ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 15, 2013

MH. MAKAMBA NA MH. KABWE WAHUDHURIA SHOW YA KIJANJA YA MWANA FA 'THE FINEST' NDANI YA UKUMBI WA MAKUMBUSHO YA TAIFA.

IMG_7288
Mwana FA akiwasili katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam huku akiwa amevalia suti matata iliyotengenezwa na mbunifu wa mavazi anayekuja kwa kasi nchini Sheria Ngowi.(Picha zote na Geofrey Mwakibete wa Mo Blog).
IMG_7336
IMG_7422
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA akikamua jukwaani wakati wa Show ya Kijanja ya The Finest iliyorindima usiku wa kuamkia leo ndani ya ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar. Nyuma yake ni Msanii Linah aliyeshirikishwa kwenye nyimbo ya YALAITI aliyoimba na Mwana FA akisubiri kutumbuiza.
IMG_7361
Msanii wa muziki wa Bongo Flava nchini Ben Paul akisindikiza kutoa burudani wakati wa show ya Mwana FA iliyopewa jina la “The Finest”. Wasanii wote walionekana nadhifu kwa kuvaa masuti ya gharama.
IMG_7357
Kutoka (kulia) ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe, akiwa na Mbunge wa Bumbuli (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba, wakiwa ni miongoni mwa mashabiki wa Mwana FA, waliohudhulia shoo hiyo. Kushoto ni Mtangazaji wa Clouds FM, Gerald Hando.
IMG_7427
Mashabiki wa Mwana FA, wakimshangilia Superstar wao wakati akitoa burudani.
IMG_7430
Mrembo wa Wema Sepetu na Kidate wake nao walikuwepo kwenye show ya wajanja.
Fa 7
Mashabi wa Mwana FA wakionekana kukongwa mioyo yao wakati wa show iliyobeba jina la  “THE FINEST”…Na kweli ilikuwa The Finest kama inavyoonekana pichani.
IMG_7330
Watu weweeeeeeeeeee…..ukumbi ulirindima Shangwe za mashabiki wa Mwana FA.
IMG_7418
Mwana FA akiendelea kuwapa raha mashabiki wake.

Asma Makau, Jojo, Shadee & Afriend wakiwa nje ya ukumbi wa makumbusho ya Taifa Dar es salaam kwaajili ya kuingia ndani kushuhudia 'The Finest'. 


Vanessa Mdee na B Dozen katika viwanja vya Makumbusho kabla ya 'The Finest' Show 

IMG_7399

Wadau wakishow love nje ya Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Halima Kambi, Dar.
KATIKA Shoo hiyo ya ‘Kijanja’ pia ilihudhuriwa na wasomi kibao huku baadhi ya wabunge kama Mh. Zitto Kabwe na January Makamba wakiwa ni miongoni mwa mashabiki wajanja waliohudhuria katika shoo hiyo ya “kijanja” ya ‘The Finest’ iliyofanyika  katika Ukumbi Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.

Mwana FA, pia alisindikizwa na na baadhi ya wasanii kama, Ben Paul, Linah, Maua, Dully Sykes na wengine kibao pamoja na bendi ya Njenje.

Show ilifana sana kutokana na utaratibu na mpangilio na maandalizi ya shoo yenyewe na MwanaFA aliweza kufanya yake jukwaani na kuwapagawisha mashabiki wake katika usiku ule.

SERENGETI BREWERIES YAWAPONGEZA WASHINDI WA FAINALI ZA GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE

 Wakuu usiku huu, Serengeti Breweries Ltd imefanya hafla ya kuwapongeza washiriki wa Guinness Football Challenge, pamoja na kuwapongeza washindi wawili waliofika hadi fainali za mashindano hayo ya kukuza vipaji vya mpira. 

