ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 14, 2013

WAKAZI WA MWANZA SASA KUTOKA PASIANSI HADI NYEGEZI KWA KUTUMIA KIVUKO CHA MWENDO KASI.









 







BILIONI 1 KUKAMILISHA UJENZI WA DARAJA LA MABATINI NA UJENZI WA NJIA NNE BARABARA YA UWANJA WANDEGE WAJA.

WAKALA wa Barabara Mkoa wa Mwanza (TANROAD) kutumia iasi cha shilingi bilioni 1.3 kukamilisha ujenzi wa Daraja la juu kwa watembe kwa miguu eneo la Mabatini Kata ya Mbugani Wilaya ya Nyamagana  Mkoani hapa.

Hatua hiyo inatokana na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuri kumwaagiza Mkandarasi Kampuni ya Nordic Consstruction Ltd ambapo garama zote zimetolewa kiasi cha shilingi  milioni 888,530,039/= kwa ujenzi na Mkataba wa Usimamizi akilipwa kiasi cha shilingi milioni 135,350,000/=  na kufanya thamani kuwa bilioni1.

Akizungumza na mamia ya wananchi na viongozi mbalimbali wa Mkoa ,Wilaya ya Nyamagana, Jiji la Mwanza leo kwenye hafla fupi ya uwekaji jiwe la msingi katika eneo la mradi huo, alisema kwamba Mkandarasi anatakiwa kutekeleza mradi huo kwa wakati na kuzingatia Mkataba wake kutokana na kulipwa fedha yote.

Dkt. Magufuri alisema kuwa serikali kupitia Wizara yake ya Ujenzi itaendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 kwa uboresha wa miundombinu ya barabara na vivuko vya majini na watembea kwa miguu ikiwa ni madaraja.

“Tuliahidi na sasa tumetekeleza, mnaona leo tumeweka jiwe la msingi na kazi ya ujenzi inaendelea naamini kufikia Desmba 25 daraja hili litakuwa likifunguliwa na sherehe za Chrismas watu watapita hapa na kupata frusa ya kupiga picha kama wanavyofanya kwenye eneo la samaki ikiwa ni kuongeza ajira na utalii”alisema.

“Tumedhamiria kupunguza msongamano wa magari kuingia mjini na kupunguza vifo ambapo takwimu za ajari zinaonyesha zaidi ya watu 12 wamekufa na wengine 20 wamepata majelaha na vilema vya maisha hivyo serikali kuchukua hatua ya kutoa pole kwa waliopoteza maisha na kuwatakia majeruhi kupona haraka amina” alisema.

Aliongeza kuwa serikali sikivu ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete itaendelea kuboresha Miundombinu ambapo hivi sasa Mkandarasi yupo eneo la mradi wa Ujenzi wa barabara ya Lami ya Usagara hadi Kisesa yenye urefu wa kilomita 17 kwa garama ya shilingi bilioni 17.9 zilizotolewa na serikali kwa asilimia 100.

“Tumedhamilia kuondoa msongamano wa magari na watu kulazimika kutumia barabara kufika miji tayari Wizara yangu tayari imeanzisha mchakato wa kujenga kivuko cha kisasa ndani ya ziwa Victoria ambacho kitatoa huduma ya usafiri kuanziaia eneo la Pansiasi kupitia maeneo ya Kirumba mwaloni hadi Nyegezi” alisisitiza

Huku pia akisisitiza kuweka kwenye mipango ya ukarabati wa ujenzi wa barabara za Isamilo, Mabatini hadi zahanati ya Kata ya Mbugani na maeneo mengine yaliyosahulika kwa kuongeza kwenye bajeti ya mwaka ujao kupitia fedha za mfuko wa barabara ili kuiwezesha halmashauri ya jiji kuzijenga na kuziboresha.

Awali Meneja wa Tanroad Mkoa wa Mwanza Injinia Leonarld Kadashi akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi huo alisema kuwa Mkandarasi kwa sasa ameisha tekeleza kwa asilimia 60 ya kazi yake na tayari fidia ya shilingi milioni 9.5 imetolewa kwa uhamishaji nguzo za Tanesco maeneo yote.

