ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 13, 2013

WAKAZI WA TABORA WACHANGAMKIA MCHEZO WA POOL

Mchezaji wa timu ya Texas pool klab ya Mkoa wa Tabora Salum Kazuga akijitayarisha kupiga mpira wakati wa mazoezi ya klabu yao iliyofanyika mkoani hapo jana. 

Mchezaji wa timu ya Texas pool klab ya Mkoa wa Tabora Shabani Ramadhani akijitayarisha kupiga mpira wakati wa mazoezi ya klabu yao iliyofanyika mkoani hapo jana picha na SUPER D

Friday, July 12, 2013

MKAPA AFANYA ZIARA FUPI YA GHAFLA KUIMARISHA UTENDAJI OFISI ZA CCM MKOA MWANZA

Rais Mtaafu Mhe. Benjamin William Mkapa akisaini kitabu cha wageni ofisi za CCM mkoa wa Mwanza ambapo alifanya ziara ya kuimarisha Chama kiutendaji kwa kazi za ndani.

Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya masuala muhimu ya chama mbele ya Rais Mstaafu pamoja na makada na viongozi wa ngazi mbalimbali mkoa wa Mwanza.

Wafanyakazi wa CCM mkoa wa Mwanza walijumuika na kikao hiki cha ghafla kilichofanywa na Mhe. Rais mstaafu.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Mkoa wa Mwanza akitoa malezo ya hatua na maendeleo ya umoja wake mbele ya Mhe. Rais mstaafu Ben Mkapa.

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akitoa malezo ya jinsi kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Mwanza ilivyojipanga kuhakikisha wananchi wanaishi salama bila hofu .

Mhe. Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akitoa maelekezo na uzoefu kwa makada na viongozi wa CCM mkoa wa Mwanza hii ilikuwa mapema leo kabla ya kushiriki hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo la BMC inayofanyika leo usiku Gold Crest Hotel Mwanza.

Mkapa akiagana na wadau wa CCM mkoa wa Mwanza mara baada ya kumaliza kikao hicho.

MWILI WA HUMPHREY SIMON (MASWI) WAAGWA JIJINI MWANZA: KUZIKWA KESHO MUSOMA

Jeneza lililoubeba mwili wa marehemu Humphrey Simon likiwa limewasili Nyumbani kwake Nyakato Sokoni kwaajili ya heshima za mwisho na kukesha kisha kesho asubuhi safari kuelekea Musoma kwa mazishi.

Wakati ukipokelewa nyumbani kwake toka hospitali ya rufaa Bugando.

Mc Bonke akiongoza shughuli na taratibu nzima msibani.

Mjomba wa marehemu Archtc. Tega akitoa taratibu za jinsi familia ilivyopanga juu ya safari ya mwisho ya kuuhifadhi mwili wa marehemu.

Ilikuwa ni majonzi wakati mke wa marehemu Humphrey Simon, Bi Neema akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu mumewe ambaye walifunga ndoa mwaka juzi tu (2011)

Ndugu jamaa na marafiki wakitoa heshima zao za mwisho.

Hatua za kuuaga mwili wa marehemu zikiendelea kwa upande wa akinamama.

Bibi wa marehemu alipata wakati mgumu.

Marafiki wa marehemu wakiuaga mwili wa marehemu mbele ni Mr.Dinno akifuatiwa na Mr. Chacha.

Mjomba wa marehemu akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu mwanaye.

Huzuni kwa marafiki: Dada Less akiuaga mwili wa marehemu.

Ibada ya kuuaga mwili wa marehemu ilifanyika jioni ya leo kisha mwili utalala hapa nyumbani kwa marehemu ambapo kesho jumamosi asubuhi safari kuelekea Musoma itafanyika kwajili ya mazishi.

AIRTEL YATOA FUTARI KWA WATOTO YATIMA MIKOA MINNE

Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye hafla fupi ya makabidhiano  ya vyakula vya kufuturisha watoto yatima katika vitu vilivyopo mikoa ya Dar es salaam, Mbeya, Arusha, Mwanza katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani iliyofanyika  katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salam , akifuatiwa na meneja wa huduma za Jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi

Meneja  Uhusiano wa Jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi  akimkabidhi mwakilishi wa Bakwata Ustadh Hassan Malangali vyakula vya kufuturisha katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani  vilivyotolewa kwa vituo vitatu vya watoto yatima Dar es Salaam (hawapo pichani)  vituo vitakavyofaidika zaidi ni vya Dar es salaam, Mbeya, Mwanza, Arusha hafla ya  akabidhiano iliyofanyika  katika ofisi za Airtel  Morocco jijini Dar Es Salam

