ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 27, 2013

MWANZA HUDUMA YATOA MIFUKO 200 YA SARUJI KUBORESHA VYOO VYA SHULE 4 ZA MSINGI WILAYA YA NYAMAGANA

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga wa pili kulia pamoja na Mkurugenzi wa Duka la vifaa vya ujenzi la Bw. Zuri Nanji wa kwanza kulia wakikabidhi mifuko 50 kwa uongozi wa shule ya msingi Butimba Mazoezi  A na B iliyopo Kata ya Butimba kwaajili ya ujenzi wa vyoo vya shule hiyo. 
 MKUU wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga jana alikabidhi jumla ya mifuko 200 ya  saruji kwa shule nne za msingi katika Kata nne za Wilaya hiyo ikiwa ni mkakati wake wa kuchangia, kuhamasisha mendeleo na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa vitendo.

Konisaga ambaye amekuwa akihamasisha mkubwawa maendeleo na kuhakikisha kero mbalimbali za kijamii zinatafutiwa ufumbuzi wa haraka kwenye sekta zote ambapo katika msaada huo alioukabidhi kwa lengo la kupunguza upungufu wa matundu ya vyoo kwenye baadhi ya shule hizo zinazokabiliwa na changamoto hiyo kutokana na wingi wa wanafunzi.

“Msaada huu wa saruji mifuko 200 umetolewa kwangu na mfanyabiashara maarufu Jijini Mwanza Zuri Nanji maarufu kwa jina la ‘Mwanza Huduma’ ambaye alikuja ofisini kwangu na kuniahidi kunisaidia kwenye sekta ya Elimu lakini kwa shule za msingi na eneo alilopendekeza ni kwenye ujenzi wa vyoo ili kusaidia kuongeza matundu ya vyoo jambo ambalo litasaidia kupunguza msongamano kwa wanafunzi wakihitaji kujisaidia”alisema

Mkuu huyo wa Wilaya alisema kwamba kutokana na msaada huo aliamua kuugawa kwenye shule za msingi nne kati ya 81 zilizopo katika Wilaya hiyo ambapo shule zilizonufaika na msaada huo ni Butimba Mazoezi  A na B iliyopo Kata ya Butimba, Ibanda iliyopo Kata ya Mkolani, Igogo B iliyopo Kata ya Igogo na Igoma iliyopo Kata ya Igoma.
Pamoja na makabidhiano hayo yaliyofanywa shule ya msingi Butimba imeendeleza juhudi zake za ujenzi wa vyoo ili kupunguza makali ya changamoto iliyopo.

Msafara wa Mkuu wa wilaya ya Nyamagana na wadau wake ukirejea toka kwenye ukaguzi shule ya msingi Butimba Mazoezi  A na B iliyopo Kata ya Butimba..

Konisaga pia alipata fursa fupi ya kuzungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Butimba Mazoezi  A na B iliyopo Kata ya Butimba.

Makabidhiano ya Mifuko 50 ya saruji kwa shule ya Msingi Mkolani.

Waalimu na wanafunzi shule ya msingi mkolani.

Saruji ikishushwa shule ya msingi Mkolani.

Mifuko 50 ya Saruji kwa shule ya msingi Mkolani. 

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akizungumza na waalimu, wanafunzi na uongozi wa kamati shule ya msingi Igogo ambapo alikabidhi mifuko 50 kwaajili ya ujenzi wa vyoo vya shule hiyo.

Vyoo vya shule ya msingi Igogo ambavyo tayari vimejengwa. 

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akikabidhi Naibu Meya John Minja mifuko 50 ya saruji huku akishuhudiwa na viongozi wa kamati na waalimu wa shule ya msingi Igogo B iliyopo Kata ya Igogo wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza kwaajili ya ujenzi wa vyoo vya shule hiyo.

Kabla ya makabidhiano kwa shule ya msingi Igoma waalimu na wanafunzi walikutanishwa katika ukumbi wa shule hii kwaajili ya kupata changamoto zilizopo.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga (wa pili kutoka kushoto) akikabidhi mifuko 50 kwa uongozi wa shule ya msingi Igoma kwaajili ya ujenzi wa vyoo vya shule hiyo.

