ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 5, 2014

VIKOBA VYAZINDULIWA MWANZA NA MSTAHIKI MEYA MABULA.

Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akizindua mfuko wa kuweka na kukopeshana ujulikanao kama Vikoba, kushoto anaonekana Rais wa Vikoba Tanzania Bi. Devota Likokola akihamasisha kuwa mfuko huosi kwa wananchi wa mijini tu bali hata vijijini. 

Mstahiki Meya Mhe. Mabula ameahidi kuwapatia wadau hao wa Vikoba kuwapatia kiwanja kwa ajili ya kujenga ofisiPICHA NA ZEPHANIA MANDIA.

MC PILIPILI, JOTI, LULU NA RICHIE RICHIE WASAKA VIPAJI MWANZA.

Picha ya pamoja ya Convoy nzima la kusakavipaji likiwa ndani ya studio za Passion Fm Mwanza mara baada ya kumaliza mahojiano na mtangazaji wa radio hiyo Philbert Kabago (mwenye head phones katikati). 
Wadau wa MTM kutoka kushoto ni Mc Pilipili, mchekeshaji wa ORIJINO KOMEDI Joti, Mtangazaji wa Passion Fm Philbert Kabago, waigizaji wa luninga Lulu pamoja na Richie Richie.

SHULE YA MOTAMBULU MOSHI YAPATA MSAADA WA VITABU TOKA AIRTEL.

Mkuu wa wilaya ya Rombo kulia akimkabidhi mwanafunzi Happnes John wa shule ya sekondari motamburu moja ya vitabu vya sayansi vilivyo tolewa na Airtell katika mpango wa shule yetu kwa shule ya sekondari Motamburu iliyopo Rombo mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa wilaya ya Rombo kulia akimkabidhi mwalimu mkuu(Abel Masuki kushoto) wa shule ya sekondari motamburu baadhi ya vitabu vya sayansi vilivyo tolewa na Airtell katika mpango wa shule yetu shuleni hapo.

Shule ya Motamburu Moshi yapata msaada wa vitabu toka Airtel
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia Program yake ya  shule yetu  imeendelea na zoezi lake la kuinua kiwango cha ufaulu katika masomo  ya sayansi ambapo imekabidhi vitabu vya ziada na kiada katika masomo ya sayansi  kwa shule ya  sekondari ya MOTAMBURU   iliyopo  Kata ya tarakea  wilaya ya  Rombo mkoani Kilimanjaro.
Akizungumzia msaada huo  Meneja biashara wa Airtel kanda ya kaskazini Brightone Majwala   alisema" program ya shule yetu inayolenga kutoa vifaa vya kufundishia mashuleni  ikiwemo  vitabu vya kiada na ziada   kwa upande wa masomo ya sayansi  ambapo mpaka sasa wameweza kufikia shule 900 katika baadhi ya mikoa ya Tanzania bara na visiwani ".

"Tutaendelea kushirikiana na serikali chini ya wizara ya elimu katika kuhakikisha tunaboresha elimu mashuleni na kupunguza changamoto za upatikanaji wa vitabu katika shule nyingi nchini. sliongeza Majwala

Mkuu wa wilaya ya Rombo Elinasi Pallangyo  ambaye ndio  alikuwa mgeni rasmi katika hafla fupi za makabidhiano hayo ,alipokea msaada wa vitabu  na kuukabidhi  kwa uongozi wa shule baada ya kukabidhiwa na meneja biashara wa Airtel kanda ya kaskazini ambapo amewashukuru airtel kwa msaada huo ambao amesema  umekuja wakati muafaka  huku akiwakumbusha wadau wengine kuiga mfano wa Airtell Katika kuchangia maswala muhimu ndani ya sekta ya elimu hususani katika maeneo ya vijijini.

Akitoa taarifa fupi ya maendeleo ya shule kwa mkuu wa wilaya  mkuu wa shule ya  sekondari MOTAMBURU Abel Masuki  ameishukuru airtel Tanzania kwa msaada huo ambao wamesema Airtel imeonyesha kuwa mfano mkubwa kwa makampuni mengi kwa kuungana na serikali kutekeleza sera  ya  elimu ya kuwaelimisha watanzania wengi  hasa walio  maskini kuwaondolea ujinga lakini pia akatoa changamoto ya vifaa vya maabara.

TSN BOYS KUKABILI MWANANCHI MEDIA KOMBE LA NSSF KESHO: MROKI AIAHIDI DAU NONO.


