ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 25, 2014

AJALI NYINGINE YA NDEGE YAUWA 116.

Abiria wote wa ndege ya Air Algerie waliangamia jangwani
Abiria wote na wahudumu wa ndege ya Air Algerie AH5017 waliangamia jangwani.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametangaza kuwa majeshi ya ufaransa yamefaulu kupata mabaki ya ndege lakini hawakuweza kuokoa nafsi hata moja.
Aidha rais Francois Hollande ametangaza kuwa majeshi hao wamepata mtambo wa kunukuu sauti ''Blackbox'' huko Mali ilikoanguka ndege hiyo iliyokuwa ikielekea mji mkuu wa Algeria Algiers.
Abiria wote wa ndege ya Air Algerie waliangamia jangwani
Ndege hiyo ilikuwa imetoka mji mkuu wa Burkina Faso Ouagadougou ikiwa na Abiria 110 na wahudumu 6 .
Abiria 51 waliokuwa ndani ya ndege hii walikuwa ni raiya wa Ufaransa.
Wengine walikuwa 27kutoka Burkina Faso, 8 kutoka Lebanon , 6 kutoka Algeria , 2 kutoka Luxembourg, 5 kutoka Canada, Wajerumani 4 .
Jamaa ya wahasiriwa wanakutana huko Ougadougu Burkina Faso
Abiria wengine walikuwa mmoja kutoka mataifa ya Cameroon , Ubeljiji ,Misri Ukraine Uswisi Mnigeria na mmoja kutoka Mali.

Waziri wa Usalama wa ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve alisema ndege hiyo iliyokuwa ikielekea Algiers kutoka mji mkuu wa Burkina Faso , Ougadougou,ilianguka kutokana na hali mbaya ya anga. KWA HISANI YA BBC.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.