ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 4, 2014

SHIRIKA LA KIMATAIFA LA COMPASSION LILIVYO FANIKIWA KUBORESHA MAISHA YA AKINAMAMA NA WATOTO MKOANI MWANZA

Mwalimu wa kituo cha Huduma ya Mtoto kanisa la Babtist lililopo Kona ya Bwiru Mwanza akizungumza na wageni wa UN waliotembelea kituo hicho kujionea utekelezaji wa huduma wanazozitolewa, ziara iliyolenga kukagua utendaji katika miradi iliyolenga kutekeleza malengo ya maendeleo ya millennia (MDG) na dira ya taifa 2025.    
BOFYA PLAY KUMSIKILIZA

 “Imekuwa kasumba ya watanzania waliowengi kulalamika bila kufanya kazi kwa bidii, maarifa na uadilifu hivyo ni lazima tuwe na mkakati na tunataka tuwe na kizazi sio cha wanung’unikaji na walalamikaji tunataka tuwe na kizazi chenye kutafuta suluhisho ufumbuzi wa matatizo na suala ya kuwasaidia watoto yatima ni jukumu letu sote kuanzia ngazi ya familia hadi taifa” 
 Pichani ni baadhi ya watoto walionufaika na mpango wa maendeleo wa Compassion Mwanza.
 Picha za ukutani.
 Alisema kuwa mkazo mkubwa umewekwa katika kuwatoa na kuwakomboa watoto waishio mazingira magumu, kuwasaidia kutoka kwenye hali za umasikini wa Kiuchumi, kiroho, Kijamii, na Kimwili na hatimaye kuwawezesha kuwa watu wazima wanaoujua wajibu wao, na wanaojitosheleza.
Moja kati ya malengo  yaliyowekwa na Kituo cha Huduma ya Mtoto ni pamoja na kuendelea kutoa huduma kwa kushirikiana na makanisa yenye ushirika wenza katika misingi ya uadilifu, utu na kuwa mawakili wema wa rasilimali za watoto na jamii na kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa katika vituo vyao vyote. 
Kutoka eneo moja kwenda jingine.
Bi hawa athumani akihadithia jinsi maisha yake yalivyo badilika mara baada kusota kwa kipindi kirefu akiishi kaika kibanda ambapo sasa anamiliki nyumba yake nzuri ya kisasa.
Pamoja na kusaidia watoto waishio mazingira magumu pia shirika la Compassion limewasaidia baadhi ya akina mama katika kuwapa elimu ya Ujasiriamali , Elimu isiyokuwa rasmi, Elimu kwa Wazazi,  Maji, Usafi na kuboresha mazingira yao kama jinsi lilivyomsaidia Bi. Hawa ambaye alikuwa amekata tamaa ya maisha kutokana na kuishi katika hali duni bila msaada. BOFYA PLAY MSIKILIZE 
Wadau wa UN wakiwa katika picha ya pamoja na Bi. Hawa Athumani, na aliye keti ni mume wa Bi. Hawa.
Wadau wa UN na Shirika la Compassion wakiagana na familia ya Bi. Hawa Athumani
SHIRIKA la Compassion International Tanzania limekuwa na mahusiano mazuri na kushirikiana na Serikali, makanisa na jamii ya watu wote wanaotuzunguka na kushirikiana nao katika malezi, makuzi na maendeleo ya kiujumla ya watoto na vijana.

Katika Afrika Mashariki ukiondoa Tanzania shirika hilo lipo Rwanda, Kenya, Uganda na Ethiopia na tayari limezalisha wasomi wengi wakiwemo madaktari na wauguzi wahasibu, wanasheria na askari ambao kwa sasa wamekuwa tegemeo kubwa kutokana na ufadhili unaotolewa na shirika hilo.

Shirika hilo la compassion internation Tanzania lilianzishwa rasmi tarehe 30/4/1999 lengo ikiwa ni kuhudumia watoto wahitaji ili kuwatoa katika umasikini wa kiroho,kiuchumi,kijamii na kimwili na baadae lilianzisha ushirika wenza na baadhi ya makanisa ya kiinjili katika mikoa ya lindi ,mtwara,Iringa  na Arusha ambapo ndio makao makuu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.