ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 6, 2013

BOTSWANA YAAHIDI KUFANYA KAZI NA IBF/AFRICA


Rais Ngowi akihutubia katika mkutano na waandishi wa  habari katika ukumbi wa BNSC
Serikali ya Botswana imeahidi kushirikiana na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) katika program yake ya “Utalii wa Michezo” na kuifanya nchi hiyo kuwa moja ya mataifa yanayong’ara kwenye medani ya masumbwi katika bara la Afrika. Ahadi hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Michezo la Botswana bwana Persy Raditladi alipofanya mazungumzo na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi katika ofisi za BNSC leo.
Rais Ngowi akiwa amesimama na Mkurugenzi
Mtendaji wa BNSC bwana Persy 
 Raditladi

Rais Ngowi yuko nchini Botswana kuutangaza mkanda wa ubingwa wa ngumi wa kimataifa ambao utashindaniwa tarehe 5 July nchini Namibia kati ya  bondia  wa Botswana Lesley Sekotswe na bondia kutoka Namibia Immanuel Naidjala. Wawili hao walitoka sare katika mpambano wa kukata na shoka wa kugombania mkanda huo tarehe 20 Machi mwaka huu katika jiji la Windhoek, nchini Namibia.

Serikali ya Botswana imeahidi kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa programu ya “Utalii wa Micheazo ya IBF” inanufaisha nchi hii yenye vivutio kadhaa vya kitalii likiwamo bonde la maarufu la “Okavango Delta”

Katika mazungumzo yao Rais Ngowi alieleza jinsi IBF inavyozinufaisha nchi ambazo zimeingia katika programu hii na namna mabondia wanaotoka katika nchi hizi wanavyonufaika na viwango vya kimataifa vya IBF. Ngowi aliielezea Botswana kama nchi yenye neema ya vipaji vya mabondia wazuri wa ridhaa na kuwashauri kuwa waweke mikakati ya mabondia wa ridhaa wanavyoweza kujiunga na ngumni za kulipwa ili waweze kufaika na vipaji vyao.

Nchi ya Botswana ni moja kati ya nchi zenye mabondia wazuri katika ngumi za ridhaa lakini kumekuweko na pengo la kuwaendeleza wanapofikia kustaafu na kutokuwa na uwazi wa namna ya kujiunga na ngumi za kulipwa. Ujio wa Rais wa IBF Afrika nchini Botswana umefanyika wakati nchi hii inapokabiliwa na sintofahamu juu ya kuwaendeleza mabondia wake wanapostaafu ngumi za ridhaa.

Mazungumzo ya Rais Ngowi na serikali ya Botswana yalitanguliwa na mkutano wa waandishi wa habari pamoja na wadau kadhaa wa ngumi za kulipwa uliofanyika katika ukumbi wa BNSC jijini Gaborone Botswana leo. Katika mkutano huo Rasi Ngowi aliuonyesha mkanda wa IBF wa kimataifa katika uzito wa bantam utakaoshindaniwa kati ya bondia wa Botswana Lesley Sekotswe na bondia kutoka Namibia Immanuel Naidjala tarehe 5 July mwaka huu jijini Windhoek, Namibia.

Rais Ngowi aliwahakikishia wadau wa ngumi wa Botswana kuwa IBF itafanya kila liwezalo kuhakikisha kuwa Botswana imejenga msingi mzuri wa ngumi za kulipwa na kutumia vipaji vilivyonavyo katika ngumi za ridhaa. Rais Ngowi aliondoka leo kwenda nchini Afrika ya Kusini ambako atakutana na wadau wa ngumi na kutangaza mapambano kadhaa ya IBF yanayotarajiwa kufanyika nchini humo kuanzia mwezi ujao! 

