ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 1, 2014

MWANZA NA HARAKATI ZAKE ZA MABADILIKO KILA KUCHAO

Mwonekano wa engo flani ya jiji la Mwanza, Ziwa Victoria na mwambao wake.
Juu kwa juu na kipande cha barabara ya Rufiji Mwanza.
Uhuru road, Pamba road, Nyerere road, Kaluta road alimuradi ni mchanganyiko.
Kilima cha Bugando na vihusishi vyake.
Uhuru juu kwa juu.
Kwa mbaaaaali vilima vya Mirongo na chini ni majengo ya shule ya msingi Mirongo 
Mirongo juu.
Juu kwa juu shule ya sekondari Thaqafa 2014, mlio soma miaka ya nyuma shuleni hapa mpoo? You C tha changes?
Katikati ya uwanja wa shule ya sekondari Thaqafa kuna kiwanja cha Basketball na Netball, ambavyo vina sapitiwa na maadhari nzuri na mazingira safi shuleni hapo.
Barabara ya Nyerere utulivu na pilika zake.
Ni moja kati ya Hotel mpya zenye hadhi jijini hapa, hoteli zilizonuia kuleta mapinduzi katika utoaji huduma za viwango vya hali ya juu, kuwakarimu wageni waingiao na kutoka.
Chini ardhini hadi ziwa Victoria ndani ya jiji la Mwanza, kutakapo fanyika Serengeti Fiesta ya kwanza kwa mwaka 2014, kutana na Bismark Rock.

EBOLA YASABABISHA MECHI KUTIBUKA.

Mechi kati ya Sierra Leone na Seychelles yatibuka kutokana na hofu ya Ebola.
Mechi kati ya Sierra Leone na Seychelles ya kuwania tikiti ya kushiriki katika kombe la mabingwa barani Afrika mwakani imetibuka.
Hiyo inafuatia hatua ya maafisa wa Ushelisheli kuwanyima Sierra Leone ruhusa ya kuingia nchini humo wakihofia wanaweza kueneza Ebola.
Yamkini timu hiyo ilikuwa ikipania kusafiri lakini maafisa wa usafiri wa ndege katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi wakawaarifu kuwa Ushelisheli haijaidhinisha safari yao kuingia nchini humo.
Timu hiyo ililazimika kurejea hotelini mjini Nairobi Kenya ambako wamekuwa wakipiga kambi tangu Jumatano.
Rais wa shirikisho la soka la Sierra Leone Elvis Chetty ameiambia BBC kuwa amepokea habari kutoka kwa Wizara ya afya ya Ushelisheli kuwa angependa waiahirishe mechi hiyo kutokana na hofu ya kuenea kwa Ebola.
Barua hiyo ya Wizara ya Afya inaelezea hofu ya kisiwa hicho ya kutokea mlipuko wa homa ya Ebola.
Chetty aliendelea kusema kuwa kufuatia tahadhari iliyotangazwa leo na rais wa Sierra Leone kuwa huenda ugonjwa huo ukadhibitiwa katika kipindi cha miezi minne ijayo basi huenda mechi hiyo haitachezwa kamwe.
Hatua hiyo huenda ikasababisha Ushelisheli ikapigwa marufuku ya kushiriki mashindano hayo.
Sierra Leone, ilishinda mkondo wa kwanza mabao mawili kwa nunge .
Ebola ilivyoenea Afrika Magharibi.
Mechi hiyo ilichezwa juma lililopita.
Chetty alisema kuwa kuambatana na sheria za shirikisho la soka barani Afrika CAF, mechi hiyo inasiku 3 tu za kuchezwa vinginevyo wapinzani walistahili kupewa ilani siku 10 kabla ya tarehe iliyopangiwa mechi yenyewe.
''Ninaamini kuwa tayari Mshelisheli ameamua liwe liwalo hatocheza mechi hiyo na hilo huenda likaisababishia taifa hilo marufuku ya kipindi kirefu.

''Kimsingi taifa lote lilikuwa limechangamkia mechi hii na ni jambo la kusikitisha sana''.
CHANZO:BBC SWAHILI.

Thursday, July 31, 2014

WAREMBO REDS MISS MWANZA 2014 WAANZA KAMBI RASMI.

