ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 8, 2014

STAND UNITED YAONA MWEZI YAIGONGA 1-0 MBEYA CITY DIMBA LA CCM KAMBARAGE.

Kwa mara ya kwanza ikicheza nyumbani Stand United hii leo imeonja utamu wa ligi kuu soka Tanzania bara mara baada ya kupata ushindi wake wa kwanza ndani ya ligi hiyo kwa kuifunga Mbeya City 1-0 mchezo ukichezwa dimba la CCM Kambarage mjini Shinyanga.
Mashabiki wa Mbeya City walikuwa na mbwembwe kiasi cha kuliweka kiganjani dimba hilo nao mashabiki wa Stand wakiwa kama wamenyeshewa mvua kwa muda wa takribani dakika 45 za kipindi cha kwanza na dakika kama 15 za kipindi cha pili lakini mambo yalibadilika baada ya hapo furaha yao ikageuka kuwa kilio.
Mbwembwe mwanzo mwisho...lakini mwisho wa mchezo Mbeya City wanatoka vichwa chini...
Dakika ya 76 Shangwe za mashabiki wa Stand United zatawala safari hii zikiwa na maana zaidi baada ya mshambuliaji wa timu hiyo Chibibiere Abisalum, ambaye ni raia wa Nigeria kupasia mpira kambani akipokea pande safi toka kwa Musa Said Kimbu aliye wapunguza mabeki wa Mbeya City.
ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA YALIYOJIRI:-

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA MAHAKAMA YA KIMBARI YA RWANDA ICTR ARUSHA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye Maadhimisho ya miaka 20 ya Mahakama ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), ulioanza leo Novemba 8, 2014 kwenye Ukumbi wa AICC Jijini Arusha. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitazama baadhi ya picha za kumbukumbu za Mahakama ya Kimbari zilizo katika ukumbi huo wakati akiondoka baada ya kufungua rasmi Mkutano wa Maadhimisho ya miaka 20 ya Mahakama ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda ICTR, ulioanza leo Novemba 8, 2014 kwenye Ukumbi wa AICC Jijini Arusha. Picha na OMR
Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano huo wakimsikiliza makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia. Picha na OMR
Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano huo wakimsikiliza makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia. Picha na OMR
Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano huo wakimsikiliza makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wa mkutano huo wa maadhimisho ya miaka 20 ya Mahakama ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), ulioanza leo Novemba 8, 2014 kwenye Ukumbi wa AICC Jijini Arusha. Picha na OMR

HATIMAYE MISS TANZANIA 2014 SITTI MTEMVU ALIVUA RASMI TAJI, MSHINDI NAMBA MBILI AULA.

Taarifa tunazozipata sasa hivi kupitia Breaking News ya Clouds Fm iliyotoka katika kipindi cha Club 10 na Wewe, inasema kuwa Miss Tanzania 2014-2015 Sitti Mtemvu ameamua kulivua taji hilo rasmi mara baada ya kuandamwa sana na vyombo mbalimbali vya habari sambamba na mitandao ya kijamii.

Mpango huo wa kulivua taji utamnufaisha mshindi wa pili Lillian Kamazima, ambaye ndiye atakaye kuwa mrithi wa Taji hilo sanjari na zawadi zitakazo rudishwa na Sitti.

Taarifa hizo zinaendelea kusema kuwa mnyange huyo hivi sasa yuko katika ukumbi wa JB Belmonte jijini Dar es salaam akikamilisha hatua hiyo ambayo ni kwa mara ya kwanza imetokea ndani ya Historia ya Miss Tanzania.. (ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA) ITAENDELEA....
TOP 3: Mrembo, Sitti Abbas Mtemvu, akiwa katika picha ya pamoja na Mshindi wa pili, Lillian Kamazima (kulia) na Mshindi wa Tatu, Jihhan Dimachk, baada ya kutawazwa rasmi kuwa washindi katika shindano la Taifa lililofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam,. Mrembo huyo ambaye ni binti wa Mbunge wa Temeke, pia ni Miss Temeke Abbas Mtemvu alitokea  Kitongoji cha  Chang'ombe hii leo ametangaza kulitema taji hilo.

HABARI HII TAENDELEA HIVI PUNDE.......

