ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 12, 2014

HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA YAIZAWADIA TIMU MABINGWA WA KOMBE LA DUNIA VIJANA WA MITAANI ZAWADI YA ENEO LA ARDHI KWA KIWANJA CHA MICHEZO.

Mabingwa wa dunia Timu ya vijana wa mitaani wa kituo cha TSC Academy wakiwasili katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa MOIL Aritaf Mansoor aka Dogo ambaye pia ni Rais wa TSC Academy akiwa amelinyanyua juu kombe la Dunia kwa vijana wa mitaani lililotwaliwa na TSC Academy ya Mwanza Tanzania wakati wakuingia katika himaya ya uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evaristi Ndikilo ameongoza maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza katika mapokezi ya Timu ya Watoto wa mitaani TSC Academy ambao ni mabingwa wa dunia iliyowasili leo nyumbani jijini hapa ikiwa ni majira ya saa nane mchana ikitokea mjini Dodoma ambako pia ilipata fursa ya kutembelea Bunge la Katiba linaloendelea sanjari na kulionyesha kombe hilo kwa waheshimiwa.
Licha ya Ofisi yake kuwazawadia wachezaji hao pamoja na benchi lake la ufundi kiasi cha shilingi milioni moja laki mbili na elfu kumi (kila mmoja akipata sh 110,000/=) Ndikilo ameyanyooshea kidole makampuni yanayosita kuwekeza kwenye michezo akisema kuwa hakuna dhambi kubwa kama kukata tamaa, licha ya hayo bado suala la Mwanza kukosa timu ligi kuu soka Tanzania Bara linamuumiza kichwa mkuu huyo..(MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY HAPA CHINI)

Katika mapokezi ndani ya uwanja wa michezo Nyamagana, Halmashauri ya jiji la Mwanza kupitia mkurugenzi wake Hassan Hida aliyekuwa ameambatana na Mstahiki Meya wa Jiji hilo Stanslaus Mabula, imeahidi kutenga eneo la ardhi kama zawadi kwaajili ya kujengwa kiwanja cha soka kwa kituo cha TSC.


Kampuni ya MOIL kupitia Mkurugenzi wake Aritaf Mansoor imetoa kiasi cha dola elfu moja kwa kila mchezaji. Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Antony Diallo amewazawadia kila mchezaji na viongozi full set ya kingamuzi bora cha Continental. 
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evaristi Ndikilo akinyanyua juu kombe la dunia lililo twaliwa na Vijana wa mitaani wa kituo cha TSC Academy cha jijini Mwanza kwenye mashindano hayo yaliyofanyika nchini Brazil.
Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akinyanyua juu kombe la dunia lililo twaliwa na Vijana wa mitaani wa kituo cha TSC Academy cha jijini Mwanza kwenye mashindano hayo yaliyofanyika nchini Brazil.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evaristi Ndikilo akimvisha taji mwenyekiti wa vilabu mkoa wa Mwanza John Kadutu aliye ambatana na timu hiyo nchini Brazil na hatimaye kuibuka mabingwa wa dunia kombe la vijana wa mitaani. 
Mataji kwa wachezaji walio iletea sifa Tanzania.
Mambo kadhaa yamejitokeza leo wakati wa hitimisho la mapokezi ya Mabingwa hao jijini Mwanza moja kati ya yale yaliyowavutia wengi ni simulizi ya changamoto walizokutana nazo kuanzia uongozi wa timu hiyo na hadi wachezaji Mutani Yangwe ni Mkurugenzi wa TSC Academy na hapa anasimulia (BOFYA PLAY KUMSIKILIZA ALICHOSEMA).


Kushoto huyu ndiye kijana aliye pachika mabao matatu ya ushindi yaliyoipatia ubingwa TSC. 
Kocha wa timu hiyo mabingwa wa dunia Suleiman Jabir kutoka Zanzibar amewashukuru uongozi wa TSC kwa kumwamini na kumkabidhi timu licha ya mkoa kuwa na makocha wengi wenye ubora lakini anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumjalia uwezo akili na maarifa kuwaongoza vijana wenye vipaji na hatimaye kuliletea taifa la Tanzania sifa alimaliza na kusema "Muungano Oyeeeeee!!!" kauli ambayo ilishangiliwa kwa nguvu na maelfu ya wahudhuriaji.
Ngoma wa muziki wa ngoma asili kutoka kwa wataalamu wa muziki wa asili kutoka Bujora Mwanza Tanzania.
Bango lajieleza.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Antony Diallo amewazawadia kila mchezaji na viongozi full set ya kingamuzi cha Continental na hapa mkuu wa mkoa alikuwa akikabidhi ikiwa ni zamu ya kocha wa timu hiyo mabingwa wa dunia Suleiman Jabir kutoka Zanzibar.
Moja ya engo ya mahudhurio ndani ya Nyamagana stadium Mwanza.
Picha ya Pamoja.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.