ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 23, 2014

CHAMA CHA BAISKELI CHASIMAMISHA WAJUMBE WAWILI KWA UTOVU WA NIDHAMU.

Katibu Mkuu wa Chama cha Baiskeli Tanzania (CHABATA) John Machemba (kushoto) akitoa tamko la kuwasimamisha wajumbe wawili wa chama hicho ngazi ya Taifa kutoka mikoa ya Mwanza na Arusha baada ya kuthibitisha tuhuma zilizokuwa zikiwakabili. Wengine katika picha ni Mwenyekiti Taifa wa chama hicho Saimon Tungu (katikati) na Katibu msaidizi Fabian Bukanu.
Katibu Mkuu wa Chama cha Baiskeli mkoa wa Mwanza Salum King (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Baiskeli mkoa wa Simiyu, Balele (kulia) walikuwa ni moja kati ya wahudhuriaji kusanyiko la tamko.
Taswira ya mkutano huo.
UONGOZI wa Chama cha Baiskeli nchini Tanzania (CHABATA) umeeleza kuwa uamuzi wa kikao cha Kamati ya Utekelezaji taifa kuwasimamisha Wajumbe wawili wa Chama hicho ngazi ya Taifa kutoka mikoa ya Arusha na Mwanza  kuwa ulizingatia taratibu na kanuni dhidi ya tuhuma zinazowakabili.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza Katibu Mkuu wa CHABATA, John Machemba alieleza maamuzi yaliofikiwa na kikao hicho kilichofanyika hivi majuzi mkoani Shinyanga kuzungumzia mambo mbalimbali ya mchezo huo Kanda ya Ziwa na nchi kwa ujumla.

Machemba alisema kwamba, “Tulipowaita katika kikao baada ya kujadili tuhuma za viongozi hao wawili ili waje kujieleza kwa wajumbe juu ya tuhuma zao ilibainika kuwa tuhuma hizo niza ukweli baada ya wao kukubali baadhi ya tuhuma zao, hivyo kuamliwa kusimamishwa hadi kusubiri maamuzi ya mkutano mkuu taifa,”alisisitiza.

Katibu huyo aliwataja waliosimamishwa ni Moses Andrew (Arusha) na Lucas Bupilipili (Mwanza) ambao ni wajumbe wa Kamati hiyo kufatia tuhuma zinazowakabili ambapo moja ya tuhuma hizo zimedaiwa ni Utovu wa nidhamu walioonyesha hivyo kusubilia majaliwa ya maamuzi ya mkutano mkuu utakaoketi badaye.

Naye Mwenyekiti wa Chama hicho Saimon Jackson alieleza kuwa kikao cha kamati tendaji kiliwachagua Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Seleman Kova kuendelea kuwa mlezi wa chama hicho huku Mbunge wa zamani wa Shinyanga Leonarld Derefa akiteuliwa kuwa mshauri mkuu na wakili Shabani Masamaki pia kuwa mshauri wa Chama hicho.

Jackson aliweka bayana gharama za mashindano ya mbio za baiskeli zilizofanyika mkoani Shinyanga zilizotolewa na wadhamini Kampuni ya Barrick inayomiliki Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi kilikuwa kiasi cha Sh. Milioni 97.5 na kukana kuwepo matumizi mabaya ya sehemu ya fedha hizo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.