ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 17, 2014

JIJI LA MWANZA LAPEWA HESHIMA KUWA WENYEJI KILELE CHA TUZO ZA USAFI WA MAZINGIRA MAJIJI NCHINI.

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Halfa Hida, amewaeleza Madiwani wa jiji hilo kuteuliwa kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya kilele cha kutoa Tuzo kwa washindi wa usafi na mazingira nchini.

Maadhimisho hayo yanataraji kufanyika Juni 5 mwaka huu,  chini ya uratibu wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) iliyo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu kabla ya zawadi na Tuzo hizo kutolewa na ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira.
Hida aliwataka wataalamu na watendaji wa Jiji hilo kujiandaa na maadhimisho hayo, ambapo tayari ofisi ya Waziri Mkuu imeisha toa vigezo vya kushindaniwa na Majiji, Manispaa na Halmashauri za wilaya nchini kote.
“ Watendaji wa Kata na Mitaa tuendelee na mkakati wetu wa usafi kwenye Kata na Mitaa ikiwa ni pamoja na kuendelea kuweka mazingira yetu katika hali ya usafi ili jiji hilo liibuke tena na tuzo ya ushindi kwa mara ya tisa mfululizo,” alisisitiza

Mkurugenzi Hida alisema juzi kwamba, “Tutumie sheria ndogo ndogo za Hamashauri yetu na kuhamasisha wananchi na vikundi vya usafi kuweka mazingira katika hali ya usafi kabla ya wakaguzi kupita kwenye Mitaa na Kata kutoa maksi.” Alieleza.
Aidha alifafanua kwamba, pia katika maadhimisho hayo jiji linategemewa kupata wageni kutoka Majiji, Miji, Manispaa na Halmashauri za Wilaya za ndani na  nje ya nchi, ambao wamekaribishwa kushiriki katika maadhimisho hayo.

Huku akitamba kunyakua ushindi kwa mara ya tisa, Hida aliwaagiza maafisa afya wa jiji hilo kuweka mikakati ya kuendeleza usafi katika jiji hilo aliloliita Smart City ili kuwa kivutio kwa wawekaezaji na wageni watakaokuja.
Kwa upande wake, Meya wa Jiji hilo Stanslaus Mabula amemtaka Mbunge wa jimbo la Nyamagana Ezekia Wenje aache kuwachochea wafanyabiashara ndogondogo (machinga) na kuwachonganisha na viongozi wa serikali na Jiji ili wavunje taratibu, kanuni na sheria za Mipango miji.

Meya, Mabula akihutubia Baraza la Madiwani wa jiji hilo, alisema kwamba licha ya Wenje kutoshiriki mara kwa mara vikao vya baraza hilo, lakini amekuwa akiwahamasisha wamachinga  na wafanyabiashara wengine kufanya biashara katika maeneo wasiyo ruhusiwa jambo ambalo linaweza kusabaisha jiji hilo lipoteze ushindi.

“Kwa hili niwaombe wafanyabishara wanaofanya biashara katika maeneo yasiyo ruhusiwa ikiwa pamoja na wanaopanga bidhaa nje ya maduka na sehemu za wapiti kwa miguu, waache mara moja kwani wanavunja sheria ya mazingira ya mwaka 2004 kifungu namba 187 (1) na 191 Act Cap 20/2004.” Alisema.

Alitowa wito kwa Madiwani na wataalamu wa afya waendelee kusimamia mpango kabambe wa usafi na Mazingira wa jiji hilo uliozinduliwa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo ambao hutekelezwa kila mwanzoni mwa wiki ya kwanza ya kila mwezi.

MWONGOZAJI, MWIGIZAJI MAHIRI BONGO MOVIE ADAM KUAMBIANA AFARIKI DUNIA.

Enzi za uhai wake mwigizaji Adam Kuambiana.
INAKUWA  vigumu kuamini kutoa taarifa kuwa yule muongozaji filamu maarufu ambaye vilevile ni mwigizaji wa filamu katika soko la Bongo Movie, Adam Kuambiana kuwa amefariki dunia.