“Hali ya vyoo kwenye shule hizi si nzuri sana hivyo Mudau huyu ‘Mwanza Huduma’ ameguswa na hali hiyo na kuonyesha umuhimu wake kutokana na shughuli zake nyingi kuzifanyia Wilayani kwetu kweli ni mfano wa kuigwa kwani shule hizi ni mali ya wazazi ambao wanatakiwa kuchangia uboreshaji wake ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, madawati na matundu ya vyoo” alisisitiza.

Konisaga alisema kwamba wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule za msingi  na sekondariwanao wajibu mkubwa kwa kushirikiana na walimu na kamati zao za shule hizo kuboresha miundombinu kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji na Serikali kwa kuchangia fedha ili kupunguza aidha kuondoa kero mbalimbali kwenye miradi ya maendeleo inayotoa huduma za kijamii kwenye sekta zote kwenye maeneo yao.

“Viongozi wa serikali ni kusimamia ulinzi na amani ya wananchi na kuwahamasisha pia kuchangia miradi ya maendeleo kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji na serikali Kuu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ili kuwawezesha kupatiwa huduma bora kama inavyokusudiwa na wananchi kuwaepuka wanasiasa wanaowahamasisha kutochangia miradi hiyo eti ni jukumu lake hao hawafai  na wasiwaunge mkono”alisema Mkuu huyo.

Konisaga aliwataka viongozi wa Kamati za shule hizo zilizokabidhiwa msaada huo kuacha tabia ya kuweka mafundi na kuwaacha wakichakachua na kufanya ujenzi hafifu na kusababisha majengo hayo kuwa chini ya kiwango na hata kuharibika kwa wakati mfupi jambo ambalo limekuwa likiwakatisha tamaa baadhi ya wadau, wafanyabiashara na wafadhili kuendelea kuchangia tena kwenye miradi mbalimbali ya kijamii.

Naye kwa upande wake Zuri  Nanji ‘Mwanza Huduma’ alisema kwamba hali ni mbaya sana kwenye shule za msingi ambapo kuna watoto wengi (wanafunzi) ambao kutokana na matundu ya vyoo kuwa machache husababisha wanafunzi hao kujisaidia holela na kuharibu mazingira na kuwa hatarishi kwa afya zao ikiwemo kukumbwa na magonjwa ya kuambukiza hali iliyomfanya kusaidi kwa kutoa msaada huo.

“Nitaendelea kuwa mdau wa  kuchangia saruji na vifaa vingine vya ujenzi kwenye shule za msingi na sekondari ili kuhakikisha juhudi za kushirikiana na Jamii na kuiunga mkono serikali kutoa huduma kwa wananchi inatekelezwa kwa wakati kupitia pia sekta binafisi  ili kuwapatia huduma zinazositaili kwenye maeneo yao bila kuwabagua kutokana na tofauti ya kipato”alisema


Kwa mujibu wa maelezo ya kitaalamu ya mafundi wa Ujenzi wa majengo na Mwanza Huduma alieleza kuwa kila Shule hizo zilizopatiwa kila moja mifuko ya saruji 50 yenye uwezo wa kutoa tofari 1400 kwa kila mfuko mmoja wa kilo 50 unaouwezo wa kutoa tofari 28 hadi 32 na kuhitaji maji mengi hali inayoimarisha kuta za majengo na kuwa imara na bora baada ya kukamilika huku vyoo vya matundu 8 vya kisasa vikitumia tofari 450 tu .

BAVON KUSHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA LEO NA WANA BEAT AGENDA HOME MWANZA

 Eh bana siku kama ya leo miaka kadhaa iliyopita ni siku ya kuzaliwa Prizenta wa kipindi kinacho hit' ile mbayaaaa kwa srini yako ndani ya lebo ya TBC1, hapa naizungumzia show ya Beat Agenda, na mbazdeiwa ni ma-men men Bavon.
Yuko tayari 'Rock City' kwaajili ya kujumuika na watu wake wa home kwaajili ya kula bata sambamba na kupokea mibaraka ya Mwanza Kwanza.
Ofcoz jioni ya leo kuna bonge la Party pande hii... Unauliza party wapi? 
Mcheki mwenyewe kwa sms...'''' 

Halla to Yaaa!! 
Happy Birthday Bavon.