JOHN MNYIKA AONGOZA MAAFALI YA KWANZA CHUO CHA MAFUNZO YA JINSIA (GTI)

Zifuatazo ni picha mbalimbali za matukio ya sherehe za mahafali ya Kwanza ya Chuo cha Jinsia (GTI), zilizofanyika jana mchana katika viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Mabibo, jijini Dar es Salaam. 
Mmoja wa wahitimu akitunukiwa cheti cha mafunzo ya GTI na mgeni rasmi wa maafali ya kwanza ya Chuo cha mafunzo ya jinsia, na Mhe. Mbunge John Mnyika

Mwenyekiti wa Bodi ya GTI,Marry Rusimbi (aliyesimama) akihutubia

Baadhi ya wahadhiri wa chuo cha mafunzo ya Jinsia GTI wakiwa kwenye mahafali

Baadhi ya wafanyakazi wa TGNP wakiwa katika mahafali

Mgeni rasmi, John Mnyika akizungumza na kusanyiko hususani wahitimu.

Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia, Dk. Diana Mwiru (kulia) akihutubia katika hafla hiyo

Bendi ya Jeshi la Polisi Tanzania ikiwajibika katika mahafali hayo

Bendi ya Polisi ikiwajibika

Maandamano ya mahafali

Maandamano mgeni rasmi na viongozi wa GTI na TGNP

Maandamano ya mgeni rasmi na viongozi wa GTI na TGNP.
Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) jana kimetoa wahitimu wa kwanza wa mafunzo ya jinsia katika ngazi ya cheti. Mgeni rasmi katika mahafali hayo ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia tiketi ya CHADEMA, John Mnyika. 

Picha zote zimeandaliwa na mtandao wa www.thehabari.com.

LIGI DARAJA LA 3 NGAZI YA MKOA WA MWANZA LIVER SIDE WAONA MWEZI

Ratiba ya ligi soka daraja la tatu ngazi ya mkoa wa Mwanza inayoendelea kwenye uwanja wa Nyamagana.
Ndani ya uwanja wa Nyamagana jijini mwanza katika ligi soka daraja la 3 ngazi ya mkoa inayoendelea, mchezo baina ya Lake Worious na Liver side uliochezwa tarehe 4/04/2013, ulimalizika kwa River Side kuibuka kidedea kwa mara ya kwanza kwenye ligi hiyo kwa kuifunga Lake Worious ya Ukerewe bao 1-0, mfungaji akiwa ni Frank Kulwa kwenye ungwe ya lalasalama.
Mmoja kati ya washambuliaji wa Liver side akiukokotoa mpira toka pembe moja ya uwanja wa Nyamagana katika mchuano wa soka ligi daraja la tatungazi ya mkoa.
Kwa matokeo hayo kwa mara ya kwanza Liver side imeambulia pointi na kuwa na pointi 3, huku timu ya Lake Worious ikibakia na pointi zake 7 ilizozivuna hadi sasa.
Msahambuliaji wa Liver side Frank Kulwa akiinyanyasa ngome ya Lake Worious.

"Ngoma katikati ya miguu huku kila timuikijitahidi kwa ufundi kuona ni jinsi gani inapata ushindi"

"Ni hatari langoni mwa Lake Worious lakini anajitokeza pale beki wa timu hiyo na kuiondosha hatari..."

Friday, April 5, 2013

HAPA NA PALE NA MJI WA KATORO GEITA

Mji wa Katoro bado uko kwenye mchakato wa kusambaza nguzo hatimaye umeme upatikane hivyo katika kipindi hiki umeme unaotumika ni wa jenereta na sola hivyo kuna wasambazaji binafsi wanaotoa huduma ya umeme kama unavyoona pichani juu nguzo zikipita toka upande mmoja wa barabara hadi upande mwingine.

Kwenye msafara wa mamba kenge nao wamo.

Uwekezaji katika sekta ya biashara.

Mnyamwezi Cafe.

Chadema ikiendelea kujiimarisha vijijini.

Chama banika....katikati ya muji.