Adam Kuambiana amefariki dunia wakati akipelekwa katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam kwa matibabu alfajiri ya kuamkia leo.

Inatajwa kuwa kabla ya kuzidiwa marehemu alianguka chooni akiwa location katika hoteli ya Silver Rado iliyopo Sinza kwa Remy jijini humo ambapo kabla ya mauti kumfika, Adam alikuwa akilalamika kuwa anasumbuliwa na tumbo.

Kwa hivi sasa mwili wa marehemu uko katika mochwari za hospitali hiyo, ukisubiri taratibu nyingine za mipango ya kifamilia hatimaye kupumzishwa katika nyumba yake ya milele.

Taarifa zaidi tutaendelea kukufikishia kadri zitakavyokuwa zikitufikia.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!

PUMA ENERGY TANZANIA YAZINDUA VILAINISHI VYA CASTROL NA KITUO CHA MAFUTA CHA OSTERBAY DAR.

  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUMA Energy Tanzania, Bw. Phillipe Corsaletti akiongea katika uzinduzi wa Vilainishi vya Castrol vilivyoendana na uzinduzi wa kituo kipya cha Mafuta kilichopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Wageni na wafanyakazi wa kampuni ya PUMA Energy Tanzania wakifuatilia uzinduzi wa Vilainishi vya Castrol vilivyoendana na uzinduzi wa kituo kipya cha Mafuta kilichopo Masaki jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa Kituo Kipya cha Mafuta kilichopo Masaki jijini Dar es Salaam.
Gari litakalotumiwa katika mashindano ya Magari yanayotarajia kufanyika Mwishoni mwa wiki.
Wateja wakipatiwa huduma na wafanyakazi wa kampuni ya PUMA Energy Tanzania.
Meneja Mauzo wa Vilainishi vya Castrol, Gilbert Chacha akizungumza wakati wa uzinduzi ambapo alisema kuwa Vilaainishi vya Castrol vina ubora wa kimataifa na hutumika katika magari, viwanda, meli, ndege. Kwa sasa wana aina mbili za Vilainishi hivyo Castrol GTX 20W50 na GTX Diesel 15W40. Pembeni yake niMshereheshaji Shebe Machumani na dereva wa gari la Mashindano.
Meneja wa Usalama wakati wa Kazi wa Kampuni ya PUMA Energy Tanzania, Jonathan Mmari akizungumza machache.
Walioko mbele kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya PUMA Energy Tanzania, Dkt. Ben Moshi na  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUMA Energy Tanzania, Bw. Phillipe Corsaletti wakiwa na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa Vilainishi vya Castrol vilivyoendana na uzinduzi wa kituo kipya cha Mafuta kilichopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUMA Energy Tanzania, Bw. Phillipe Corsaletti akionyesha picha ya sanamu itakayotumika kutambulisha vilainishi vya Castrol wakati wa uzinduzi wa Vilainishi vya Castrol vilivyoendana na uzinduzi wa kituo kipya cha Mafuta kilichopo Oysterbay jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Mshereheshaji Shebe Machumani.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUMA Energy Tanzania, Bw. Phillipe Corsaletti na Mshereheshaji Shebe Machumani wakionyesha vilainishi vya Castrol.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUMA Energy Tanzania, Bw. Phillipe Corsaletti akitoa zawadi ya pesa taslimu shilingi laki mbili kwa mfanyakazi bora namba tatu wa Mwezi wa Aprili, Andrew Jagy wakati wa uzinduzi wa Vilainishi vya Castrol vilivyoendana na uzinduzi wa kituo kipya cha Mafuta kilichopo Oysterbay jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Mshereheshaji Shebe Machumani.
Mfanyakazi bora namba mbili wa Mwezi wa Aprili, Samwel Joseph akionyesha pesa taslimu shilingi laki na nusu alizozawadiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUMA Energy Tanzania, Bw. Phillipe Corsaletti wakati wa uzinduzi wa Vilainishi vya Castrol vilivyoendana na uzinduzi wa kituo kipya cha Mafuta kilichopo Oysterbay jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Mshereheshaji Shebe Machumani.
 Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya PUMA Energy Tanzania, Dkt. Ben Moshi akimkabidhi Mfanyakazi bora namba moja wa Mwezi wa Aprili, Janeth Martine pesa taslimu shilingi laki mbili na nusu wakati wa uzinduzi wa Vilainishi vya Castrol vilivyoendana na uzinduzi wa kituo kipya cha Mafuta kilichopo Oysterbay jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUMA Energy Tanzania, Bw. Phillipe Corsaletti.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUMA Energy Tanzania, Bw. Phillipe Corsaletti akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi bora wa mwezi Aprili. Kampuni hiyo hutoa zawadi kila mwezi kwa wafanyakazi wanaofanyakazi vizuri. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