Zifuatazo ni picha mbalimbali kuonesha hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam katika Hotel JB Belmont na kuhudhuriwa Viongozi waandamizi wa SBL, akiwemo Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Epraimu Mafuru na wageni mbalimbali waalikwa pamoja na wanahabari. 
Mmoja wa washindi pekee waliofika fainali Guinness Football Challenge kutoka Tanzania akionesha manjonjo



Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Epraimu Mafuru akiwa na washindi pekee waliofika hadi fainali kutoka Tanzania



PPF YAKUTANA NA WAAJIRI WA MIGODI KANDA YA ZIWA KUTOA ELIMU JUU YA MIFUKO YA JAMII

Meneja wa PPF kanda ya ziwa Meshark Bandawe akizungumza na waajili wa makampuni mbalimbali ya migodi kanda ya ziwa kuhusu shughuli mbalimbali za uendeshaji wa mfuko huo wa jamii na sheria zake.

Waajili mbalimbali kutoka makampuni ya Geita Mine, North Mara, African Barrick Tanzania, Tulawaka, Caspian Tanzania Limited, Majour Drill na Twigg Gold Mine, wamehudhuria semina jii kwa mwitikio wa asilimia 100. 

Waajili wa migodini pamoja na waandishi wa habari wakinakili point zilizokuwa zikiwasilishwa na meneja wa kanda.

Waajili ndiyo nguzo kubwa ya kuwasilisha ujumbe hivyo PPF imeona ni vyema kukutana nao hapa na kutoa seminakuwaelimisha manufaa ya kushiriki katika kuwawekea akiba ya baadaye wafanyakazi wao.

Waajili hawa watakuwa mabalozi wa PPF kuhakikisha ujumbe wa mifuko ya jamii na taratibu zake unafika kwa wafanyakazi wote waajiliwa ambao ni wanachama.

Ni safu ya wafanyakazi wa PPF tawi la Mwanza walio na dhamana ya utoaji elimu, Kutoka kushoto ni Happyness Manyenye, Zaida Mahava, Jackson Mashiku, Grace Balele, Stela Mashiku na Zaida Mahava, wakiwa wamejipanga wakisikiliza kilichokuwa kinajiri.

PPF imekuwa na utaratibu wa kukutana na waajiri kuhakikisha kwamba pamoja  na kuwa na kazi za msingi za kuandikisha wanachama kutoka sehemu zote za ajira, kukusanya michango yao, kuwekeza pamoja na kulipa mafao lakini pia kuhakikisha inatimiza wajibu wake wa kutoa elimu kwa wanachama wake kufahamu kwa undani wanachokichangia na nini wanategemea kupata kutoka kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii.

Kumekuwa na changamoto kubwa kwa baadhi ya waajili nchini kuzembea kuwasilisha michango kwa wakati.

Katika semina hii moja kati ya mada zilizojadiliwa ni pamoja na taratibu za kisheria na adhabu zipi zitachukuliwa kwa ajili ambao hawatatekeleza majukumu yaokwa mujibu wa sheria.

Jumla ya mafao 7 yanatolewa na PPF ikiwa ni pamoja na Mafao ya uzeeni, Kinua mgongo, Mafao ya ulemavu na ugonjwa, Mafao ya kifo, Mafao ya wategemezi na Mafao ya elimu ambapo PPF kwa sasa inasomesha zaidi ya watoto 1000 nchi nzima ambao walezi wao ambao walikuwa wanachama wa PPF walitangulia mbele za haki hivyo imebeba jukumu la kuwasomesha kwa mujibu wa fao la wanachama waliofariki mpaka wafike kidato cha nne.

Friday, June 14, 2013

KILA MMOJA ANAWEZA KUONEKANA KINARA KWA KUJITOKEZA NA KUCHANGIA DAMU ILI KUWEZA KUOKOA VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO PAMOJA NA WATOTO WACHANGA NA WALE WENYE UHITAJI WA DAMU




Na Shommi B.
KILA tarehe 14 juni Dunia inaazimisha siku ya wachangia damu duniani(World Blood Donor Day) ikiwa na lengo la kuwashukuru na kuwatambua wale wote ambao kwa kuelewa umuhimu wa damu salama huwa wanajitolea kuchangia damu kwa hiari.

Jamii inahimizwa kuchangia damu ili kuokoa vifo hususani vya mama wajawazito na watoto wachanga vinavyotokea wakati wa kujifungua huku tatizo kubwa la vifo hivyo ikitajwa kuwa ni damu.