Friday, July 26, 2013

TAIFA STARS YAPASWA KUSAHAU YALIYOPITA ILI KUFUZU MTIHANI WA KESHO DHIDI YA UGANDA

Kabla ya kuondoka jijini Mwanza ambako Stars walikuwa wameweka kambi waliagwa uwanja wa ndege wa Mwanza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alikuwa akielekea mkoani Kagera kwenye maadhimisho ya siku ya Mashujaa.
Uganda The Cranes wanayo kila sababu ya kuingia kwenye fainali za CHAN mwakani ila hilo litakamilika mara baada ya kuvuka kikwazo kikubwa kwa kuidhibiti timu ya soka ya Tanzania Taifa Stars katika mchezo wa pili hapo kesho jumamosi.
The Cranes walioweka historia nzuri kwa mashindano yaliyopita ya mwaka 2011 yaliyofanyika nchini Sudan mpaka sasa wamekwisha tumbukiza mguu mmoja kwenye fainali za mashindano hayo ambazo zitakwenda kupigwa nchini Afrika ya Kusini mara baada ya kufanikiwa kuilaza Tanzania bao 1-0 katika mchezo uliofanyika jijini Dar es salaam.
The Cranes wanakutana uso kwa uso na Taifa Stars Jumamosi ya kesho ya tarehe 27 kwenye uwanja wa Mandela National Stadium katika mchezo unaotajwa kuwa utakuwa ni wa vuta nikuvute.
Taifa Stars walipokuwa kambini Mwanza.
TATHIMINI:-The Cranes have not lost at home since the controversial 1-0 loss to South Africa in 2004. Between that period and now, Cranes have managed to tame Africa giants Nigeria, Zambia, Angola among others and also earned a respectable draw against 2002 World Cup quarter finalists Senegal. Added to the fact that Tanzania are poor travelers, the Cranes have an edge. Question is, can Kim Poulsen’s charges bring the record to halt?
Uganda’s good record against Tanzania: Uganda Cranes have a formidable record against Tanzania with 24 victories while Tanzania has only managed 11. Besides, the Cranes have garnered victories in the previous two meetings (3-0 duringCecafa Tusker Challenge Cup and 0-1 in the Chan qualifiers).
Uganda leads on aggregate: Going into the final leg, the Cranes just need to avoid defeat to advance to the finals. The Cranes won the first leg encounter at National Stadium, Dar es Salaam thanks to Denis Guma’s solitary goal. It remains to be seen whether Taifa Stars can overturn the result but this is unlikely given the Cranes are home.
Micho’s tactical acumen and knowledge about Tanzania Soccer: Unlike his counterpart Kim Poulsen, Uganda Cranes Coach Micho is a bit knowledgeable about Tanzanian football than Kim knows about Uganda.
The Serb has faced Tanzanian players as national team and club coach during his SC Villa days plus he spent a full season at Yanga FC where he won the league title un beaten. During this time, he coached a number of players in the current Taifa Stars side and played against many as his opponents. This helps him plan his tactics according to opponents like it happened in the first leg.
Taifa Stars are predictable: There is nothing as better as planning to solve a problem you are well versed with. This is exactly what Cranes and Micho have as they face Tanzania. The Tanzanian squad is a bit predictable since it’s the same squad that features in other competitions including CecafaAfcon and World Cup qualifiers. This is opposite to the current Cranes side which has only Hamza Muwonge, Denis Guma and Hassan Wasswa as regulars in the side.
Can Taifa Stars against all odds beat Uganda at home? Hilo ndilo swali jibu lake kupatikana kesho.

MWANDISHI WA HABARI JACLINE AAGWA NA KUZIKWA LEO KITANGILI JIJINI MWANZA

Marehemu Jackline Wanna Since 1970 - 23/07/2013.


Mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari mwanamama Jacline Wanna umeagwa leo nyumbani kwake eneo la Nyamanoro, kisha ukazikwa katika makaburi ya Kitangiri jijini Mwanza


Mwandishi wa Habari Leo Grace Chilongola akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Jacline Wanna.


Wakijumuika kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Jacline Wanna ni safu ya waandishi wa habari mbele ni Novatus Makongo


Heshima kwa mwili wa marehemu zikiendelea.


Sitta Tuma akitoa heshima kwa mwili wa marehemu Jacline Wanna.


Radio Maria nayo iliwakilishwa.


Mwili wa marehemu ukitolewa nyumbani kwake kuelekea mazikoni.


Majira ya saa 9 na dakika kadhaa msafara kuelekea makaburi ya Kitangiri.


Ni katika eneo la makaburi ya Kitangiri.