Kikosi cha TSN Boys

TIMU ya soka ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) inashuka dimba la Sigara, Chang’ombe, Dar es Salaam kuikabili Mwananchi katika Kombe la NSSF kwa Vyombo vya Habari 2014.

Mechi hiyo itakayochezwa LEO (jumamosi) saa 2 asubuhi, itakuwa muhimu kwa timu zote mbili kwani mshindi atasonga mbele katika hatua ya robo fainali zitakazoanza Jumatatu ijayo.

TSN imetinga hatua hiyo baada ya kupewa ushindi kutokana na wapinzani wao, Mlimani Media kuwatumia wachezaji ambao hawakuwa halali. Mlimani Media ilikuwa imeshinda kwa mabao 9-0.

Mwananchi ni mechi yake ya kwanza. Mbali ya mechi hiyo, mechi nyingine kesho ni kati ya Tumaini dhidi ya Sahara Media, wakati upande wa netiboli, itakuwa ni mechi za robo fainali kati ya Business Times dhidi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), wenyeji NSSF dhidi ya Tumaini Media.

TSN Boys wapo katika hamasa na ari kubwa ya mchezo huo wa kesho ambapo Meneja wa Timu hiyo, Mroki Mroki "Father Kidevu"  ameahidi kuzawadia mfungaji wa kila goli kitita cha shilingi 5,000. 

"Niliahidi katika mchezo wa awali na hata sasa bado ahadi yangu ipo pale pale kwa kila goli nitalilipia shilingi 5,000 nahiyo haina longolongo lengo ni kuhamasisha ushindi kwa timu yetu," alisema Mroki.

Aidha Mroki amesema atakuwepo uwanjani kuhakikisha ushindi unapatikana kwa vijana wa TSN Boys na kusonga mbele katika mashindano hayo. 

Katika mechi za jana, mabingwa watetezi wa soka, Jambo JANA walitolewa baada ya kufungwa mabao 2-1 na Free Media kwa mabao ya Saleh Mohammed.

Bao la Jambo JANA lilifungwa na Zahoro Mlanzi. Aidha, Changomoto ilisonga mbele baada ya kuilaza New Habari kwa penalti 7-6, baada ya sare ya bao 1-1. Free Media na New Habari zilisonga mbele kama timu bora mbili zilizoshindwa, lakini zikiwa na matokeo mazuri (best looser).

Katika netiboli, Mlimani Media ilishindwa kutamba kwa Habari Zanzibar kwa kufungwa mabao 19-15, wakati IPP iliizamisha Global Publishers kwa
mabao 27-8.

JAJI AUGUSTINEO RAMADHANI AWATAKA WAJUMBE KUJADILI RASIMU KWA MAKINI.

Makamu mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Augustino Ramadhani akiongea jijini Dar es Salaam jana Aprili 3, 2014 katika wa mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The  Open Society Initiative  For  Eastern African Tanzania  (OSIEA). Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Mjadala huo, Profesa Chris Maina, pamoja na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Ayoub Rioba.
Kamishana wa zamani wa Tume ya Uchaguzi  ya Zanzibar - ZEC, Dkt. Nassor Seif Amour akitoa ufafanuzi  jijini Dar es Salaam jana Aprili 3, 2014 katika wa mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The  Open Society Initiative  For  Eastern African Tanzania  (OSIEA).  Pembeni ni Makamu mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Augustino Ramadhani na Mwenyekiti wa Mjadala huo, Profesa Chris Maina.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Ayoub Rioba akitoa maelezo jinsi vyombo vya habari vinavyoshiriki katika mchakato wa kupata katiba mpya, wakati wa mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The  Open Society Initiative  For  Eastern African Tanzania  (OSIEA).
Washiriki walioshiriki katika mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The  Open Society Initiative  For  Eastern African Tanzania  (OSIEA).
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Ayoub Rioba akitoa maelezo jinsi vyombo vya habari vinavyoshiriki katika mchakato wa kupata katiba mpya, wakati wa mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The  Open Society Initiative  For  Eastern African Tanzania  (OSIEA).
Washiriki walioshiriki katika mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The  Open Society Initiative  For  Eastern African Tanzania  (OSIEA).
Washiriki walioshiriki katika mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The  Open Society Initiative  For  Eastern African Tanzania  (OSIEA).
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHWashiriki walioshiriki katika mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The  Open Society Initiative  For  Eastern African Tanzania  (OSIEA).
Wadau wakitoa michango yao katika mjadala huo.
Wadau wakitoa michango yao katika mjadala huo.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dr Wilbroad Slaa akiuliza swali mara baada ya majadiliano.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dr Wilbroad Slaa akijadili jambo na Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Hellen Kijo-Bisimba (kushoto) na Mwenyekiti wa Mjadala huo, Profesa Chris Maina (kati). Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. ---

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Aliyekuwa makamu mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Mstaafu Augustino Ramadhani amewataka wajumbe wa bunge maalumu la katiba kujadili vipengele vya rasimu hiyo kwa kuviboresha badala ya kulumbana.

