ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 28, 2014

ULEVI CHANZO CHA KUPOROMOKA KWA MASUMBWI NCHINI

Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akimfua bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mazoezi.

BONDIA namba moja nchini katika uzito wa  light welterweight ,  Ibrahimu Class 'King class Mawe' ameibuka na kukemea vikali tabia ya baadhi ya mabondia kwenda kwenye mapambano ya ngumi bila kuwa na nidhamu au kuchukulia kama wanakwenda 'picnic'.

Ameyazungumza hayo katika ukurasa wake wa facebook mapema hivi karibuni akipinga matukio yanayo fanywa na baadhi ya mabondia wakubwa nchini Tanzania kwa kuingia ukumbini huku wakiwa wamelewa au mkononi wakiwa wameshika chupa za vileo.

Bondia huyo alienda mbali zaidi kwa kusema kuwa bondia anapo kwenda kwenye ngumi yupo kazini kwa kuwa ni kazi kama kazi nyingine hivyo anapokwenda haijalishi siku hiyo anacheza au hachezi, hivyo ni lazima awe na nidhamu kwa mashabiki ili apate wapenzi wengi na wapya zaidi.

Wapenzi wa ngumi wanapatikana kwenye ngumi, "Haiwezekani shabiki anayekutambua akutambulishe kwa watu wenye staha zaoau mashabiki wengine wa ukweli, ohoo 'King Class Mawe' yule ameshika bia" hawezi kukubali na hali hiyo akijua fika atakutana na majibu na maswali "Bondia mwenyewe mlevi namna ile?" Hali hiyo inapoteza mwelekeo wa mashabiki wa mchezo wa masumbwi nchini.

Class aliongea hayo hivi karibuni baada ya mabondia Mada Maugo na Thomasi Mashali kuamua kuzipiga kavu kavu kwa kitu kilichotambulika kuwa wao ni walevi tena wakiwa katika ukumbi wa ngumi Frends Corner Manzese

"Kitendo hiki cha kupigana ovyo sikiingi mkono hata siku moja wakati walishapigana uringoni sasa watafute promota ili wapigane tena" "Kitendo chao cha kupigana ovyo kinatukosesha thamani sisi mabondia chipkizi ambapo mchezo huu wa masumbwi tunautegemea na tunaupenda kwa kuwa tuna malengo nao"

"Ushauri wangu kwa mabondia wasifanye kuwa kwenda kwenye ngumi wanaenda kwenye starehe na kama unajiona wewe mlevi bora ubaki nyumbani kwako unywe basi na si vinginevyo kwa kulewa mbele ya mashabiki wa mchezo wa masumbwi nchini tunaonekana mabondia wote walevi, tafadhalini mabondia wenzangu na samahani kama nitakuwa nimewakwaza nawaomba tushilikiane ili mchezo wa masumbwi usonge mbele. Alimaliza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.