Meneja  Uhusiano wa Jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi  akiwakabidhi Saida Makope mmoja wa wakilishi wa kituo cha watoto yatima mjini Dar Es Salaam  katika  hafla fupi ya makabidhiano  ya vyakula vya kufuturisha katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani  vilivyotolewa kwa vituo vitatu vya watoto yatima jijini Dar Es Salaam  iliyofanyika katika ofisi za Airtel  Morocco jijini Dar Es Salam  akifuatiwa na mwakilishi wa Bakwata ustadhi Ustadh Hassan Malangali .

.

AIRTEL YATOA FUTARI KWA WATOTO YATIMA MIKOA MINNE
*       Wateja Airtel sasa kupata muda wa dua, nukuu za qurani, mawaidha kwa kutuma neno Ramadhani kwenda 15322 kwa shilingi 153 tu kwa siku. Kampuni za simu za mkononi za Airtel Tanzania kupitia Kitengo chake cha huduma kwa Jamii wametoa msaada kwa vituo vitatu jijini Dar Es Salaam vya watoto yatima katika mwezi mtukufu wa Ramadhani vikifuatiwa na vituo vingine katika mikoa ya Arusha, Mwanza na Mbeya ili kusaidia watoto wanaolelewa kwenye vituo hivyo.

Msaada huo umetolewa kwa lengo la kuwalenga watoto kutoka mikoa minne ambayo ni Dar Es Salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya kwa watoto hawa wanaohitaji upendo  hususani katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani. Baadhi ya vitu vilivyotolewa ni Mchele,Sukari, maharagwe,unga, mafuta ya kupikia,maziwa, juice, majani ya chai na
sabuni vyenye dhamani ya shilingi milioni tano na nusu.

Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano iliyoandaliwa katika makao makuu ya  Airtel jijini Dar Es Salaam, Meneja uhusiano wa huduma kwa Jamii bi Hawa Bayumi alisema "kwa kutambua umuhimu wa Jamii tunayofanya nayo biashara kampuni ya Airtel tumeamua turudishe kiasi cha faida tunayopata kwa wananchi ili iwasaidie.

Akifafanua alisema kwa muda wa miaka 11 iliyopita tumeweza kusaidia Jamii mbalimbali ya watanzania ndani ya mfungo wa Ramadhani na bila kuacha nyanja za elimu, michezo kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na kukosa huduma mbalimbali za kijamii.

Kwa mwaka huu kupitia Kitengo chake cha huduma kwa Jamii tutarudisha tulichokipata na tutaweza kufikia watoto zaidi ya 300 wa mikoa ya Dar Es Salaam, Arusha , Mwanza na Mbeya na mpaka sasa  kwa mwaka huu Airtel imegharamia zaidi ya shilingi millini 150 katika kukuza kiwango cha elimu kwa watoto wetu hapa Tanzania," alisema Bayumi.

Bayumi aliongeza kwa kusema kwamba Airtel inapenda kuwatakia kheri na Baraka katika mwezi huu mtukufu na tangu kuanza kwa Mwezi mtukufu wa Ramadhan, wateja wa Airtel wanaweza kufurahia huduma maalumu ya Ramadhani kwa kutuma neno RAMADHANI kwenda namba 15322 kwa shilingi 153 tu kwa siku. Katika huduma hii mteja atapokea dua, nukuu za qurani, mawaidha na taraweh salat moja kwa moja kwenye simu yake, kila siku.

Naye katibu mkuu wa Bakwata Sheikh Suleiman Lolila  ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema mbali ya hafla hiyo makabidhiano ya chakula imetoa fursa kwa waislam kutoka maeneo mbalimbali kukutana pamoja na kukumbushana juu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. 

Aidha Lolila licha ya kuishukuru Airtel Tanzania kwa misaada inayotoa kwa Jamii alisema jambo hilo linahitaji pongezi na kutaka liungwe mkono na kuigwa na kampuni zingine hapa nchini.

CROWN PAINTS YAFUNGUWA TAWI JIPYA MWANZA

Mkurugenzi wa Crown Paints Ramesh Rao akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujio wa kampuni yake nchini Tanzania.
Kampuni ya utengenezaji na uuzaji wa rangi aina ya Crown Paints toka nchini Kenya leo imefunguwa tawi lake jipya mkoani Mwanza ili kupanua soko lake nchini Tanzania na kuleta ustawi wa wananchi wa Afrika Mashariki.