Jaji Ramadhani ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati wa mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya OSIEA.

Amesema kuwa, tume ya mabadiliko ya katiba imefanyakazi yake ya kuwasikiliza wananchi na kuandika rasimu ambayo ipo mbele ya wajumbe hao, na hivyo kutoa wito kwao kujadili kwa makuni ili kutengeneza mustakabali mzuri wa Tanzania kwa kuzingatia hoja na kila upande wa Muungano. 

“Sisi kama tume tumefanya kwa kadiri ya uwezo wetu na tumepata rasimu ya pili, sasa ni jukumu la wajumbe wa bunge la katiba kujadili na kuboresha vipengele vilivyomo kwenye rasimu hiyo na kuachana na malumbano”. Alisema Jaji Ramadhani.

“kila mmoja akitaka kipengele chake kiwemo kwenye rasimu hiyo, ni jambo lisilowezekana, kinachotakiwa hapa ni wajumbe kujadili na kupendekeza mambo yenye maslahi kwa taifa kwa sasa na baadae”. Alisisitiza Jaji Ramadhani

Jaji Ramadhni amesema, vipengele vinavyobishaniwa vinajadilika na vinaweza kuboreshwa zaidi kwa malahi ya pande zote mbili ili kupata katiba yenye kutoa nafasi kwa kila upande wa Muungano katika kushiriki katika ujenzi wa taifa. “Vipengele vinavyoshindaniwa vinafaamika na wajumbe wanaweza kutumia busara kuvijadili na kuvitolea maamuzi kwa manufaa ya nchi ambayo inasubiri kwa hamu Katiba Mpya” alisema Jaji Ramadhani.

Akiongelea nafasi ya vyombo vya habari kwenye mchakto huo Muhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dr Ayoub Rioba amesema, bado vyombo vya habari havijapewa nafasi ya kutosha kisheria kushiriki katika kuelimisha umma kuhusiana na mchakato huo.

“ Vyombo vya habari bado havijapewa nafasi yoyote kwenye mchakato huu bali vinafanya kazi kwa mazoea na pia kuna vipingamizi vingi vinawekwa kuwazuia waandishi wa habri kuandika habari za bunge la katiba” alisema Dr Rioba.

Kamishana wa zamani wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar –ZEC, Dr Nassor Seif Amour amwataka wajumbe wa Bunge la katiba kuzingatia matakwa ya wananchi badala ya kujadili maoni yao binafsi ama matakwa ya vyama wanavyoviwakilisha.

“Sisi tunawakumbusha wajumbe wa bunge maalumu la katiba kukumbuka maoni wanayoyajidili kuwa ni ya wananchi sasa wasiweke maoni yao ama ya chama katika mchakato huu ili wasitunge rasimu mpya badala ya kuiboresha”. Alisema Dr. Nassor.

Mjadala huo umehudhuriwa na wawakilishi kutoka makundi mbalimbali ya wananchi, asasi za kiraia na wanasiasa.

RIDHIWANI KIKWETE AKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI,KUZUNGUMZIA MWENENDO WAKAMPENI ZAKE.

Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wake na waandishi hao wakati akizungumzia mwenendo mzima wa Kampeni zake,leo April 4,2014,Nyumbani kwake Msoga.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete.

MGOMBEA ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete, amesema akipata ridhaa ya wananchi, atahakikisha anajenga stendi ya mabasi na soko ili kutoa fursa kwa vijana kupata eneo la kuuzia bidhaa zao.



Ridhiwani amesema nia ni kuhakikisha vijana wanaouza bidhaa za vinywaji na zingine waweze kuwauzia abiria wa mabasi yatakayowekewa masharti ya kuingia stendi.



