ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 24, 2014

CHIDI BENZ AKAMATWA AIRPORT NA MADAWA YA KULEVYA.

Kuna taarifa zilitoka on millardayo.com leo jioni kuhusu msanii wa muziki wa kizazi kipya Chidi Benz kukamatwa na dawa za kulevya  katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam akiwa anaelekea Mbeya kwenye show ya Instagram Party ambayo inatarajiwa kufanyika kesho.
Ambapo hatimaye kupitia Amlifanya imefahamika ni kweli msanii huyu amekamatwa leo mchana akiwa katika sehemu ya kuondokea uwanjani hapo ambapo baada ya alifanyiwa upekuzi na kubainika amebeba dawa hizo ambapo ni kete 14 za dawa za kulevya kwenye mfuko wa shati lake na misokoto miwili ya bangi.
Dar es Salaam International AirportKwenye mahojiano kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Hamisi Selemani ambae ni kamanda wa polisi katika viwanja vya ndege Tanzania amethibitisha kukamatwa kwa Chidi Benz na kusema msanii huyu alipohojiwa amekiri kweli kuwa dawa hizo ni zake.
Amesema ‘Alikuja Airport kwa ajili ya safari kwenda Mbeya, kete hizo 14 za dawa za kulevya zilikua zimefungwafungwa na nailoni na pia amekutwa na vifaa vingine vinavyohusiana na watu wanaotumia dawa za kulevya, kuna kigae na kijiko na yeye mwenyewe anakiri ni vitu vyake huwa anatumia ila anashangaa ni kwa nini vimeweza kubaki kwenye mfuko, tutamfikisha Mahakamani baada ya kuweza kubaini ni dawa aina gani za kulevya’
Sauti ya Kamishna Hamis Sulemani akithibitisha tukio hilo unaweza kuusikiliza hapa. BOFYA PLAY KUISIKILIZA.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.