ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 30, 2014

KILI MUSIC TOUR MWANZA YASUBIRIWA KWA HAMU.

Brand Manager wa Bia ya Kilimanjaro kutoka Kampuni ya Bia nchini (TBL) akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo katika ukumbi wa Gold Crest jijini Mwanza tayari kwa mpango mzima wa burudani kesho Jumamosi uwanja wa CCM Kirumba Mwanza. MSIKILIZE HAPA KWA KUBOFYA PLAY.


Kutoka kushoto ni Joh Makini, Richie Mavoko, Laban Mbibo aka Dabo 'The Energy God',na Young Killer wakiwa meza moja kuzungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Mwanza
Mkali wa muziki wa Africa Mashariki mwanadada Mwasiti Almasi ametoa ahadi kwa mashabiki wake kutoa burudani yenye utofauti 'full kiwango' kwani kila siku sanaa yake amekuwa akiiongezea kitu kipya.
Richie Mavoko.
Nikki wa Pili (L), Mwasiti (R).
Kutoka kushoto ni Mwasiti Almasi, Ommy Dimpoz, Ben Paul, G. Nacko, Young Killer na mkali wa Ragga Dabo. 
Tyme ya Ommy Dimpoz kuzungumza na wanahabari.
Richie Mavoko (L) na Joh Makini (R).
BAADA ya Kilimanjaro Music Tour kuonesha mafanikio makubwa Mjini Moshi ambapo show ya kwanza kabisa ilifanyika Jumamosi iliyopita, sasa masikio yote na macho yanaelekea jijini Mwanza ambapo show ya aina yake itafanyika katika uwanja wa CCM Kirumba Jumamosi ya Tarehe 31 na tayari wakazi wa meonekana kuisubiri kwa hamu show hiyo ambayo ndiyo gumzo sasa nchini.

Tayari joto la show hiyo limeshaanza kwa Promosheni mbalimbali natayari imeanza kuleta msisimko mkubwa kwa wakazi wa Rock City huku waadhamini, Kilimanjaro Premium Lager wakiwaahidi wakazi wa Mwanza mambo makubwa zaidi.

Wasanii watakaoipamba show hiyo tayari wako jijini Mwanza ambaoni pamoja na Ommy Dimpoz, Izzo Biznes, Christian Bella, Fid Q, Weusi (Joh Makini, Niki wa Pili, G. Nako) Mwasiti, Young Killer, Vanessa Mdee na Richie Mavoko.

Meneja wa Bia ya kilimanjaro Premium Lager amesisitiza kuwa hii siyo ziara ya washindi a Tuzo za Mziki za Kilimanjaro (Kili Music Awards), bali ni ziara ya kuwasaidia wasanii kutangaza kazi zao mikoani.

"Huwezi kupeleka kila mtu lakini tumejitahidi kuwachukuwa wasanii mbalimbali ili wapelekeburudani mikoani na waweze kutangaza kazi zao" alisema.

Ameongeza kuwa baada ya wakazi wa Moshi kuipokea vizuri ziara hiyo, ni matarajio ya Kilimanjaro Premium Lager kuwa show ya Mwanza itakuwa kubwa zaidi. "Baada ya kutoka Mwanza,ziara hii itaelekea Kahama Juni 7, Kigoma Juni 14, Iringa Juni 21, Mbeya Agosti 9, Dodoma Agosti 16, Tanga Agosti 23,Mtwara Agosti 30, Dar es Salaa September 6"

Kaulimbiu ya mwaka huu ni 'Zungusha Kikwetukwetu' 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.