ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 30, 2015

AIRTEL YATANGAZA TANO BORA YA SHINDANO LA AIRTEL TRACE MUSIC STARS

Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza majina ya washiriki walioingia 5 bora katika mashindano ya Airtel Trace Music Stars , akishuhudia Meneja Masoko wa Airtel Bi Anethy Muga
Meneja Masoko wa Airtel Bi Anethy Muga akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza majina ya washiriki walioingia 5 bora katika mashindano ya Airtel Trace Music Stars akishuhudia
Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki waliongia 5 bora katika mashindano ya kuvumbua vipaji vya mziki ya Airtel Trace Music Strars . finali za mshindano hayo zinategeme kufanyika mwanzoni mwa mwezi wa pili kulis ni  Meneja Masoko wa Airtel Bi Anethy Muga
  Press Release
 Airtel yatangaza tano bora ya shindano la Airtel Trace Music Stars * Mshindi wa Airtel Trace Music kupatikana katika Finali itakayofanyika tarehe 7 februari Kampuni ya simu ya mkononi leo imetangaza washiriki walioingia tano bora katika shindano la Airtel Trace Music star shindano lenye lengo la kusaka na kuibua vibaji kwa wanamuziki chipukizi.

Shindano hilo lililozinduliwa rasmi mwaka jana Oktaba limefika katika hatua za fainali ambapo mshindi wa Airtel Trace Tanzania atapatikana katika finali inayotegemea kufanyika mwanzoni mwa mwenzi wa pili mwaka huu ambapo mshindi huyu ataenda kushiriki mashindano ya Airtel Trace Music Stars Afrika yatakayoshirikisha washiriki wengine kutoka nchi 13 barani Afrika

Akiongea na waandishi wa habari Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga alisema" leo tunayofuraha kubwa kutangaza majina ya washiriki waliofanya vizuri katika mashindano haya na kupata nafasi ya kuingia katika tano bora na kuweza kumpata mmoja kati yao atakaeibuka na ushindi wa kuiwakilisha nchi yetu katika mashindano ya Airtel Trace Afrika".

 Akiendelea kufafanua Aneth alisema "Washiriki hawa watano ni kati ya wengi waliothubutu kuonyesha uwezo wao wa kushiriki kwa kupiga simu, kuimba na kutuma nyimbo zao na hatimae majaji wamesikiliza vipaji vyao kama walivyoimba na kuwachagua kuingia tano bora (top 5), sasa kura nyingi toka kwa watanzania ndio itakayomuwezesha mmoja wao kupata uhindi wa kwanza wa Airtel Trace Tanzania.

Mashindano haya yanalengo la kuinua vibaji vya musiki kwa vijana wetu kuzifikia ndoto zao na kuwawezesha kuonyesha vipaji vyao ndani na nje ya nchi. Airtel tunajisikia furaha kuwa sehemu ya mafanikio yao na sehemu ya kuinua vipaji vya wanamuziki chipukizi kwa kupitia mashindano haya ya Airtel Trace Music Stars.

Napenda kuwapongeza na kuwatia hamasa wale wote walioshiriki na pia hawa waliofanya vizuri na kufika katika hatua hii muhimu ya mashindano haya. Akitangaza majina ya walioibuka kwenye tano bora Meneja Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando alisema " tunawashukuru watanzania na wanamuziki chipukizi kwa kushiriki katika shindano hili na mpaka sasa tunaovijana wengi waliojaribu kuonyesha uwezo wao wa kuimba, lakini kama mnavyofahamu haya ni mashindao hivyo napenda kuwaleta kwenu wale waliofanya vizuri zaidi na kuingia katika hatua hii ya mchuano mkali .

Waliobahatika kuingia tano bora ni pamoja na Nalimi Mayunga mwenye namba ya ushiriki (YUN), Christopher Kihwele (TOJ), Tracy Eminence (MHR), Beautus Henry (BOB) na Rose Mbuya (ROS) Natoa wito kwa watanzania , wadau mbalimbali na wapenzi wa muziki kuwapigia kura washiriki hawa kwa kupiga kutuma sms yenye jina la fumbo la mshiriki kwenda kwenye namba 15594

Hii ni nafasi ya pekee kwa watanzania kuonyesha uwezo na vipaji vyao katika anga za Afrika hivyo ni matumaini yetu kuwa washiriki hawa watajifua vyema ili kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika pindi mshindi atakapo patikana.

Akiongea mara baada ya kutangaza kuwa moja ya tano bora Christopher Kiwhele alisema" najisikia furaha sana kupata nafasi hii ya kuwa moja ya tano bora, kwakweli kwangu ni kama ndoto, siamini kama nimeweza kufudhu ma kufika katika hatua hii kubwa, na amini ntaendelea kufanya vizuri kwani naendelea kujiandaa vyema, nimetamani sana kuwa mwimbaji nyota na mwimbaji anayenivutia zaidi ni Ed sheeran naamini kupitia mashindano haya ntafika mbali na kutumiza ndoto zangu.

Nawaomba watanzania watuunge mkono na kutupigia kura ili kuendelea kufanya vizuri na hatimae kuwakilisha nchi yetu vyema katika mashindano ya Afrika. Washiriki tano bora wa Airtel Trace music Star sasa wako kambini ambapo wanapata mafunzo yatakayoendelea hadi fainali inayotegeme kufanyika tarehe 7 mwenzi wa pili 2015 jijini Dar es saalam.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.