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA IJITIMAI YA KIMATAIFA MJINI MOROGORO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi semina ya mafunzo ya Kiislamu (IJITIMAI) iliyofunguliwa jana Novemba 7, 2014 kwenye Msikiti wa Jabalhira, mjini Morogorogo. Picha na OMR 
Sehemu ya waumini wa dini ya kiislam waliohudhuria hafla hiyo ya ufunguzi wa  IJITIMAI, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakati akiondoka baada ya kufungua rasmi IJITIMAI hiyo katika msikiti wa Jabalhira, mjini Morogorogo. Picha na OMR 

MPINA ATAKA POSHO ZA WABUNGE ZILIPE DENI MSD KUOKOA MAISHA YA WATANZANIA

Mbunge wa Jimbo la Kisesa Luhaga J. Mpina (kulia) akikabidhi mashuka kwa hospitali ya Wilaya ya Meatu kwa Mkurugenzi wa wilaya hiyo Isaya M. Moses. PICHA kwa hisani ya maktaba yetu 2012. 
SAKATA la ukosefu wa dawa katika hospitali zote za umma limetikisa Bunge baada ya Mbunge wa Jimbo la Kisesa(CCM), Luhaga Mpina kutaka bunge hilo liahirishwe ili fedha zinazotumika kuwalipa posho zikusanywe ziende kununua dawa kuokoa maisha ya watanzania wanaokufa kila siku kwa kukosa dawa.
Hatua hiyo ya Mpina ilikuja kufuatia maelezo yaliyotolewa na Serikali kuwa inakwenda kukaa kikao cha kujadili suala hilo majibu ambayo hajakumridhisha mbunge huyo.
Mpina ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Uchumi,Viwanda na Biashara alisema watanzania wanaendelea kupoteza maisha huku Serikali ikiendelea kulifanyia mzaha jambo hilo nyeti.
Alisema wakati wa vikao vya kamati za Bunge vilivyokaa Dar Es Salaam wiki mbili zilizopita, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, Margareth Sitta na kamati yake waliitaka Serikali ilipe deni ya Sh.bilioni 100 linalodaiwa na Bohari Kuu ya Dawa(MSD) ili kunusuru vifo vya wananchi wanyonge bado Serikali imeendelea kusuasua katika jambo hilo.
Hata hivyo Mpina alielezea kusikitishwa kwake na Serikali kushindwa kutaja waliohusika kuiba sh.bilioni 37 za kununulia dawa huku pia ikishindwa kutaja hatua ilizochukua dhidi ya watu hao.
Kufuatia hali hiyo alimba Mwongozo kwa Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai kukubali kuahirisha mkutano wa 16 na wa 17 wa Bunge hilo ili fedha zilizokuwa zitumike kulipana posho zipelekwe haraka MSD kulipa deni hilo ili kunusuru maisha ya wananchi wasio na hatia wanaondelea kufariki kwa kukosa dawa.
Alisema hospitali zote za Umma zinakabiliwa na ukosefu wa dawa huku kwenye jimbo la Kisesa ikikosekana hata dawa aina ya Oral ya kuzuia kuharisha kwa watoto wachanga ambao nao wanapoteza maisha kwa kukosa dawa hiyo.
"Mheshimiwa Naibu Spika leo Serikali inasema inaenda kukaa kikao wakati hospitali nchi nzima hazina dawa watu wanakufa kwa kukosa dawa,kwa kuwa Serikali imeshindwa kutatua tatizo hili basi mkutano wa 16 na 17 wa Bunge hili liahirishwe ili fedha hizi zitumike kununua dawa zikatibu wananchi hawa waokufa bila dawa" alisema Mpina.
Kufuatilia mwongozo huo, Naibu Spika Ndugai alisema hoja hiyo ya Mpina ni nyeti na kwamba itajadiliwa kwenye Kamati ya uongozi ili kufanya uamuzi.
'Mh Mpina hoja yako ni nzito sasa itabidi ipelekwe kwenye kamati ya uongozi itakayokutana leo jioni (jana) ili kulijadili na kulifanyia uamuzi"alisema Ndugai.
Katika hatua nyingine Mbunge wa Kigoma Kusini(NCCR-Mageuzi), David Kafulila ameliomba bunge kujadili suala la ufisadi wa IPTL kutokana na unyeti wa suala hilo baada ya Serikali kuonekana kuikalia ripoti hiyo isiwasishwe bungeni.
"Mheshimiwa Naibu Spika naomba bunge lako likubali tusimamishe shughuli zote za bunge tujadili suala hili la IPTL ambalo limesababisha wafadhili kukatisha misaada yao na kuathiri mwenendo wa shughuli za Serikali"alisema Kafulila.
Baada ya Kafulila kuomba mwongozo huo, Mnadhimu wa Shughuli za Serikali bungeni, William Lukuvi alisema uchunguzi wa suala la IPTL bado unaendelea kufanywa na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali(CAG) na kwamba utakapokamilika ripoti hiyo itawasilishwa bungeni.
Lukuvi ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu wa Bunge alisema taarifa alizonazo uchunguzi wa CAG uko kwenye hatua za mwisho na kwamba utakapokamilika utawekwa wazi.
Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba alimtaka Naibu Spika aruhusu kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza suala hilo.
Ndugai alisema hoja ya kuundwa Kamati teule nayo itawasilishwa kwenye kikao cha kamati ya uongozi ya Bunge kujadiliwa.
Naye Mbunge wa Nzega(CCM), Dkt. Khamis Kigwangala aliomba mwongozo kuhusu kauli iliyotolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga kuhusu baadhi ya Kamati za kutojua mipaka yake.
Kingwangala alimtaka Naibu Waziri huyo kufuta kauli yake bungeni kwani inaweza kuathiri utendaji wa Kamati za Bunge kwa kufanya ionekane hazijui majukumu yake na kusababisha maagizo na ushauri inayokuwa inatoa kuonekana pia ni batili.
Hata hivyo Ndugai alilitolea ufafanuzi suala hilo na kusisitiza kuwa Kamati za Bunge ziko kusheria na zitaendelea kutelekeza majukumu yake bila kuingiliwa na mihimili mingine ya dola.