Doris Robert.
Aisha Ally.
Lisa Abdalah.
Zaki Lema.
Christina Jilulu.
Tekla Samuel.
Amina Bega.
Doris Robert.
Mmoja kati ya waandaaji  maarufu Kanda ya Ziwa Mr. John Dotto (wa pili kulia walioketi mbele) akizungumza na baadhi ya washiriki wa kinyag'anyiro cha Redds Miss Mwanza 2014 katika ukumbi wa VIP Villa Park Mwanza, ambapo kambi imeanza rasmi jana. Mchakato wa kumpata mrembo kwa shindano hilo utafanyika usiku wa sikukuu ya Nanenane tarehe 8/08/2014 katika ukumbi wa Jb Belmont Hotel Mwanza.
Sehemu ya warembo hao.
Kutoka kulia hadi kushoto.
Ni warembo nane kati ya kumi na mbili watakaoshiriki kinyang'anyiro cha Redds Miss Mwanza 2014 shindano hilo utafanyika usiku wa sikukuu ya Nanenane tarehe 8/08/2014 katika ukumbi wa Jb Belmont Hotel Mwanza.

MECHI ILIYOCHEZWA JANA:- MANCHESTER CITY v/s LIVERPOOL 2-2 SECOND HALF TIME FULL MATCH RECORD HD 2014 NA PENATI 1-3

Manchester City vs Liverpool match report: Simon Mignolet the penalty hero as Reds win on spot-kicks.

Shuhudia video kipindi kizima cha pili cha mchezo huo wa kirafiki kugombea ngao maalum kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya Uingereza 2014-2015. 

Hapa chini ni video ya magoli ndani ya dakika 90 Manchester City 2 v/s Liverpoool 2 pamoja na mikwaju ya penati iliyoamua ushindi kwa Liverpool kwa mikwaju 1-3.

PICHA ZA EXTRA BONGO WALIVYO PAGAWISHA EID MOSI NDANI YA JEMBE BEACH MWANZA

Kiongozi wa Xtra Bongo Ally Chocky Mzee wa Farasi akiinadi album mpya ya Xtra Bongo ndani ya usiku wa burudani ya kusherehekea sikukuu ya Eid El Fitri uliofanyika Jembe Beach aka Skylight Beach Resort Malimbe Mwanza.
Xtra Bongo wakilishambulia jukwaa ndani ya Jembe Beach Mwanza katika kusherehekea sikukuu ya Eid El - Fitri ambapo kundi hilo lilisisimua mashabiki vya kutosha.
Dancer mahiri nchini Super Nyamwela (kulia) akiwaongoza wenzake kutoa burudani jukwaani.
Kona ya Mashabiki wakiserebuka.
Umesomeka.....
Bass guitar lilishikiliwa na jamaa huyu...
Kiongozi wa Xtra Bongo Ally Chocky Mzee wa Farasi (kushoto) akimtambulisha jukwaani Banza Stone (wa pili toka kushoto) wakati bendi hiyo ilipotoa burudani kwa wakazi wa jiji la Mwanza katika kusherehekea sikukuu ya Eid El Fitri uliofanyika Jembe Beach aka Skylight Beach Resort.
Sasa ni  wakati wa kuonyesha mautundu....
Hatariiii!!!
The Style....
Team Jembe.
Mbona kazi....
Hapo Jeh!!
Uwiiiiiiiii....uwaaaaaa!!!
Live.
Upande wa pili disco kama kawa, hivyo ulikuwa na uchaguzi wa kuchagua aina ya burudani unayoitaka, muziki wa Band au ngoma za hatari na disco la ufukweni toka Jembe Djz. Pichani ni DVJ K-flip.
Wadau wa Skylight beach resort wakiduarika...
Chungulia imo.

Tuesday, July 29, 2014

LIGI YA EPL VERY SOON KUANZA KUTIMUA VUMBI, USAJILI NAO UMECHACHAMAA.

Cedrick A. G. Sengo (L) na Cuthbert A. G. Sengo (R)
Divorc Origi katika mojawapo ya mechi za Ubelgiji
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ubelgiji Divorc Origi hatimaye amejiunga na timu ya Liverpool.

Baba yake Origi, Mike Okoth, ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu taifa ya Kenya Harambee Stars amethibitsha mwanawe Divorc amesaini mkataba na Liverpool ambao walifurahishwa na mchezo wake mzuri alipoiwakilisha Ubelgiji kwenye kombe la dunia.
Arsenal yamsajili Chambers
Kilabu ya Uingereza ya Arsenal imemsajili mlinzi wa kilabu ya Southampton Calum Chambers kwa takriban paundi millioni 16.
Mchezaji huyo wa timu ya Uingereza isiozidi umri wa miaka 19 alifanyiwa ukaguzi wa kimatibabu siku ya ijumaa.
Chambers mwenye umri wa miaka 19 ameshiriki mara 25 katika timu ya soka ya taifa la Uingereza na kwamba Arsenal inamuona kama suluhu wa safu ya ulinzi wa kulia na katikati .
Arsenal pia inamsaka mchezaji wa kiungo cha kati wa Southampton Morgan Schneiderlin mwenye umri wa miaka 24 ambaye aliichezea timu ya Ufaransa katika kombe la dunia.