Friday, May 16, 2014

PENGO JINGINE MUZIKI WA DANSI NCHINI


TASNIA ya muziki wa dansi nchini Tnzania imepata pigo mara baada ya mmoja kati ya mwimbaji nyota wake aliyewahi kufanya vyema Amina Ngaluma 'Japanese' kufariki dunia.

Muimbaji huyo aliyetamba na bendi za Tam Tam na Double M Sound, amefariki dunia jana akiwa nchini Thailand alipokuwa akiishi kikazi.

Kwa mujibu wa mume wa marehemu  ambaye pia ni mwanamuziki Rashid Sumuni, amethibitisha kifo cha mkewe na kuongeza kuwa mkewe alikuwa nchini humo akiwa na mkataba wa moja ya bendi nchini Thailand inayojulikana kwa jina la Jambo Survival aliyokuwa akiimba.

Siku nne zilizopita alipata taarifa kutoka kwa kiongozi wa bendi hiyo Hassan Shuu kuwa marehemu mkewe amekimbizwa hospitali mara baada ya kupata maumivu makali ya kichwa.

Mpaka anakimbizwa kupatiwa matibabu kwenye moja ya hospitali kubwa nchini Thailand inatajwa kuwa alikuwa katika hali mbaya kiasi kwamba ilifika kipindi marehemu 'Japanese' alizidiwa hata akawa hajitambui.

"Toka jumamosi alikuwa hajitambui na jana majira ya saa 6 nilipata simu kuwa mke wangu kaaga dunia" Alisema Rashid Sumuni wakati akihojiwa na Amplifaya ya Clouds fm.

Moja ya nyimbo zilizompa umaarufu ni Mgumba No.1 aliouimba na bendi ya African Revolution 'Tam Tam' chini ya Mwinjuma Muumini.

 G. Sengo blog inapenda kuwapa pole ndugu,  jamaa na marafiki wa karibu wa familia, mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amen.

REDS MISS SIMIYU YAPANIA KUTETEMESHA MISS TANZANIA.

Catherine Palmer (20)
Patricia Phinias (22).
Connie Frederick (21)
Asia Mohamed (20)
Coletha Jastine (21)
Esthar Martin (22)
Caroline Akut (21)
Mariam Yusuph (19)
Reira Abeid (21)
Elizabeth Gordian (21)
Huyu ndiye Matron wa washiriki wa Redds Miss Simiyu 2014 Bi. Clara Ayoub.
Washiriki katika picha ya pamoja.
Sehemu ya waalikwa na waandishi wa habari walio hudhuria tukio la utambulisho wa wanyange hao ambao watakwenda kushindanishwa katika kinyang'anyiro hicho kitakachofanyika mnamo tarehe 7/06/2014 mkoani Simiyu.
Mratibu wa Redds Miss Simiyu 2014 omary Bakari (katikati) akiwa na wanyange wa kinyanganyiro kitakacho fanyika tarehe 7/06/2014 mkoa mpya wa Simiyu.
WAREMBO 16 kutoka Wilaya tano za Mkoa wa Simiyu wameingia kambini kujiandaa na kinyang’anyiro cha kuwania taji la REDD'S Miss Simiyu lililopanwa kufanyika Juni 7 mwaka huu mkoani hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Muandaaji wa shindano hilo Mkoa wa Simiyu kwa mwaka 2014/2015, Omary Bakari, alisema kwamba tayari warembo 16 wako kambini kuanzia juzi watakaoshiriki shindano la REDD'S Miss Simiyu kutoka Wilaya za Bariadi, Busega, Itilima, Maswa na Meatu.