“Ujenzi wa daraja hili la kisasa unaenda sambamba na upanuzi wa njia tatu badala ya mbili kwenye barabara ya Nyerere kuanzia eneo la Nata hadi Buzuruga lengo ikiwa ni kupunguza msongamano wa magari kuingia mjini wakati wa asubuhi na kutoka jioni kwani mkandarasi yupo eneo la mradi na utatumia bilioni 2 kwa awamu ya kwanza”alisema na kuongeza.

Kuwa awamu hiyo ya kwanza itaishia eneo la Sinai na awamu ya pili itaanzia Sinai na kuishia kwenye daraja la Buzuruga ikiwa ni pamoja na kuweka taa za kuongozea magari na watembea kwa miguu eneo la makutano ya barabara ya Barnaba na Mahina kwa garama ya bilioni 2 na kufanya thamani kuwa zaidi ya bilioni 4.

Kwa upande wake Meya wa Jiji la Mwanza Stanislaus Mabula aliomba kwa Waziri Dkt. Magufuri daraja hilo kuwekewa uzio ili kuzuia watoto kuvuka kiholela hivyo kuhatarisha maisha yao na kumpongeza kwa juhudi kubwa ya kuendelea kusaidia Jiji la Mwanza ambapo kiasi cha bilioni 1 alichokitoa kwa jiji hilo kinatekeleza ujenzi wa barabara za mawe ambazo ni Mkuyuni-Nyakurunduma, Capil point-Idara ya maji, Sweya-Ihumilo, 

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo ametoa ombi maalumu kwa Waziri Magufuri kuweka mkakati wa kuipanua barabara ya Makongoro inayouelekea Uwanja wa Ndege toka mjini kati kuwa ya njia nne kutokana na kujengwa jengo la kisasa la kitega uchumi la Kituo cha Biashara eneo la Ghana na Upanuzi wa Uwanja wa Ndege unaoendelea kujengwa kwa sasa kuwa na hadhi ya kimataifa.

SALHA ISRAEL ATEMBELEA KAMBI YA TANZANIA TOP MODEL 2013


 Mrembo Salha Israel atembelea kambi ya washiriki wa sindano la Tanzania Top model iliopo katika hoteli ya Jb Belmont iliyopo maeneo ya posta kwa lengo la kuwapa mbinu mbalimbali za kufanya vizuri jukwaani kwani shindano hilo lina upinzani mkali kwa washiriki wenyewe kwa wenyewe.

  Salha alitoa mbinu mbalimbali za kujiamini kwa mwanamitindo awapo jukwaani pamoja na mbinu za kujibu maswali kiusahihi kwa wanahabari ambapo imezoeleka kwa washiriki wengi hushindwa kujibu maswali kiusahihi kitu ambacho hupunguza ari ya shindano.
Washiriki wakimsikiliza kwa makini Salha Israel wakati akiongea nao.
Salha israel mrembo alieng'ara miaka ya 2011 katika mashindano ya urembo nchini,akiongea na washiriki wa Tanzania Top Model 2013 namna ya kujiamini wakiwa katika jukwaa na kujibu maswali endapo watakabiliana na vyombo vya habari.
 Fainali za mashindano haya zitafanyika desemba 7,pia washiriki watapigiwa kura na wananchi ambapo namba maalumu itaolewa hivi punde kumpigia mshiriki umpendae ili kumuongezea alama amabazo zitamwezesha mshiriki wako ashinde.

TSC YAOMBA WADHAMINI KUSAPOTI TANZANIA KUELEKEA KOMBE LA DUNIA LA WATOTO WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU 2014 BRAZIL

                      Kocha Slyvester Mash.                                                       Aritaf Mansoor aka Dogo. 
 NA ALBERT G. SENGO.
MWANZA.

Mazoezi kwa timu ya Taifa ya Tanzania kwa watoto waishio katika Mazingira magumu yaaendelea jijini Mwanza.