Takwimu zinaonyesha kina mama 48,000 na watoto 8,000 ufariki dunia kutokana na upungufu wa damu hapa Tanzania,kiwango ambacho ni kikubwa kuliko nchi yoyote duniani kwa mujibu wa wataalamu wa afya.
Kiasi cha chupa 450,000 za damu zinahitajika kwa mwaka Nchini Tanzania huku kiasi kikubwa kikitumika kuokoa maisha ya mama na watoto lakini cha kusikitisha chupa 150,000 za damu ndizo zinazopatikana na kusambazwa.

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha jumla ya damu zinazotolewa kila mwaka ulimwenguni kwa utaratibu wa kujitolea ni chupa milioni 80.

Katika idadi hiyo niliyoitaja nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania hutoa asilimia 38 tu idadi ambayo haiendani na asilimia 82 ya wagonjwa ambao tiba yao ina uhitaji wa damu.

Imebainishwa wagonjwa wenye uhitaji wa damu kwa wingi ni watoto chini ya miaka mitano,wanawake wajawazito,watu wanaopata ajali pamoja na wale wenye magonjwa mbalimbali yanayosababisha upungufu wa damu.

Tunaweza kuokoa vifo vinavyotokana na upungufu wa damu kwa kujitoa kuchangia damu kwani kitendo cha kuchangia damu ni kitendo cha kibinadamu kwani kinaokoa maisha ya binadamu.


Kila siku nchini Tanzania, wanawake 23 wanapoteza maisha kutokana na matazizo ya uzazi na watoto wachanga 131 hufariki dunia.

Damu salama maana yake ni ile damu ambayo haina vimelea vya maradhi ambayo yanaweza kuambukiza mtu mwingine iwapo mtu huyo ataongezewa.

Maradhi ambayo yametajwa na kuweza kuambukiza kupitia kwenye damu ni Ukimwi (HIV),Homa ya Ini (Hepatitis) pamoja na Kaswende (Syphilis) ambayo yanachunguzwa na vituo vya damu salama vilivyopo kila kanda.

Majukumu makuu ya vituo vya damu salama vinatakiwa kuhakikisha malengo ya upatikanaji wa damu salama yanafikiwa ikiwa ni pamoja na kutoa uhamasishaji kwa jamii ili kuweza kuchangia.

Lakini licha ya kuhamasisha jamii kujitoa kuchangia damu kitu muhimu kinachopaswa kufanywa na vituo vya damu salama ni kuhakikisha damu inapimwa kwa usahihi na kwa utaalamu wa hali ya juu ili kuhakikisha usalama wake.

Nikirejea katika suala la kuchangia watu wengi hawatambui umuhimu wa kujitolea kuchangia damu katika kuokoa maisha ya binadamu ili hatimaye kila mtu mwenye afya nzuri awe mchangiaji damu wa mara kwa mara.
Katika uzinduzi wa kampeni ya kuchangia damu mkoani Mara iliyofanyika Wilayani Bunda,mkurugenzi wa Shirika la (Evidence For Action) Craig Ferla linaloshughulika na kampeni ya uchangiaji wa damu Tanzania alisema vifo vya akina mama na watoto wachanga wakati wa kujifungua ni vingi hapa Nchini kuliko sehemu nyingine Duniani hivyo wanaweza kuokolewa kwa kuchangia damu.

Kila mmoja wetu anaweza kuchukua hatua katika kuokoa vifo vya mama zetu pamoja na woto wachanga wakati wa ujauzito na kujifungua ikiwa wewe ni mwanafamilia,jirani,mwanajamii,mwanamtaa,kiongozi wa dini au mtu yoyote yule unaweza kuleta mabadiliko katika kuokoa maisha ya mama na mtoto wake mchanga.

Hali hii ya akina mama na watoto wetu wachanga inatisha na kuna kila sababu ya kuchukua hatua kuweza kuokoa vifo vinavyotokana na ukosefu wa damu.

