ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 6, 2014

JULIAS KISARAWE KUMVAA MOROBEST JUN 7

Julias Kisarawe na Morobest wakinyanyuliwa mikono juu kuashiria wamekubalika kuzipiga baada ya kupima na kwenda sawa
Bondia Julias Kisarawe kesho anategemea kupanda ulingoni kuzipiga na Hassan Kiwale "Morobest" .katika ukumbi wa Friends Corner Manzese katika pambano la round nane. 

Akizungumza na vyanzo habari hizi muandaaji Sempai Gola na ofisa wa ngumi za kulipwa nchini Pembe Ndava walisema maandalizi yote yapo kamili, na mabondia wapo katika hali nzuri ukiondoa kasoro ndogo iliojitokeza kwa Moro Best alikuwa acheze na fadhili majia na sasa atacheza na Julias Thomas Kisarawe ambae ni mbadala mkali kwani Kisarawe hajapoteza mchezo katika michezo yake kumi na mbili aliyocheza.mpambano unategemewa kuanza jioni mida ya saa kumi na kutakuwepo na mapambano mengi mno ya utangulizi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.