Ujio wa Crown Paints nchini Tanzania umekuja kukidhi mahitaji ya uboreshaji wa kudumu wa muonekano wa majengo ndani na nje hasa ukizingatia miji na majiji mengi nchini yameshuhudia kasi ya ujenzi wa majengo mapya sambamba na nyumba nyingi mpya za kisasa hivyo Crown Paint imekuja wakati muafaka kuuza bidhaa bora zenye kulinda na kuleta uthamani halisi wa majengo hayo.
Afisa Uhusiano wa Crown Paints Bi. Elly Fred akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi katika Ukumbi wa JB Belmont jijini Mwanza.
Kampuni ya Crown Paint ilianzishwa mnamo mwaka 1958 Nairobi nchini Kenya nakuendelea kutanua soko lake kwa nchi mbalimbali Afrika Mashariki na nchi za COMESA.

Ilifungua tawi lake la kwanza nchini Tanzania mkoani Arusha mwezi july mwaka jana (2012) huku ikisambaza bidhaa zake katika mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza.

Hivyo ujio huu utatoa fursa  kwa wakazi wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kupata bidhaa kwa bei nafuu zaidi na kujichagulia aina za rangi wanazotaka kulingana na mahitaji.
Afisa Uhusiano na Masoko wa Crown Paints Bi. Elly Fred akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi katika Ukumbi wa JB Belmont jijini Mwanza.
"Tuna rangi za kupamba nyumba ndani na nje, tuna rangi za magari na vilevile tuna rangi kwaajili ya vyuma, bidhaa nyingi zikitengenezwa toka kiwanda chetu kilichopo nchini Kenya na nyingine tukiziagiza toka Afrika ya Kusini na Uingereza ambapo zinauzwa kupitia jina na nembo yetu nasi tukitumika kuzisambaza sokoni"  alisema Bi Elly.
Bw. Stanley Kipkoech ambaye ni Meneja Masoko wa Crown Paints akizungumza na wandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo. 
"Tuna mpango na tayari tumewaelekeza watafiti wetu kutembelea maeneo mbalimbali ya huduma za kijamii kama Shule, Vituo vya afya na kadhalika ili kubaini changamoto mbalimbali zinazokabili maeneo hayo na ndani ya miezi michache ijayo tutakuwa na kampeni ya kuboresha shule angalau 4 na vituo viwili vya afya vilivyopo ndani ya mkoa wa Mwanza" alisema Bw. Stanley.
Biidhaa za Crown Paints
The goal is to capture at least 50 per cent of the Tanzania paint market. This will partly entail setting up depots and mini plants to serve the rising demand for paint as the Tanzanian government and private sector invest more in infrastructure.

"We will leverage or superior brand quality supported by strong reseach and development to successfully rollout in the Tanzanian market," added Rao.
Wanahabari.

Thursday, July 11, 2013

TANZIA:- HUMPHREY SIMON KATUTOKA

Marehemu Humphrey Simon 
Ni vigumu kuamini lakini hii ndiyo hali halisi wapendwa kuwa Humphrey Simon amefariki dunia mapema leo asubuhi kiasi cha saa moja na nusu hivi mara baada ya kuanguka bafuni. Taarifa zinasema kuwa mara baada ya wana familia yake kuona kakawia kutoka bafuni ilibidi kwenda kugonga mlango, kimya kilipozidi bila majibu ndipo walipoamua kuingia bafuni na kumkuta sakafuni akihema kwa shida sana.

Huku huduma ya kwanza ikitolewa,,, Taarifa za haraka zilifikishwa kwa mjomba wa marehemu ambaye alifika eneo la tukio na kumkimbiza hospitali ya Aga Khan ili kujaribu kuokoa maisha yake na alipofikishwa hospitalini hapo wauguzi waligundua kuwa tayari amekwisha aga dunia ndipo taratibu zikafanywa mwili ukapelekwa Hospitali ya Rufaa Bugando kwa hifadhi.

Merehemu kabla ya kuanzisha miradi yake binafsi ya ujasiliamali alikuwa mfanyakazi wa kitengo cha masoko cha Radio Clouds Mwanza.