Kama tunataka akina mama na na watoto wetu wachanga wapite salama katika kipindi cha ujauzito na kujifungua ni lazima kwa pamoja tuhakikishe vituo vya tiba vinatoa huduma stahiki kwa mama zetu na pia wanawake wanaojifungulia katika vituo vya tiba vyenye wahudumu wenye ujuzi.

Inaelezwa kiwango kikubwa cha uhaba wa damu kinachangia kwa kiasi kikubwa kinapelekea akina wengi kufa wakati wa kujifunguana hata kupelekea vifo vya watoto wachanga kutokana na tatizo hilo.

Ni kuhimizana wanajamii kuchangia kutoa damu kadri inavyowezekana kutokana na ukubwa wa tatizo ambalo tayari limekwisha kuelezwa ni kubwa nchini Tanzania kuliko nchi yoyote duniani.

Kutokana na tatizo kubwa la damu,Serikali ya Tanzania kupitia Rais Jakaya Kikwete Septemba  mwaka 2008 alitoa hotuba inayohimiza suala la afya ikiwemo kutanzama afya ya mama pamoja na watoto wachanga katika kuokoa maisha yao hapa namnukuu.

"Ni lazima tuongeze kwa kiasi kikubwa mgawo wa rasilimali fedha katika afya ya mama na watoto wachanga. Ili kutimiza malengo tuliyojiwekea, inabidi tuongeze fedha katika afya ya mama na watoto wachanga kwa kiasi cha dola za kimarekani bilioni tano kila mwaka ifikapo mwaka 2010, na ongezeko la dola bilioni nane kila mwaka kufikia mwaka 2015.

Pia ni muhimu katika kuwekeza katika kuongeza idadi ya wahudumu wenye ujuzi--wauguzi, wakunga, wataalamu wa maabara na madaktari. Tunahitaji ziada ya wahudumu wenye ujuzi milioni moja kufikia mwaka 2010 ili kuhakikisha uwepo wa huduma za kuokoa maisha ya akina mama katika kipindi chote cha ujauzito na wakati wa kujifungua."

Septemba mwaka 2010, katika mkutano wa malengo ya milenia mjini New York, Tanzania ilikuwa mojawapo ya serikali zilizotoa ahadi ya “kuokoa maisha ya wanawake na watoto milioni sitini kufikia mwaka 2015.

Jitihada hizi za Serikali hazipaswi kuachiwa pekee yake bali kila mwana jamii kwa nafasi yake anaoumuhimu mkubwa wa kuona umuhimu wa kuchangia damu na kuokoa vofo vya mama wajawazito pamoja na watoto wetu wachanga wanaozaliwa na kufa kila siku kutokana na tatizo la damu.

AIRTEL YAWAOMBA WATANZANIA KUWAOKOA WAWAKILISHI WA TZ BBA


·        Wateja wa Airtel Lipieni DSTV kwa Airtel Money mambo mazuri yaja

Watanzani wametakiwa kuwapigia kura nyingi kadri wawezavyo, wawakilishi wao katika shindano la Big Brother Africa ‘The Chase’ linaloendelea nchini Afrika Kusini ili kuhakikisha wanaendelea kubaki ‘mjengoni’ wakipeperusha bendera ya taifa.

Wito huo, umetolewa na Meneja Uhusiano wa Kampuni ya simu ya Airtel Tanzania, nayodhamini shindano hilo,Jackson Mmbando, huku akiwataja wawakilishi hao wa Tanzania kuwa ni Feza Kessy  na Ammy Nando. 

Mmbandoalisema kuwa, ili kuendelea kumbakisha Feza katika kinyang’anyiro cha BBA ‘The Chase,’ Watanzania wanapaswa kutuma ujumbe wenye jina ‘FEZA’ kwenda namba 15456, ili kumuokoa mshiriki huyo aliyeingia mara mbili kikaangoni, tofauti na Nando(22), ambaye anafanya vizuri.

“Watanzania tuna kila sababu za kuwapigia kura wawakilishi wetu, ili waweze kuwakilisha vema na kipaumbele zaidi kiwe kwa kumpigia Feza kwa kuandika jina lake kwa herufi kubwa “FEZA” kisha kwenda kwa namba 15456,” alisema Mmbando.