Akizungumza katika mkutano wake na Waandishi wa habari alipokuwa akielezea mwenendo mzima wa Kampeni zake, Ridhiwani amesema kiu yake ni kuona vijana wanapata masoko ya uhakika ya bidhaa zao.



Amesema atashirikiana na  madiwani wa halmashauri kutafuta eneo nzuri la kujenga stendi na soko hilo litasaidia kuinua jimbo la Chalinze kiuchumi.



“Nimesikia watu wanasema kuhamishwa kwa mizani ya Chalinze , vijana watakosa mahali pa kufanyia biashara zao.Kimsingi mizani si eneo la kufanyia biashara kwanza mabasi yanasimama muda mfupi lakini suluhisho ni stendi,”alisema


Alisema lengo ni kuhakikisha wanatumia fursa ya kuwa njia panda ya mikoa ya Kaskazini na Nyanda za juu Kusini na mikoa ya Kati , kuhakikisha kunakuwa na soko la uhakika.

ADA YA KUUOMBEA MWILI WA ALIYEKUWA ASKOFU WA KANISA LA ANGLICAN DAYOSISI YA KATI GODFREY MHOGOLO.

Jeneza likiwa na  mwili wa aliyekuwa Askofu wa kanisa la Anglican Dayosisi ya Dodoma Godfrey Mdimi Mhogolo aliyefariki wiki iliyopita nchini Afrika ya Kusini alikopelekwa kwa matibabu likiwa ndani ya kanisa kuu la Roho Mtakatifu wakati wa ibada maalumu.
Waumini na viongozi wa kanisa la Anglican Dayosisi ya kati wakilishusha Jeneza lilibeba mwili wa aliyekuwa askofu wa kanisa hilo Godfrey Mhogolo ulipofikishwa kwa mara ya kwanza tokea alipofariki nchini Afrika ya Kusini kanisani hapo kwa ajili ya kufanyiwa ibada ya maombezi.
Wachungaji na makasisi wa Kaanisa la Anglican Dayosisi ya Kati wakiwa wamejipanga nje ya kanisa la Roho mtakatifu mjini Dodoma kwa ajili ya kuupokea mwili aliyekuwa Askofu wa kanisa hilo Godfrey Mhogolo.
Waumini wa kanisa la Anglican wakiwa kwenye mahema yaliyowekwa nje ya kanisa kuu la Roho Mtakatifu walipokuwa wakifuatilia ibada ya kuuombea mwili wa aliyekuwa Askofu wa Kanisa hilo kanda ya Dodoma  aliyefariki wiki iliyopita alipokuwa kwenye matibabu nchini Afrika ya Kusini.
Wageni mbalimbali kutoka nje ya nchi wakiwa ndani ya kanisa la Roho Mtakatifu kwa ajili ya ibada maaumu ya kuuombea mwili liyekuwa askofu wa kanisa hilo Godfrey Mhogolo aliyefariki wiki iliyopita alipokuwa kwenye matibabu Afrika ya Kusini.
Ndani ya kanisa la Roho mtakatifu waumini wakifuatila ibada ya kuuombea mwili wa aliyekuwa askofu wa kanisa hilo Godfrey Mhogolo aliyefariki wiki iliyopita akiwa kwenye matibabu.
Baadhi ya Viongozi wa Serekali wakiwa kwenye ibada hiyo.
Waumini wa kanisa hilo wakiwa ndani ya hema lilijengwa katika eneo la makaburi ya kuzikia viongozi wa kanisa la Anglican Dayosisi ya kati ambapo walikuwa wakiandaa sehemu ya kuuzikia mwili wa aliyekuwa Askofu wa Kanisa hilo Godfrey Mhogolo unaotarjiwa kuzikwa leo Jumamosi.
PICHA NA JOHN BANDA WA PAMOJA BLOG

Friday, April 4, 2014

WAONYESHA UZALENDO KWA KUSAFISHA MIFEREJI MTAA MZIMA.

Ili kuonyesha kuwa wamehamasika na kampeni ya Onyesha Uzalendo Tangaza Upendo iliyoasisiwa na kituo Cha Radio Clouds Fm nchini, vijana wa mtaa wa Mwaloni karibu na soko kuu la samaki Mwaloni Kirumba Mwanza wameamua kujitolea kuzibua mifereji ya maji taka mtaa mzima ili kurahisisha utiririshaji wa maji kipindi cha mvua.
Vijana hao wapatao saba ambao walisema majina yao siyo muhimu zaidi ya vitendo wamesema kuwa ni elimu tu inahitajika kwa jamii yetu kubadilika na kuwa watekelezaji zaidi ya wazungumzaji na kwa kuliona hilo wameamua kuanza katika mtaa wao ili vijana wegine waige mfano.

