ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 14, 2014

AIRTEL YAKABIDHI MILIONI 50 KWA MSHINDI WA PROMOSHENI YA MIMI NI BINGWA LEO.

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa makabidhiano ya hundi kwa Mshindi  wa Promosheni  ya Mimi ni Bingwa, aliyejishindia Shilingi Milioni 50, Bw. Kagombo Rashind Jacob (kushoto). Pembeni ni Meneja Masoko wa Airtel , Upendo Nkini.
Meneja Masoko  wa Airtel , Upendo Nkini (kushoto) akikabidhi hundi kwa Mshindi  wa Promosheni  ya Mimi ni Bingwa, aliyejishindia Shilingi Milioni 50, Bw. Kagombo Rashind Jacob (kushoto). Pembeni ni  kushoto ni rafiki wa mshindi huyo Antidius Diocresi.
Mshindi  wa Promosheni  ya Mimi ni Bingwa, aliyejishindia Shilingi Milioni 50, Bw. Kagombo Rashind Jacob (kushoto) akiongea kushukuru kampuni ya Airtel Tanzania kwa kuweza kuanzisha promosheni hiyo ambayo imeweza kumfanya akawa bingwa. Pembeni ni  Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando.
Airtel yakabidhi milioni 50 kwa mshindi wa promosheni ya MIMI ni Bingwa leo 
 
·         Washindi wengine 14 kwenda OLD-TRAFFPORD Uingereza kesho -Ijumaa

 
KAMPUNI ya simu za mkononi ya kupitia promosheni yake ya mimi ni bingwa  iliyomalizika hivi karibuni imemkabidhi mshindi wake BW, Rashidi Kagombora mkazi wa Bukoba hundi ya shilingi milioni 50 leo katika hafla iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel Dar es salaam 
 
Akiongea wakati wa makabidhiano hayo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema “Airtel tunawashukuru wateja wote walioshiriki kikamilifu katika promosheni yetu ya MIMI NI BINGWA, leo tunamkabidhi bw, Kagombola kitita chake kupitia hundi hii ya mfano na baada ya siku chache pesa zake zitaingia katika akaunti yake ya benki moja kwa moja”
 
Vilevile tunafuraha kuwatangazia kuwa jumla ya wateja 14 wa Airtel walioshiriki katika promosheni ya MIMI BINGWA wataondoka kesho kwenda nchini Uingereza jiji la Manchester CITY na watapata nafasi ya kushuhudia soka LIVE kati ya Manchester United na Liverpool siku ya jumapili tarehe 16/03/2014 soka litakalochezwa saa 9 na nusu alasiri. 
 
Washindi wa MIMI NI BINGWA wanaotarajiwa  kuondoka kesho siku ya ijumaa ni GEOFREY DAVID MSITU, JOSEPH STEVEN MAMBO,SEVERA MORIS MATHIAS, HARRSON WILSON, RAFAEL WAIRES KABENGA, EDMUND HENRY KAGIMBO, AMINIYEU NLILIE NATAI, MAULID BARAKA KITENGE, JOSEPH MOSES NDOSSI, CHARLES JOSEPH BUCHWA, GOODLUCK RICHARD KIMARO, RAHABA EUSEBIUS MVUONI, RAJAB SAID MANGARA, na watasindikizwa na  Meneja Masoko wa Airtel Bi UPENDO GILLIARD NKINITunatoa  pongezi kwa washindi wote walioibuka na zawadi mbalimbali  kupitia promosheni hii iliyodumu kwa muda wa miezi mitatu. Pia tunawapongeza wateja wengine wote walioshiriki katika promosheni lakini hawakushinda ikumbukwe kuwa hii ni bahati nasibu hivyo kila mtu anajishindia kwa bahati yake 
 
Nae  mshindi wa Promosheni hiyo Bw, Rashidi Kagombola alisema “ninafurahi sana kuwa mshindi wa mamilioni haya, kwa kweli namshukuru sana mungu kwa kuniwezesha kubadili maisha kwa haraka hivi, leo hii natoa ahadi kwa Airtel na watanzania wenzangu kuwa nitahakikisha nazitumia kwa uangalifu pesa hizi ili kukuza biashara yamgu ya samaki”
 
Promosheni MIMI BINGWA imekwisha huku jumla ya pesa taslim milioni mia tatu ishirini na nne 324 zikiwa zimekwenda kwa wateja toka mikoa na sehemu mbalimbali, vile vile jumla ya washindi wengine 35 wamepata zawadi ya nafasi yakusafiri na kwenda Uingereza katika jiji la Manchester na watalipiwa kila kitu ikiwa ni pamoja na gharama za malazi, usafiri, pamoja na gharama zote za kuandaa safari hadi kupatikana kwa hati ya kusafiria na VISA ya kwenda Uingereza na kushuhudia SOKA katika kiwanja cha OLD Traford cha Mabingwa watetezi wa ligi ya Uingereza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.