ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 23, 2014

HOSPITALI YA NYAMAGANA KATA YA BUTIMBA YAKABIDHIWA VIFAA.

NA PETER FABIAN, MWANZA.
HOSPITALI ya Wilaya ya Nyamagana iliyopo Kata ya Butimba jijini hapa, mkoani Mwanza, imepatiwa msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya Idara ya Upasuaji na Wodi ya Wazazi wanaotaka kujifungua.



Msaada huo uliotolewa juzi na raia wawili kutoka nchini Canada baada ya kukutana na Meya wa Jiji la Mwanza Stanislaus Mabula na kumweleza kusudio lao la kutaka kutoa msaada wa kijamii ikiwa ni vifaa vya hospitali kwa lengo la kuwasaidia wagonjwa wasioweza kuchangia gharama za matibabu.
Raia Susan Bibbings na mumewe Mark kutoka Jiji la West Voncover BC nchini Canada wakikabidhi vifaa hivyo, walieleza kusudio lao la kulisaidia zaidi Jiji la Mwanza kutokana na maaongezi ya kina waliyofanya na Meya Mabula na kuhamasika na hali halisi waliyoiona katika Hospitali hiyo baada ya kuitembelea.



“Tumetembelea kwenye Wodi za wagonjwa wanawake, wanaume, watoto na wazazi lakini tumeingia chumba cha Upasuaji, X-Ray, Maabara, Meno, Dawa, Masijara na Wodi ya Wamama wajawazito wanaosubiria kujifungua, tumeguswa na tumeahidi kureta misaada zaidi baada ya kurejea nyumbani Canada tutaanza kutafuta wafadhili mbalimbali kutuunga mkono,”alisema Susan.
Ni katika foleni ya kusubiri tiba Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana iliyopo Kata ya Butimba.
Kwa upande wake Meya Mabula alisema kwamba, kutolewa kwa vifaa hivyo kutaongeza chachu ya madaktari na wauguzi kutoa huduma kwa wagonjwa wanaofika katika hospitali hiyo, pamoja na kukabiliwa na changamoto mbalimbali zilizopo katika hospitali hiyo tunaendelea kuzifanyia kazi ili kuhakikisha wananchi wanaofika kupata huduma kwa wakati ikiwa na kupata dawa.

“Marafiki zetu hawa wameamua kutusaidia baadhi ya vifaa katika maeneo ya Upasuaji, Wodi ya wanawake wajawazito wanaosubiria kujifungua, lakini wametuahidi msaada mkubwa ambapo wameeleza kuwa wataleta Kontena la vifaa mbalimbali vikiwemo vifaa btiba na wameonyesha kuguswa na mapungufu waliyoyaona katika hospitali yetu,”alisema.
Aidha Mabula aliwahakikishia Wahisani hao kwamba watakaporeta Kotena la vifaa vya msaada kwa ajili ya hospitali hiyo Halmashauri ya Jiji iko tayari kulipia gharama za Bandarini na usafirishaji hadi jijini hapa ili kuhakikisha masaada huo unaanza kutumika haraka kwa wananchi wa Wilaya na Jiji la Mwanza.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana Ngaila amewashukuru raia hao kwa msaada huo na kuahidi kuutumia vyema ili kusaidia wagonjwa ambao baadhi yao hutibiwa bure ikwemo wazee, watoto na wanawake wanaojifungulia katika hospitali hiyo.
“Vifaa hivi vina ubora unaokubalika na vitatuwezesha kutoa huduma nzuri na imepunguza pengo la vifaa tiba vinavyohitajika ikilinganishwa bado kuna changamoto nyingi kutokana na Bajeti yetu pia kuwa ndogo jambo ambalo hupelekea baadhi ya vifaa tiba kuwa na upungufu kiasi,” alisema Dr. Ngaila.

Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (wa kwanza kushoto) akiwa na marafiki ambao ni  Raia Susan Bibbings na mumewe Mark kutoka Jiji la West Voncover BC nchini Canada kwakiagana kutoka hospitalini hapa mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo vya afya.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.