Friday, November 7, 2014

KILA IJUMAA SKYLIGHT HUKISANUKISHA NAMNA HII @THAI VILLAGE MASAKI DAR.

DSC_0154
Sam Mapenzi;……Kuna Watu Hatari, Wenye Mapenzi Zenye Siri Kali,…Letu Nalo Lina Jua Kali, Penzi Letu Serikali,….Wajua Nakupenda, Malaika…..Aneth Kushaba;…..I’m Going Koo Koo Koo, So Koo Koo Coz I, I, Love You, (Aiyayaaaaa)….I’m Going Koo Koo Koo, So Koo Koo Coz I, I Love You,….(Aiyayaaaaa)…Hizi zote utazipata Skylight Band si kwingine...tukutane baadaeeee!
DSC_0225
Majembe ya Skylight Band yakitoa burudani ya kukata na shoka kwa mashabiki wao Ijumaa iliyopita ndani ya ukumbi wa Thai Village Masaki jijini Dar..Kutoka kushoto ni Aneth Kushaba AK47, Mkongwe wa muziki wa dansi Joniko Flower, Sony Masamba a.k.a Fally Ipupa wa bongo, Digna Mbepera na Sam Mapenzi.
DSC_0242
Kikosi kazi cha Skylight Band kikiongozwa na rapa Joniko Flower kutoa burudani kwa mashabiki wake (hawapo pichani) Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha maraha cha Thai Village Masaki jijini Dar.

DSC_0244
Kutoka kushoto ni Aneth Kushaba AK47, Sony Masamba, Bela Kombo, Sam Mapenzi na Digna Mbepera wakijibu mapigo ya mashabiki wa Skylight Band kwa staili ya aina yake.
DSC_0254
Mashabiki wa Skylight Band wakijibu mapigo kwa staili ya "Yachuma chuma"...Muguu wa kushoto mbele wa kulia nyuma, Yachuma chuma nataka mukanda Yachuma chuma....raha iliyoje unakosaje sasa, fanya uje tukutane pale kati.
DSC_0255
Na huku nako hawavumi lakini wamo kama inavyoonekana pichani.
DSC_0261
Wadau nao wakaendelea kujiachia......Asanteni kwa kuja na kuitakia wito wa Ukodak kwa sana bila woga...!
DSC_0013
Divas wa Skylight Band wakiongozwa na Meneja wa bendi Aneth Kushaba AK47 kutoa burudani kwa mashabiki wao. Kulia ni Bela Kombo na kushoto ni Digna Mbepera kwenye show iliyowabamba wakazi wa jiji la Dar Ijumaa iliyopita ndani ya Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0174
Wadada warembo kama hawa wanapatikana Skylight Band pekeee...ni Kila Ijumaa ndani ya Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0017
Digna Mbepera akifanya yake huku akipewa back up na Aneth Kushaba AK47.
DSC_0033
Aneth Kushaba AK47 a.k.a "Komando Kipensi" akifanya yake jukwaani huku akipewa sapoti na Digna Mbepera sambamba na Hashim Donode.
DSC_0060
Hashim Donode akitumbuiza mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0071
Sura mpya ndani ya Skylight Band Bela Kombo akiwapa raha mashabiki wa bendi hiyo Ijumaa iliyopita ndani ya kiunga cha Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0119
Sony Masamba a.k.a Fally Ipupa wa Bongo akiporomosha mavocal ya hatari kwa mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
3
Utaniambia nini zaidi ya Skylight Band, Band ya wajanja na wakali wa town..! tukutane baadae ndio utajua!
7
Jamani Skylight Band kuna raha jamani hebu cheki swahiba hapo pichani alivyoshikwa na hisia mpaka anataka kulia....Skylight Band wamchoma kumoyo jamani...! Dada nae hapo pembeni sasa wewe ni sheeeeeedahhhh!
DSC_0157