Wamesema kuwa utunzaji wa mazingira ni njia ya kuendeleza afya kwa njia ya kuzuia mawasiliano ya binadamu na athari za taka. Athari zinaweza kuwa za kimwili, mikrobiyolojia, biyolojia au kemikali vikolezo vya ugonjwa. 

Wameyafanya hayo wakijua kabisa kuna baadhi ya wananchi wenzaomtaani hutupa taka zisizo pashwa kutupwa kwenye mifereji ya wazi kama  vile kinyesi, taka ambazo zinaweza kusababisha matatizo ya afya kwa binadamu na wanyama.

  Taka nyingine zisizofaa kwa mifereji ya mitaani iliyo wazi ni pamoja na taka ngumu, maji machafu, taka za viwandani, na taka za kilimo. 

Usafi kama huu ni njia ya kuzuia magonjwa unaweza kutumika kwa ufumbuzi handisi (kama majitaka na matibabu ya maji machafu.

Upungufu wa usafi wa mazingira ni sababu kuu ya maradhi duniani kote hivyo uboreshaji wa mazingira una manufaa makubwa kujikinga na athari mbalimbali kwa afya ya wote katika kaya na katika jamii. Big up kwa kuonyesha Uzalendo kwa vijana wa Kirumba.

PICHA ZA MATUKIO SHEREHE ZA WIKI YA ELIMU WILAYANI ITILIMA.

Bango la makaribisho.
Mgeni rasmi aliyealikwa kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Simiyu bwana Maganga na mkuu wa wilaya ya itilima Georgina Bundala wakiwasili katika sherehe hizo.
Wananchi walio hudhulia katika sherehe hizo za wiki ya Elimu .
Mwanafunzi bora wasomo la hesabukandayamagharibi akikabidhiwa cheti na fedha taslimu kutoka shule ya sekondari Nkoma.
Baadhi la walimu walio tunukiwa vyeti kwaajili ya ufundishaji wao uliofanya wilaya pamoja na wanafunzi kufaulu masomo yao.
Diwani wa kata ya migato akipokea cheti cha kiongozi bora katika shereheza wiki ya elimu   wilayani Itilima.
Wananchi. 
Mwakilishi wa mkuu wa mkoa Bwana Maganga akitoa hotuba kama ilivyoandaliwa na mkuu wa mkoa wa Simiyu.
Baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari Itilima, Inalona.
PICHA: FAUSTINE FABIAN.

TAASISI YA BRIEN HOLDEN KUZINDUA HUDUMA YA UPIMAJI MACHO NA UTOAJI MIWANI KWA GHARAMA NAFUU.

Ofisa Mkazi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Brien Holden Vision, Eden Mashayo akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam jana kuhisina na uzinduzi wa upimaji macho utakao fanyika Dar es Slaam free market mkabala na kituo cha DSTV , Kinondoni jijini Dr es Salaam. Kushoto ni Mratibu mradi huo Violet Shirima.
Ofisa Mkazi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Brien Holden Vision, Eden Mashayo akionesha miwani itakayozinduliwa.
********
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa utoaji wa huduma ya macho bure, itakayofanyika Dar es Slaam free market mkabala na kituo cha DSTV , Kinondoni jijini Dr es Salaam.

Ofisa Mkazi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Brien Holden Vision, Eden Mashayo alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema wameamua kutoa huduma hiyo bure kwa sababu inakadiriwa, watanzania Milioni 3.5 wameathirika na ugonjwa wa macho wengi wao ni  wenye umri wa miaka 40 na kuendelea.

Alisema huduma hiyo itaanza kutolewa leo hadi Aprili 11 mwaka huu jijini Dr es Salaam, kuhamasisha watu kuwa na desturi ya kupima macho mara nyingi zaidi.

 ‘’Tumeandaa miwani za aina 12 ambazo saizi zote zinapatikana na tutaziuza kwa bei nafuu kuliko wanavyouza mawakala wengine’’ alisema Mashayo.

Aliongeza kuwa Taasisi hiyo inatoa huduma katika mikoa nane ambayo ni Mbeya, Mwanza, Mtwara, Singida, Iringa, Dodoma, Songea na Lindi.