Mwili wa marehemu ukishushwa kwenye nyumba yake ya milele.


Mashuhuda.


Uliumbwa kwa udongo na mavumbini utarudi.


Shukurani za MPC ziliwasilishwa na Makamu Mwenyekiti Mr. Mpagaze


Salamu za UTPC ziliwasilishwa na Victor Maleko.


Katibu wa Mwenezi wa CCM Wilaya ya Nyamagana Mr. Mustapha aliwakilisha salamu za Chama cha mapinduzi.


Waandishi wa habari wakiweka maua kwenye kaburi la hayati Jacline Wanna.


Wakiweka mashada ya maua kwenye nyumba ya milele ya mpendwa wao.


Hawa ni watoto wa marehemu aliowaacha.


Mara baada ya hatua za mazishi kukamilika mume wa marehemu katikati (mwenye kauda suti nyeusi) alijumuika na nduguze katika sala.

ZAMU YA WAPENZI MKOA WA MWANZA KUDUMISHA MAHUSIANO

Ni tukio kubwa la aina yake kwa ajili  ya wanandoa na marafiki walio katika mahusiano, kufanyika Alhamisi ya tarehe 08 Agust  2013, msemaji mkuu wa kongamano hilo ni Mtaalam Chris Mauki.

 Tiketi zimeanza kuuzwa wahi yako mapema, kwa maelezo zaidi piga simu namba 0767224409

Thursday, July 25, 2013

MNEC GACHUMA ALIVYOFUTURISHA WAISLAMU MWANZA

Mgeni rasmi wa hafla hiyo ya futari Mkuu wa Wilaya ya Nayamagana Baraka Konisaga alipata fursa ya kutoa shukurani na neno kidogo kwa wadau waliohudhuria hafla hiyo ya futari iliyoandaliwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM wilaya ya Tarime 'Omary' Christopher Gachuma katika ukumbi wa new Mwanza Hotel na kuhudhuriwa na mamia ya waislamu na wageni wengine.

Mkuu huyo wa wilaya amewaasa wafanyabiashara kuepuka upandishaji bei wa bidhaa kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kwani huwaumiza na kuwakomoa waislamuwenzao kitendo ambacho ni dhambi kwa Mwenyezi Mungu. 

Mashekhe, Mkuu wa wilaya pamoja na mwenyeji wa hafla hiyo ya futari MNEC 'Omary 'Gachuma wakijipatia chakula sahanini.

Marafiki wakiwa kwenye foleni ya maakuli walitumia muda huokupiga soga.

Mbunge wa Lorya Mhe. Lameck Airo akichukuwa chakula na pembeni yake ni Mzee wa Mwanza Charles Masalakulangwa.

Wadau wa PPF waliwakilishwa na Mr. Bandawe (mwenye miwani katikati)

Wadau toka chamani.

Mmoja kati ya Maafisa Uhusiano toka Ofisi za jiji la Mwanza Dr. Kaaya (kushoto) akijadiliana na mwendeshaji wa Hafla   hiyo ya Futari, Shekhe Hassan Kabete (kulia) na katikati ni Mkurugenzi wa Radio Metro Fm Hamran Batenga.

Kiduarisho hiki kiliwakilishwa na wadau hawa wa nguvu.

Meneja wa Airtel kanda ya Ziwa Ally Maswanya akiwa na wadau wake naye alijumuika kwenye kusanyiko hili la kirafiki zaidi.

Mwenyeji wa Hafla hiyo ya futari MNEC Gachuma (kulia) akiwa na Katibu wa BAKWATA mkoa wa Mwanza Shekhe Mohamed Bara.

Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (katikati) akiwa na mwenyeji wake MNEC 'Omary' Gachuma (kushoto) na wadau wengine wakipata futuru huku wakisikiliza yanayojiri.

Jumuiko la kirafiki.

Mara baada ya kufuturishwa dua fupi ilisomwa sambamba na shukurani kwa tukio hili ambalo limekuwa na ada ya kufanyika kila mwaka mara moja msimu huu..

Jumuiko.

Ni tukio jema...

Inshahlah Mwenyezi Mungu aendelee kumjalia muandaaji, Mweshimiwa Gachuma aendeleza ibada hii ambayo imekuwa chachu kwa Wanamwanza kudumisha amani na Upendo kwani huwakutanisha watu wa dini mbalimbali na kushiriki tukio la imani moja kiurafiki zaidi.