Mshindi wa mwaka huu, atajinyakulia kitita cha Dola za 300,000 za Marekani.Tangu shindano hilo lianze ni Mtanzania Richard, ndiye pekee aliyewahi kushinda shindano hilo.

Mashindanohayo yanayofanyika kwa mara ya nane, yanashirikisha washiriki 24 kutoka nchi 14za Afrika na watakaa ndani ya nyumba hiyo kwa siku 90, ambako kusalia kwao mjengoni kunategemea kura za watazamaji wa shindano hilo.

Katikahatua nyingine, Mmbando aliwataka Watanzania kuendelea kulipia huduma zao zaDSTV kupitia Airtel money, kwani kuna kuna kitu cha ziada kinakuja kwa ajili yao.

“Airtel ili kuleta burudani zaidi kwa wale wanaolipia huduma na vifurushi vya kila mwezi vya DSTV kupitia huduma ya Airtel Money kuna mambo mazuri yenye kuvutia yanakuja yatakayowafanya waendeleee kutosheka zaidi kupitia huduma zetu zote” alimaliza kwa kusema bw, Mmbando.

REDD'S MISS KINONDONI 2013 KUFANYIKA KATIKA HOTELI YA GOLDEN TULIP JIJINI DAR

Mratibu wa shindano la Redd's Miss Kinondoni 2013, Deniss Ssebo akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na shindano hilo, alisema kuwa mwaka huu imeleta mapinduzi Makubwa katika sekta ya Afya, Elimu pamoja na Ajira.
Ambapo mshindi wa kwanza atapata udhamini wa masomo (Scholarship) kwa muda wa mika miwili katika kuendeleza masomo yake na kama amemaliza kusoma basi atapa ajira kwenye hoteli ya kimataifa ya JB Belmonte kulingana na elimu aliyonayo. Pia atapata shopping vocha kutoka Oriflame ya tshs. 300,000 pamoja na fedha taslimu tshs. 500,000.
Mshindi wa pili;  atapata udhamini wa masomo (Scholarship) ya mwaka mmoja, fedha taslimu 300,000 na shopping vocha kutoka Oriflame ya tshs. 200,000.
Mshindi wa tatu;  atapata udhamini wa masomo (Scholarship) ya mwaka mmoja, fedha taslimu 200,000 na shopping vocha kutoka Oriflame ya tshs. 100,000.
Mshindi wa 4 na tano; watapata uthamini wa masomo ya kompyuta ya miezi sita. Mshindi wa nne atapata pia pesa taslimu laki mbili  na nusu na wa 5 laki moja na nusu.Washiriki wengine wote watapata kifuta jasho cha shilingi laki mbili kwa kila mmoja.
Mashindano ya Redd's Miss Kinondoni 2013 yanatarajia kufanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip siku ya Ijumaa 21 June 2013. Viingilio katika onyesho hilo ni shs. 60,000 VIP, shs. 25,000 kwa tiketi za kawaida na meza ya watu ukitazama zawadi.
Mashindano ya Redd's Miss Kinondoni yanatarajiwa kufanyika June 21, huku walowa yamedhaminiwa na Redd's Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, Mrokim Blog, SufianMafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog, DjChoka Blog na Kajunason Blog.
 Muonekano wa warembo wa Redd's Miss Kinondoni 2013
 Kila mmoja akiwa na furaha na bashasha.
 Baada ya mkutano na waandishi wa habari warembo walipata nafasi ya kutembelea ofisi za wadhamini wao ambao ni Oriflame Natural Beauty Products zilizopo jengo la Mkapa jijini Dar es Salaam, na hapo waliweza kupata semina ya kuelezewa jinsi vipodozi vyao vinavyofanya kazi kama pichani unavyoona mwezeshaji akitoa somo kwa warembo.
 Mmoja ya warembo wa Redd's Miss Kinondoni 2013 akiuliza swali kwa mwezeshaji.
Kila mrembo akijaribu kuweka kumbu kumbu kwa yale waliyokuwa wakifundishwa.