ali Kiba kupiga shoo ya 'live' Sauti za Busara Feb 12

Na Andrew Chale
Mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ali Kiba ametamba kukonga nyoyo watu mbalimbali watakaojitokeza kwenye tamasha la 12 la Sauti za Busara linalotarajia kufanyika, Februari 12 hadi 15, Ngome Kongwe, Zanzubar.

Ali Kiba alieleza hayo leo Alhamisi, Januari 29. wakati wa mkutano wa ulioandaliwa na Busara Promotions, wandaaji wa tamasha hilo kubwa la Kimataifa linalofanya muziki wa 'Live',  ambapo kwa mwaka huu zaidi ya wanamuziki na vikundi 37, watatoa burudani kwenye tamasha hilo kwenye viunga vya Ngome Kongwe, Unguja, Zanzibar.

Akizungumza mbele ya wandishi wa habari, Ali Kiba alisema kwa sasa amejiandaa kutoa burudani ya aina na ambayo itakonga nyoyo kwa watu wote watakaojitokeza kushuhudia tamasha hilo.

"Hii itakuwa ni zawadi kwa watanzania wote kunishuhudia nikiimba 'live' bila kutumia 'cd' kama wafanyavyo wengine. Mimi ni mwanamuziki na nimesoma muziki hivyo nitapiga muziki wa nguvu jukwaani" alisema Ali Kiba.

Na kuongeza kuwa, kwa sasa yupo kwenye mazoezi ya muda mrefu wa kujifua na bendi maalum  kwa ajili ya shoo hiyo huku akitamba kuwa, yeye ni msanii kwani muziki aliusomea na kujifunza huko nyuma alipokuwa  katika Nyumba ya kuibua vipaji THT, ambapo alijifunza vitu vingi ikiwemo kuimba muziki wa bendi na 'live'.

Aidha, aliwaomba wapenzi na wadau wa muziki kujitokeza kwa wingi 

kushuhudia tamasha hilo kwani wasanii mbalimbali wa ndani na nje watatoa burudani ya kipekee.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya Busara Promotion, wandaaji wa tamasha hilo, Simai Mohammed, alisema tamasha limeweza kuongeza ajira na uchumi wa Zanzibar kwani pia limeongeza fursa za utalii.

Kwa upande wake, Meneja wa tamasha  hilo, Journey Ramadhani, alisema tamasha hilo limeweza kuongeza fursa kila mwaka ikiwemo kutoa ajira kwa vijana wa kitanzania kwa asilimia 90, ambapo kwa mwaka huu wanatarajia kuwa na watendaji kazi na wa kujitolewa watakolipwa katika kusaidia tamasha hilo, zaidi ya watu 150.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa tamasha hilo, Yusuf Mahmoud 'Dj Yusuf' alisema tamasha hilo limeweza kuibua wasanii mbalimbali ikiwemo kujitangaza kimataifa.

Aidha, Dj Yusuf alieleza kuwa, tamasha la mwaka huu litaendana na kauli mbiu ya kuimiza Amani, pia wameandaa tuzo maalum na zawadi maalum kwa wasanii wa Tanzania watakaoshinda katika kutunga nyimbo za amani.

Mbali na Ali Kiba, Wasanii wengine Isabel Novella kutoka  Msumbiji, Ihhashi Elimhlophe (Afrika Kusini),   Tcheka (Cape Verde),   Diabel Cissokho (Senegal),  Culture Musical Club (Zanzibar),  Msafiri Zawose (Tanzania),   Aline Frazão (Angola),   Tsiliva (Madagascar),   Leo Mkanyia and the Swahili Blues Band (Tanzania),   Mohamed Ilyas & Nyota Zameremeta (Zanzibar),   Thaïs Diarra (Senegal / Mali / Uswisi),   Liza Kamikazi and band (Rwanda),   Erik Aliana (Cameroon),  Mpamanga (Madagascar),   Mgodro Group (Zanzibar),   Rico Single & Swahili Vibes (Zanzibar),   Zee Town Sojaz (Zanzibar),   Ifa Band (Tanzania) na wengine wengi. Maelezo zaidi yanapatikana katika www.busaramusic.org

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.