ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 17, 2014

MKENYA WA KWANZA KUTINGA OSCAR

>Orodha ya walioteuliwa kuwania tuzo za Oscar, imetolewa.
>Mkenya wa kwanza kuwahi kuwa katika Orodha hiyo pia ametajwa.
Lupita mwenye umri wa miaka 30 amepata uteuzi wa kuwa muigizaji msaidizi bora zaidi katika filamu za mwaka 2013. Si Mwingine bali ni Lupita Nyong'o nyota wa filamu liyowagusa wengi yenye mada utumwa, 12 years a Slave'.
Atamenyana na magwiji wa uigizaji Julia Roberts na Jennifer Lawrence katika tamasha la tuzo za Oscars mwaka 2014.
Babake Lupita ambaye ni mwanasiasa mashuhuri nchini Kenya ameelezea kufurahishwa sana na taarifa hizo na kumtakia kila la heri binti yake.
Kwenye filamu ya '12 years a Slave', Lupita aliigiza kama mtumwa aliyetumiwa kama mtumwa wa kingono na mkubwa wake.
Tangu filamu hiyo iliyotengezwa mwaka 2013, na kutolewa, nyota ya Lupita imekuwa iking'aa kwani amejipata akiwa katika kumbi moja na wagizaji maarufu kama Brad Pitt, Julia Roberts na wengineo hali ambayo kwa wengi itasalia kuwa ndoto.
Alipata uteuzi katika tuzo za Golden Globes za Uingereza ingawa hakuweza kushinda 
THANX TO BBC SWAHILI.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.