Mkurugenzi wa kampuni ya Moil Industry Aritaf Mansoor Dogo amewataka wadau wa michezo pamoja na makampuni mbalimbali kujitokeza kuongeza nguvu katika kudhamini maandalizi hayo sambamba na kuwapatia vifaa vijana hao ili kufikia malengo ya kuutwaa ubingwa wa dunia Kombe la vijana waishio mazingira magumu. (BOFYA PLAY SIKILIZA)

SASA UNAWEZA KUEPUKA MATUMIZI MAKUBWA YA MKAA NA KUNI.

Mchuuzi na wateja wake akiuza jiko la kisasa linalotumia vipande vitatu tu vya kuni ndogo, unawasha kisha moto ukiwaka unavitoa nawe unaendelea na mapishi au uchemshaji maji. kwa ndani kwenye kuta za jiko kuna pumba za mchele au pamba ambazo huwekwa na kushindiliwa vyema zikiacha tundu katikati ambalo husaidia kupitisha moto kwaajili ya mapishi.
Majiko haya yaliyofumwa na mwandishi wa g.sengo blog PETER FABIAN yakiuzwa katika lango kuu la hospitali ya wilaya mkoani Geita yamepata wateja wengi sana kutokana na ufanisi wake na kuwapunguzia gharama za matumizi ya fedha kupitia ununuaji wa mkaa na matumizi ya kuni nyingi. 
Mjasiliamali huyu pia anauza taa zinazo tumia solar yeneye uwezo wa kuwasha taa nne ambazo utazifunga kwenye vyumba tofauti majumbani kwa matumizi ya kutoa mwanga wa kutosha kwa muda wa saa 48. 
Ni solar na taa zake zisizokula umeme mwingi zilizotengenezwa kwa teknolojia ya kisasa kuzalisha mwanga wa kutosha penye giza.
Ni bidhaa zinazozalishwa toka mkoani Arusha na sasa zimevamia kanda ya ziwa kuwaokoa wananchi na kipato chao sambamba na kulinda mazingira kwa kuepuka matumizi makubwa ya ukataji miti kuwa kuni na uzalishaji mkaa.

Wednesday, November 13, 2013

AJALI YA HIVI PUNDE YASABABISHA DEREVA WA BODABODA KUPOTEZA MGUU

TWAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI ZA KUTISHA.
Dereva wa pikipiki ya abiria maarufu kama bodaboda jina halijafahamika mpaka sasa (kwani hawezi kuongea) amepata ajali mbaya na kuvunjika kabisa mguu wake wa kulia mara baada ya kugongwa na roli la mchanga katika eneo la daraja  la Mkolani wilayani Nyamagana nje kidogo ya jiji la Mwanza.
Kwa mujibu wa Mwandishi wa G. Sengo Blog Peter Fabian aliyeweza kuwahi kufika eneo la tukio na kutoa msaada wa gari kumfikisha dereva wa pikipiki hiyo aliyopata ajali Hospitali ya Rufaa ya Bugando, annasema kuwa dereva huyo alikuwa akitokea Mkolani kuelekea Buhongwa na Roli hilo lilikuwa likitokea Buhongwa kuelekea Mkolani, imetokea wakati dereva wa roli 'akiovateki'  daladala iliyokuwa mbele yake ikibeba abilia, hivyo alipoipita tu daladala hiyo akakutana uso kwa uso na bodaboda.
Baadhi ya bodaboda na wasamalia wema wakimbeba majeruhi kumpeleka kwenye gari la MSD Kanda ya Ziwa ili kumkimbiza hospitali ya Bugando.
Hivi ndivyo mguu ulivyo vunjika baada ya kupata ajali.
Sambamba na kuvunjika mguu pia dereva huyo amevunjika vidole vitatu vya mkono wake wa kulia.
NA: PETER FABIAN

AROBAINI YA MARIAM G. MHANDO KUFANYIKA JUMAMOSI HII.

Omar George Mhando wa Muheza Tanga anawatangazia arobaini ya mdogo wake marehemu Mariam George Mhando itakayofanyika Muheza mkoani Tanga, siku ya tarehe 16/11/2013 (Jumamosi).

Marehemu Mariam aliye fariki dunia mnamo tarehe 7/10/2013 akipatiwa matibabu mkoani Arusha na kuzikwa tarehe 10/10/2013 nyumbani kwao Muheza mkoani Tanga, alikuwa mtumishi wa Voda Shop Customer Care Mwanza Kariuwa Investiment.