Bakari alisema kwamba shindano hii ni mara ya kwanza kwa Mkoa wa Simiyu kuaandaa na kushiriki mashindano ya kumsaka warimbwende watakao uwakilisha Mkoa huo katika shindano la Kitaifa la REDD'S Miss Tanzania mwaka 2014/2015 baada ya Wilaya zake kugawanywa na kuundwa Mkoa mpya wa Simiyu.

“Tayari wadhamini wa shindano hili wameisha kamilisha taratibu za udhamini wao kwa kufunga mkataba ambao umewezesha warembo hawa 16 kuingia kambini kujifua kwa kuanza mazoezi, kufundwa kimaadili na kuonyesha vipaji vyao na matarajio yao katika kuisaidia jamii endapo watafanikiwa kuwa washindi chini ya mkufunzi wao Clara Ayoub ” alisema.

Mratibu wa shindano hilo, alisema kwamba katika kunogesha shindano hilo siku hiyo kwa mara ya kwanza wananchi wa Mkoa huo watashuhudia burudani kali kutoka kwa mwanzamuziki mashuhuri wa Muziki wa Taarabu nchini Mzee Yusufu na kundi zima la Jahazi Modern Taarab, Msanii wa Bongo Fleva H Baba na wasanii wengi kutoka Kanda ya Ziwa wakiwemo wachekeshaji.

“Wito wangu kwa wananchi wa Mkoa wetu wa Simiyu wajitokeze kwa wingi kujionea vipaji vya warembo ambao wana sifa zote zinazokidhi vigezo vyakuwa washindi na kutoa Baraka zao kwa warembo wawili watakaouwakirisha mkoa huu katika shindano la kitaifa mwaka huu” alisema.

Bakari aliwataja wadhamini wa REDD'S Miss Simiyu mwaka huu kuwa ni  Kampuni ya Airtel, TBL kupitia kinywaji chake cha REDDs, Chuo cha Musoma Utalii Mkoa wa Shinyanga, Bhatt Electronic, Serengeti Stop Over, Benki ya CRDB, SBC kupitia kinywaji cha Peps, G&K Smart Hotel, Victoria Insitute, Matvila Beach na LP Gass Point.

HAPPY BIRTHDAY ADAM MCHOMVU.

Leo ni birthday ya mwanangu mwenyewe .... just maneno machache yanatosha = Happy Birthday Baba Jonii aka AD Plus, aka Baba la baba.

AIRTEL YADHAMINI MAFUNZO YA WAANDISHI.

Mwenzeshaji wa Mafunzo ya waandishi wa habari bwana Ndimata Tegambwage akiongea wakati wa uzinduzi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imedhamini mafunzo ya wapigapicha yatakayofanyika kuanzia kesho katika kituo cha Msimbazi  jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na MP5 2011 Entertainment.  Pichani katikati ni  Afisa mawasiliano na Matukio bi Dangio Kaniki akifatiwa na mratibu wa semina Mpochi
Selemani.
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imesema itaendelea kuwajengea uwezo wapiga picha za habari kwa kuendela kuwapatia mafunzo ili wapate ujuzi zaidi kwa kuwa wao ni balozi katika kuipasha jamii habari.

Hayo yalisemwa Jijini Dar es Salaam jana na Afisa Uhusiano na Matukio wa Kampuni ya Airtel  Dangio Kaniki alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya siku nne kwa wapiga picha wa habari kuwajengea
uwezo kufanya kazi katika mazingira hatarishi.

