ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 28, 2014

MAHAFARI YA 3 CHUO CHA IQRA WASOMI WAASWA KUTOIGA TAMADUNI MBAYA ZA NCHI ZA MAGHARIBI.

Mkuu wa Chuo Cha IQRA Hamza Juma akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilika kwa maafali ya tatu ya chuo hicho, wasomi 98 wamehitimu Astashahada na Shahada katika kozi mbalimbali za Utawala wa Biashara, Teknohama, Uhasibu, Manunuzi na Ugavi, Utenguzi mizigo Bandarini na usafirishaji, Mahusiano na Masoko.
Meza kuu.
Tunuku.
Unastahili.
Wahitimu.
Na vyeti vyao. 
Naibu Meya wa jiji la Mwanza, John Minja akikabidhi cheti kwa mmoja kati ya wahitimu wakati wa mahafali ya tatu ya Chuo cha Utawala wa Biashara na Teknohama cha IQRA, kilichopo Mabatini wilayani Nyamagana, jijini Mwanza.

MWANZA.
WASOMI hapa, wametakiwa kuacha kuiga tamaduni mbaya za mataifa ya Magharibi, ikiwemo ndoa za jinsia moja, ambazo ni kinyume cha maadili yetu na mila za kiafrika.

Wito huo ulitolewa juzi na Naibu Meya wa jiji la Mwanza, John Minja wakati wa mahafali ya tatu ya Chuo cha Utawala wa Biashara na Teknohama cha IQRA, kilichopo Mabatini wilayani Nyamagana, jijini Mwanza.

Hivi karibuni kumekuwepo tetesi kwamba, baadhi ya wanafunzi wanaume wa vyuo mbalimbali jijini Mwanza, tofauti na IQRA, wamekuwa wakijihusisha na Ushoga.

Naibu Meya huyo alisema, wasomi wakiwemo wahitimu wa chuo hicho, wanapaswa kuwa na tabia njema popote wawapo ikiwa pamoja na kufata maadili na tamaduni za kiafrika, wakiiga mambo yasiyofaa ya mataifa ya magharibi, watapotoka na kuongeza mmommonyoko wa maadili.

“Epukaneni sana na tabia za ushoga na ndoa za jinsia moja, mambo hayo hata Marekani hayapo sana na Afrika hatuyahitaji kabisa, Uganda wameyakataa sisi hapa ni kinyume cha sheria kabisa. Nyie mnaohitumu leo msiende kubweteka, kajiendelezeni kielimu.” Alieleza Minja na kuwataka waliohitimu taaluma ya Ugavi na Manunuzi wabishe hodi katika Halmashauri ya jiji la Mwanza, waajiliwe.

Awali akimkaribisha Minja, Mkuu wa Chuo hicho Hamza Juma alieleza kwamba,  katika mahafali hayo ya tatu, wasomi 98 wamehitimu Astashahada na Shahada katika kozi mbalimbali za Utawala wa Biashara, Teknohama, Uhasibu, Manunuzi na Ugavi, Utenguzi mizigo Bandarini na usafirishaji, Mahusiano na Masoko.

Juma alieleza kwamba, chuo chake kinakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo kukosa eneo la kujenga Chuo (wamepanga katika jengo la mtu binafsi), vifaa vya kujifunzia kama Compiyuta na kumshukuru Minja ambaye aliahidi kushghulikia kwa haraka wapate eneo la kujenga Chuo hicho.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.