ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 5, 2014

BINGWA MBIO ZA MITUMBWI KANDA YA ZIWA KUONDOKA NA 2,700,000/=

Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza zawadi za fainali za Kanda za mashindano ya bio za makasia zijulikanazo kama “Balimi Boat Race” zinazo dhaminiwa na bia ya Balimi Extara Lager zinazo tarajiwa kufanyika katika ufukwe wa Mwaloni jijini Mwanza leo.
Na Mwandishi Wetu.Mwanza
Bingwa wa fainali za mashindano ya mbio za makasia Wanaume, chini ya udhamini wa Bia ya Balimi Extra Lager yajulikanayo kama “Balimi Boat Race 2014” anatarajia kujinyakulia kitita cha pesa taslimu Shilingi Milioni 2,700,000/=,Kikombe pamoja na medali za dhahabu kwa wanakikundi hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa Bia ya Balimi Exra Lager, Edith Bebwa alisema fainali hizo zitaanza majira ya saa tatu na asubuhi na kuendelea katika ufukwe wa Mwaloni jijini Mwanza ambapo jumla ya vikundi 15 vya Wanaume kutoka katika mikoa mitano ya Kanda ya ziwa vitachuana kumtafuta bingwa wa Kanda kwa mwaka 2014 na vikundi 11 upande wa Wanawake.
Edith alisema mikoa ya Kanda ya Ziwa inayoshiriki ni Kigoma,Kagera,Mwanza,Musoma na Kisiwa cha Ukerewe ambacho kinabeba hadhi ya Mkoa.

Mshindi wa pili Wanaume atazawadiwa pesa taslimu Shilingi 2,300,000/=,mshindi wa tatu Shilingi 1,700,000/= na wa nne 900,000/=.Wakati mshindi wa tano hadi wa kumi watapata kifuta jasho cha pesa taslimu Shilingi 400,000/= kila kikundi alisema Edihi.

Upande wa wanawake bingwa wa mwaka 2014 ataibuka na kitita cha pesa taslimu Shilingi 2,300,000/=,kikombe na medali za dhahabu kwa wanakikundi wote.Mshindi wa tatu atazawadiwa Shilingi 1,700,000/=,wa tatu Shilingi 900,000/= na wa nne 700,000/= wakati mshindi wa 5 hadi wa 10 watazawadiwa kifuta jasho cha pesa taslimu Shilingi 250,000/= kila kikundi.

Nae Meneja wa Kampuni ya Bia nchini Kanda ya Ziwa, Malaki Sitaki aliwaomba wakazi wa jiji la Mwanza na vijiji jirani kujitokeza kwa wingi katika ufukwa wa Mwaloni kushuhudia fainali hizo zenye mvuto wa pekee na mwisho wafahamu nani atachukua ubingwa wa mbio hizo kwa mwaka 2014.


Meneja matukio wa TBL Kanda ya Ziwa, Erick Mwayela alisema vikundi vyote vimeshawasili jijini Mwanza tayari kwa mpambano wa kumpata bingwa wa mwaka huu na maandalizi kwa ujumla yamesha kamilika hivyo nae aliwaomba watu wajitokeze kushuhudia mbio hizo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.