"Tutaendela kuwapatia mafunzo wapiga picha ili wapate ujuzi zaidi katika utendaji wao wa kazi kwa kuwa mabalozi wetu,na tutawatafutia vifaa vya kisasa kwa ajili ya kufanyia kazi katika mazingira hatarishi"alisema Dangio

Mafunzo hayo yanaendeshwa na Baraza la Habari (MCT),na kudhaminiwa na kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na kampuni ya MP5 2011 yanashirikisha wapiga picha kutoka magazeti na TV.

Akizungumza katika mafunzo hayo mshiriki Suleiman Mpochi ambae pia ni mratibu wa mafunzo hayo alisema watanufaika nayo kwa kuwa watajifunza mbinu mpya za kufanya kazi katika mazingira hatarishi pamoja na
kufuata maadili ya taaluma ya waandishi wa habari.

Kampuni hiyo ni mara ya tatu inadhamini mafunzo hayo kwa wapiga picha za habari ambamo Mwezeshaji katika mafunzo hayo Mkongwe wa Habari katika fani ya habari Ndimara Tegambwage aliiomba kampuni kuendela
kudhamini mafunzo hayo na kuwapatia zana za kisasa za kazi wapiga picha.

FILAMU YA JOTI SANDUKU LA BABU KUINGIA SOKONI HIVI KARIBUNI


MSANII  Lucas Mhavile ‘Joti’baada ya kukaa kimya kwa mda sasa ameibuka na filamu yake ya Joti Sanduku la Babu ambayo amecheza katika husika tofauti tofauti filamu hiyo itakuwa ikisambazwa na   Kampuni yaproin promotions ya jinini Dar es salaam.

Akizungumzia filamu hiyo Joti alisema kuwa amekuja kivingini kwani kitu alichofanya katika filamu hiyo aijawai kutokea wala kufanywa na mtu yoyote yule katika tasinia hii ya filamu nchini.

 Hivyo wapenzi wangu wakae mkao wa kula tu kwani wakati wowote kuanzia sasa itakuwa inaingia sokoni kwani filamu hii si yakukosa mana unambiwa uzee mwisho chalinze mjini kila mtu honey.

Hivyo wapenzi wa filamu nawaomba wanunue nakala alisi ya filamu hiyo pindi itakapotoka ambapo nimelezea mambo mbalimbali ya ujana usichana pamoja na uzee.

 Mbali na hivyo filamu hiyo imebeba mambo matatu muhimu kwanza ina burudisha pia ina elimisha na kupata ujumbe muhimu kabisa katika jamii inayotuzunguka.'

Filamu hiyo ya kwanza tangu joti aweke kando mambo ya filamu na kujingiza katika mambo ya uchekeshaji kupitia luninga sasa ameludi tena katika filamu.

yake mwenyewe inayokwenda kwa jina la joti sanduku la babu.

Thursday, May 15, 2014

SULEIMAN TALL, DULA MBABE ULINGONI MAY 24

Bondia mzoefu wa ngumi za kulipwa nchini Suleiman said Galile ”tall” anategemea kupanda tena ulingoni may 24 katika ukumbi wa friends corner manzese kuzipiga na Abdalah Pazi “dula mbabe/kiroba” katika pambano lisilo la ubingwa. 


