ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 2, 2014

JAPO KIDUCHU PICHA ZA MEI MOSI MWANZA NA SENGEREMA.

Askari wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Sengerema akiongoza maandamano ya maadhimishio ya siku ya wafanyakazi duniani Mei mosi mjini humo.
Wafanyakazi wa sekta wa mashirika ya serikali, taasisi na makampuni ya watu binafsi walishiriki zoezi hilo. 
Maandamano wilayani Sengerema.
Imependeza.
 "Inapendeza kujumuika japo mara moja kwa mwaka na kujadili changamoto zetu" Kama wanasema wafanyakazi hawa wa wilayani Sengerema.
Ni kutoka Sengerema na sasa tueleke Mwanza mjini (Fuatilia picha zinazo fuata.)
Jijini Mwanza maandamano yafanyika na kuishia Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Meza kuu Mkuu wa wilaya ya Ilemela Amina Masenza (Kushoto) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga wakifurahia yanayojiri toka maonyesho ya wafanyakazi kupitia maandamano.
Wakiteta jambo ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nyamagana Raphael Shilatu (kushoto) na Mkuu wa wilaya ya Ilemela Amina Masenza.
Kama sehemu ya kuboresha afya kwa njia ya mazoezi huyu ni mshindi wa mbio za kufukuza kuku upande wa wanawake ni kutoka TANROAD Mwanza Bi. Mariam John.
Mshindi wa mbio za kufukuza kuku wanaume ni Spilian Kaburu kutoka TANESA.
Michezo ya Nyoka ni jadi ya ngoma za Mwanza.


Chezea burudani macho yote ya wanausalama kwenye 'utamu'.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.