8
Watu weeeeeeeeeee!
DSC_0162
DSC_0282
When it comes to Naija Flava with Sam Mapenzi....! Only at Skylight Band.
11
Team #Wanamanyoya wakiongozwa na Rais wao #SultanGijegije (kulia).
DSC_0296
Wadau wa Skylight Band wakishow love na mmoja wa Wanamanyoya.
DSC_0278
Mdau wa Fresh media na Danny Kidjo wakipata Ukodak ndani ya Skylight Band Ijumaa iliyopita.
DSC_0318
Wadau wa ukweli wa Skylight Band wakiendelea kupata Ukodak.
DSC_0294
Yeah that's Whats up....! Wadau wa Skylight Band.
DSC_0184
Bela Kombo wa Skylight Band akishow love na shabiki wake...mtoto mzuriii
DSC_0205
Aneth Kushaba AK47 na shabiki wake wa miaka nenda rudi wakipata Ukodak Back stage.

Thursday, November 6, 2014

MWANZA YADHIBITI KASHFA YA UMRI MAANDALIZI KUELEKEA COPA COCA COLA 2014-2015.

NA ALBERT G. SENGO: MWANZA
Kueleka Michuano ya Copa Coca Cola 2014 Ngazi ya Taifa, Chama cha soka mkoa wa Mwanza (MZFA) licha ya kukumbana na changamoto za udanganyifu kwa baadhi ya washiriki waliojitokeza katika mchakato wa kusaka vipaji vya umri stahiki, hivi ndivyo walivyojipanga katika ushiriki ikiwa ni sanjari na kuwa makini katika uhakiki wa suala la umri kwa wawakilishi wake kwenye michuano hiyo.

Sports Xtra imezungumza na Katibu Mkuu wa MZFA Nasib Mabrouk. BOFYA PLAY KUSIKILIZA

RAIS KIKWETE AWAAPISHA MAKATIBU WAKUU, MABALOZI, WAKUU WA MIKOA NA MAKATIBU TAWALA WAPYA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe Samwel William Shellukindo kuwa Balozi na Msaidi wa Rais Masuala ya Diplomasia leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe John Vianney Mongella kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe Halima Omary Denengo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Dkt Ibrahim Hamisi Msangi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha na kumpa vitendea kazi Dkt Yohana Budeba kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha na kumpa vitendea kazi Injinia Mbogo Futakamba kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha na kumpa vitendea kazi Dkt Donan Mmbando kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha na kumpa vitendea kazi Mhe Jack Mugendi Zoka kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha na kumpa vitendea kazi Mhe Charles Pallangyo kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Geita Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha na kumpa vitendea kazi Bw, Adoh Stephen Mapunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakiwa katika picha ya pamoja na Makatibu wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa wapya baada ya kuwaapisha Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Balozi mpya wa Tanzania Nchini Canada Mhe. Jack Mugendi Zoka (wa pili kushoto), pamoja na mabalozi wengine kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambao ni  kutoka kushoto Balozi Joseph Sokoine (Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika). Balozi Yahaya Simba (Mkurugenzi idara ya Mashariki ya Kati na Balozi Celestine Mushi, Mkurugenzi wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA ISSA MICHUZI.