Kwa watakao penda kushiriki wasiliana na mratibu kwa namba 0754 333 903 or 0715 333 903

JK AUPONGEZA MGODI WA MUWEKEZAJI MZAWA NA MZALENDO KWA KUENDESHA SHUGHULI ZAKE KISASA.

Rais JK akihutubia wafanyakazi na wananchi kwenye mgodi wa Muwekezaji mzawa na mzalendo Baraka anayemiliki kampuni ya Baraka Gold Mine iliyoko mkoani Geita.

Rais Jakaya mrisho Kikwete akipata picha ya pamoja na muwekezaji mzawa na mzalendo Baraka Ezekiel anayemiliki kampuni ya Baraka Gold Mine iliyoko mkoani Geita
Sasa tunaelekea kwenye mradi.
Rais JK alipata fursa ya kutembelea eneo la mradi kujionea hali ya uchimbaji kwa kampuni ya Baraka Gold Mine iliyoko mkoani Geita
Kazi ya uchimbaji ikiendelea.
Eneo la mradi ambalo limeajiri vijana wengi wazawa hivyo kupunguza tatizo la ajira nchini.
Sehemu ya wafanyakazi  370 wa mgodi wa muwekezaji mzawa na mzalendo Baraka anayemiliki kampuni ya Baraka Gold Mine iliyoko mkoani Geita, wakiwa katika maandamano ya kumpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete aliyetembelea eneo lao kujionea shughuli mbalimbali za uchimbaji.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Baraka Gold Mine, Baraka Ezekiel (kushoto) katika picha ya pamoja na Mkuu wa mkoa wa Geita Said Magalula (katikati) na Mkurugenzi wa kampuni ya NSAGALI LTD Emmanuel Gungu anayemiliki mgodi wa katika eneo la Ushirombo, hawa ni wawekezaji wazalendo waliomkuna rais Kikwete kupitia uwekezaji wao wa na kuchangia shughuli za maendeleo ya jamii mkoa wa Geita.
Naibu waziri wa Nishati na Madini Mhe. Steven Masele (kulia)  na Mbunge wa viti maalum Mhe. Vick Kamata (katikati) na Baraka Ezekiel ambaye ni muwekezaji mzawa na mzalendo anayemiliki kampuni ya Baraka Gold Mine iliyoko mkoani Geita.
Mwenyekitii wa CCM Geita Joseph Msukuma (katikati) na kulia ni Emmanuel Gungu Mkurugenzi na miliki wa mgodi wa Nsagali  ulioko Ushirombo wakiwa na Baraka Ezekiel ambaye ni muwekezaji mzawa na mzalendo anayemiliki kampuni ya Baraka Gold Mine iliyoko mkoani Geita.
Naibu waziri wa Nishati na Madini Steven Masele (wa tatu kutoka kushoto) akitoa maelezo kwa Mhe. Rais JK. Wengine katika picha Waziri wa Ujenzi John Magufuli (katikati) na kulia ni Baraka Ezekiel ambaye ni Mkurugenzi wa Mgodi.

Wengine kutoka kushoto ni Ahmed Mbaraka ambaye ni diwani wa kata ya Nyarugusu na Kasim Majaliwa ambaye ni Naibu waziri TAMISEMI anayeshughulikia elimu. 
Wananchi na wafanyakazi wa kampuni ya Baraka Gold Mine iliyoko mkoani Geita wakiwa kwenye kusanyiko la mkutanowa Rais JK alipotembelea mgodi wa muwekezaji mzawa na mzalendo Baraka Ezekiel anayemiliki kampuni ya Baraka Gold Mine.
Wananchi na wafanyakazi wa kampuni ya Baraka Gold Mine iliyoko mkoani Geita wakiwa kwenye kusanyiko la mkutanowa Rais JK alipotembelea mgodi wa muwekezaji mzawa na mzalendo Baraka Ezekiel anayemiliki kampuni ya Baraka Gold Mine.
NA: PETER FABIAN.