Akithibitisha kuwepo kwa pambano hilo katibu wa ngumi za kulipwa nchini na ndie anayesimamia mapambano yote ya utangulizi bw Ibrahim  Abbas kamwe amesema, “galile na dula wamekubaliana kusheza siku hiyo ya jumamosi ya terehe 24 na watazipiga katika uzito wa kg76 wakiwasindikiza Karama Nyilawila na Said Mbelwa watakao gombania ubingwa wa UBO, hapo awali ilipangwa Karama kuzipiga na Thomas Mashali ambae amepatwa na majeraha kutokana na ajali ya gari.
Pia siku hiyo kutakuwa na  mapambano mengine ya utangulizi yenye ushindani , wakati  Adam Ngange akimkabili Alan Kamote wa Tanga, Zumba Kukwe atazipiga na Kamanda wa makamanda, Ramadhan Kumbele ataoneshana umwamba na Hasan Kiwale “Moro best”, Bakari Dunda na Mbena Rajabu, huku madogo wanaokuja juu kwa kasi katika ngumi Idd Athuman atacheza na  Julias Thomas Kisarawe, Mwaite Juma na Daud Giligili.
Kamwe alimaliza kwa kusema mpaka sasa hakuna bondia mwenye matatizo wote wapo katika hali ya ushindani wanaisubiria kwa hamu hiyo siku ifikie wabanjuane kiukweliukweli na watu wategemee mashindano mazuri yenye uwezo mkubwa wa kusukuma masumbwi.

MKUU WA MKOA WA MWANZA INJINIA NDIKILO AFUNGUAA MKUTANO WA 16 WA WAKANDARASI NA WADAU WA UJENZI

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano wa Bodi ya Usajiri wa Makandarasi kwa mwaka 2014 kwa Kanda ya ziwa uliofanyika katika kituo cha mafunzo Benki Kuu Capri Point Mwanza.
Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi Eng. Boniface Muhegi amesemakuwa idadi ya makandarasi daraja la Kwanza imeongezeka toka 15 kwawalioomba kupandishwa daraja hadi kufikia 40.
Unapozungumzia ujenzi wa miundombinu kama barabara, reli, bandari, viwanja vya ndege, viwanda, mabwawa na malambo ya maji, migodi ya madini, makazi ya watu, majumba ya starehe, hospitali, shule na minara ya mawasiliano, moja kwa moja unawagusa makandarasi. Sasa wamekusanyika hapa kuhudhuria Mkutano wa 16 wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa makandarasi kwa mwaka 2014 kwa Kanda ya Ziwa uliofanyika katika kituo cha mafunzo Benki kuu Capri Point Mwanza.
Bodi ya Makandarasi imekuwa ikitumia mikutano hii kupata mrejesho kutoka kwa wadau pamoja na kutathimini maeneleo ya sekta ikiwani pamoja na kuibua mikakati mbalimbali ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili na hivyo kuleta maendeleo kwa Makandarasi, husussani Makandarasi wazalendo.
Ili kuinua uwezo wa Makandarasi Bodi ya makandarasi imekuwa ikiendesha mafunzo mbalimbali chini ya Mpango Endelevu wa Makandarasi unaopewa sapoti na Mfuko wa kusaidia Makandarasi (Contractors Assistance Fund), pamoja na Mkakati Maalum chini ya Mpango Maalum wa Kuendeleza Makandarasi wa Kizalendo. 
Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi Eng. Boniface Muhegi " Sheria ya kulipa kodi ya mwaka ilibadilika miaka mitatu iliyopita Makandarasi waliosajiliwa miaka mingi iliyopita walikuwa wamekariri kuwa zamani ulikuwa unaweza kulaza miaka miwili bila kulipa na usifutwe, lakini kwa sasa sheria hairuhusu kulaza mwaka wowote, na usipolipa sheria mama inakutaka usiendelee kuwa Mkandarasi. Sasa hii imekumba makandarasi wengi sana.. CRB imefuta Makandarasi 752 tulisikitika sana, lakini kwasababu ilikuwa ni kwa mujibu wa sherika hatukuwa na lakufanya"
Wakandarasi wameombwa kuweka wataalamu katika kusimamia shughuli zao za utendaji na kufanya kazi kwa viwango bora ili kupata thamani halisi ya fedha na kuendelea kuwa na sifa.
Kusanyiko la Makandarasi ndani ya ukumbi wa BOT Capri point Mwanza.
Makandarasi kutoka mikoa ya Mwanza, Simiyu, Kagera, Mara, Geita, Shinyanga na Tabora wakifuatilia ufunguzi wa  Mkutano huo kwa umakini.