Kesho ijumaa 12/07/2013 asubuhi mwili wa marehemu Humphrey Simon utatoka Hospitali ya Rufaa Bugando na kupelekwa nyumbani kwake Nyakato Sokoni ambapo taratibu za kuuaga mwili wa marehemu zitafanyika, mwili utalala hapo kisha jumamosi alfajiri safari itafanyika kuelekea mjini Musoma mkoani Mara kwaajili ya mazishi siku hiyo hiyo ya jumamosi.

Marehemu ameacha mke na mtoto mmoja.


BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

ANGALIA PICHA ZA BEHIND THE SCENE ZA VIDEO MAKING YA UDE UDE (Ngoma Inogile) NDANI YA BILICANAS ( MUCH MORE)

Bata huku video inaendelea

Director Pablo & Video queen

Pablo @ work

Pablo,Nancy & Equ junior

Pablo,queen dalin & Ude ude

Queen dalin akiinuka kwenda kutoa maelekezo kwa Ude ude

Ude ude & video queens on set

Ude ude @ work

Ude ude akiwa na mtoto mzuri

Videos queen

Videos queens on set
Msanii (Star) wa muziki wa kizazi kipya ambaye yupo chini ya BABUU KISAUJI (UDE UDE) Ambaye alikua kimya kidogo sasa kaamua kurudi na zote baada ya kuingia mkataba na BABUU KISAUJI ENTERTAINMENT kwa mujibu wa majibu yakebaada ya mahojiano nae. Hizi ndio picha za behind the scene ya video yake mpya iitwayo NGOMA INAGILE  ambayo Imefanywa na APEX ENTERTAINMENT PRODUCTION chini ya director PABLO ndani ya Bilicanas (Much More) Siku ya tarehe 08-07-2013.

MAISHA NI NYUMBA

Niaje,

Nimegundua hapa Mwanza kuna watu kibao wanapenda house nzuri, lakini hawajui wapi wapate design, wengine wanazifuata mpaka Dar es salaam!

Sasa baada ya kuwaza hilo, nimeona niji introduce ili raia wajue nini nafanya, so wale wapenzi wa blog hii walio interested na mambo ya housing wanicheki.

Contacts zangu:
0757-556935

Wednesday, July 10, 2013

SALVATION YATWAA UBINGWA UMOJA CUP MARA BAADA YA KUILAZA 2-0 KISIMA CHA BURUDANI

Timu ya Salvation Fc ikikabidhiwa Ng'ombe mara baada ya kuibuka washindi wa Kombe la Fainali za Umoja Cup 2013, mara baada ya kuifunga timu ya Kisima cha burudani bao 2-0 kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Goli la pili linafungwa kipindi cha pili katika dakika ya 88 mfungaji akiwa ni Emmanuel Mathew (anayepongezwa jezi namba 8 kwenye bukta)

Kabla ya goli hilo la pili Kisima cha Burudani katika dakika ya 75 ya kipindi cha pili walipata nafasi ya kusawazisha mara baada ya mmoja kati ya mabeki wa Salvation Fc kuunawa mpira kwenye eneo la hatari lakini kwa mshangao wa wengi mpigaji alikosa penati penati hiyo

Umoja Cup ni Mashindano yanayoandaliwa na Umoja wa Vijana CCM kata ya Nyamanoro yameamsha msisimko wa soka kwa vijana hali iliyosababisha mashabiki wa soka waliobahatika kuhudhuria fainali hiyo kuwa na kiu ya mashindano kama hayo tena na tena. 

Patashika za hapa na pale...

Ni mara baada ya mwamuzi wa mchezo huo kupuliza kipyenga cha mwisho kuashiria mpira finito.

Mashabiki vijana na mwamko wao.

Shangwe za vijana wa Salvation mara baada ya kuibanjua 2-0 Timu ya Kisima cha Burudani.....

Doto Joseph ambaye ni kocha mchezaji wa timu ya Kisima cha Burudani akipokea zawadi za mshindi wa pili wa Umoja Cup ambazo ni Jezi seti moja, mpira na kisha baadaye alikabidhiwa mbuzi mnyama.

Kapteni wa timu mabingwa wa Umoja Cup Salvation Fc akipokea zawadi ya jezi seti moja, mpira, kombe na walikabidhiwa ng'ombe mnyama. 


Kombe kwa mabingwa Salvation Fc.

Timu iliyokamata nafasi ya Tatu ni Afa Academy ambapo kwa upande wao waliondoka na zawadi ya mbuzi mnyama.