ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 21, 2014

REHEMA MBEGU AIZAWADIA VIFAA KAMBI YA NDONDI YA MWANANYAMALA.

Katibu wa UVCCM akitoa msaada wa gloves kwa Mwinyi Mzengela.
Hapa katibu wa UVCCM akizichapa na mmoja kati ya mabondia wakati wa makabidhiano ya vifaa vya mchezo.
"Hata mimi naweza, ngumi ni mchezo wa wote" ndivyo inavyoonekana akisema bi Rehema Mbegu, hapa akizipiga na bondia Martin Shekivuli
Issa Ommary Peche akizichapa na Mbena.
Bi. Rehema Mbegu akiwa navijana wa kituo cha BigBright pindi alipotembelea kituo hicho.

REHEMA  MBEGU AZAWADIA MABONDIA

MGOMBEA wa kiti cha ukatibu UVCCM  jimbo la kinondoni  bi Rehema Mbegu leo amewazawadia mabondia wa kambi ya bigright ya mwananyamala vifaa vya michezo vyenye thamani kubwa vikiwemo bukta za ulingoni jozi  nane za gloves, vilinda chini(groin guard), na vilinda kinywa (mouth guard).
Bi Rehema mbegu ambae ni katibu wa UVCCM kata ya mwananyamala na kiongozi wa timu ya garden queen ya kinondoni  alitoa vifaa hivyo baada ya kuombwa kwa muda mrefu na vijana hao ambao  yeye pia akiwa kama mlezi wao  awasaidie kufanya hivo.
Akizungumza na wanahabari hizi bi Rehema mbegu alisema  kuwa “kutoa ni moyo na wala si utajiri,niwajibu wetu viongozi kusaidiana katika sekta mbalimbali,  mimi sina uwezo mkubwa  wa kuwatosheleza  kwa  kila kifaa cha mazoezi mnachokihitaji ila ninatoa hivi vichache viwasaidie na kila nipatapo uwezo  sitawaacha nitakuwa nanyi  pamoja kama ilivyo sasa, na  wengine wenye uwezo nimewafungulia njia wajitokezee kuwasaidia mabondia wetu  na ninawaomba wadau wengine wa michezo ,wasiwatenge wanamichezo hasa mabondia, kwani ngumi ni mchezo mgumu na vifaa vyake ni ghali mabondia wenyewe hawamudu kutokana na kipato chao kidogo.hivo tuwasaidie vijana wetu ili tuwaokoe na majaribu ya madawa ya kulevya  na mambo mengine ya kihuni kama wizi, ukabaji na kadhalika.

Nae  kiongozi wa gym ya bigright boxing  ya mwananyamal   amemshukuru  bi Rehema mbegu kwa msaada wa vifaaa hivyo ambavyo wamesema watavitunza na kuvitumia vizuri , na tumepata vifaa hivi katika muda muafaka  hasa katika kipindi hiki cha mashindano  mfululizo yaliyo mbele yetu, kwa  mfano bondia wetu Issa omari nampepeche  atacheza tarehe 29 march na bondia toka Tanga zuberi kitandula katika  pambano la raundi sita kuwasindikiza Japhet kaseba akiminyana na Thomas mashali kugombania ubingwa wa UBO katika ukumbi wa PTA sabasaba, hivyo vifaa hivi vichache vitatusaidia sana katika mashindano haya yanayotukabili tufanye vizuri

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.