Kama umevutiwa na unataka kuwekeza Katoro mkoani Geita, basi wasiliana na dalali huyo ili uwe na makazi.

Thursday, April 4, 2013

WASANII WA FILAMU MWANZA WATEMBELEA SHULE YA WATOTO WENYE ULEMAVU YA MITINDO

Wasanii wa uigizaji filamu pamoja na uchekeshaji mkoani Mwanza, Mwishoni mwa wiki katika kusherehekea sikukuu ya Pasaka waliamua kufunga safari kwenda katika shule ya watoto wenye ulemavu ya Mitindo iliyoko wilayani Misungwi mkoani Mwanza na kutoa zawadi mblimbali walizokuwa nazo kupitia changizo walilofanya wao kwa wao.

Mwenyekiti wa Umoja wa wasanii wa Filamu Mwanza ujulikanao kama Meet Club akikabidhi kwa mkuu wa kituo kiasi walichochangishana.


Wasanii hao waliimba nao pamoja nyimbo mbalimbali na kila mmoja alishiriki kuwa karibu nao kama mzazi.

Umoja wa wasanii hawa uliiteua siku hiyo muhimu ya Pasaka kudhuru kituo hicho kwa nia ya kuwatembelea watoto hao na kujionea changamoto wanazokutana nazo, kuwafariji kwa kucheza nao na  kufurahi nao hasa ukizingatia ni siku ya sikukuu, 

Hakika watoto walijisikia vyema kutembelewa huku nao wasanii wakijifunza mengi kutoka kwa watoto hawa wanaohitaji roho ya wengi wenye huruma.

Msanii ajulikanaye kwa jina la 'Chenga Mbili' akiwa na watoto wake wa pasaka.

"Hawa ndiyo wanangu na ndiyo rafiki zangu" alisema dada huyu.

Nao watoto walijihisi kupendwa kwa ukaribu ulioonyeshwa na wasanii waigizaji wa jijini Mwanza.

Furaha tele kwani si kukaa nao tu bali watoto hao walishuhudia vimbwanga vya uigizaji.

"Tuwapende watoto hawa kwani wanastahili kupendwa" Ndivyo isemavyo picha hii.

Japo moja ya wawakilishi wasanii na watoto.

Kisha baadaye kabisa msafara wa wasanii hao wa uigizaji filamu na uchekeshaji ulirejea jijini Mwanza huku kila msanii akiwa na wazo lake kichwani kuhusu watoto hao wa Shule ya Mitindo wilayani Misungwi.

TOTO ILIPOICHARAZA PRISONS BAKORA 1-0



Toto Africans ya jijini Mwanza jana imetoka katika dimba lake la nyumbani ikiwa kifua mbele mara baada ya kuifunga Tanzania Prisons bao 1-0. Matokeo zaidi sikiliza taarifa ifuatayo iliyoruka ndani ya Sports Xtra Clouds Fm...Bofya play

Mtanange ulikuwa wa vuta nikuvute Toto wakiongoza kwa kuwa na kosakosa nyingi mikwaju mingi ya wachezaji  wake ikigonga mwamba wa goli la Prison kilawakati walipothubutu kulikaribia.


Mabadiliko kwa Tanzania Prisons.


Mashambulizi.

Wednesday, April 3, 2013

ILIVYOKUWA PASAKA GOSPEL FESTIVAL2013 MJINI KATORO GEITA.

Mwimbaji muziki wa Injili Neema Mwaipopo akihudumia kwa njia ya uimbaji kwenye viwanja vya CCM Katoro mkoani Geita.

Hapa ni katikati ya kusanyiko na mkali wa muziki wa injili Neema Mwaipopo.


Ni muimbaji mpya kabisa katika muziki wa injili si mwingine Jackline ambaye pia ni mtangazaji wa Kwaneema Fm Mwanza akitambulisha wimbo wake mpya kwa wakazi wa Katoro Geita kwenye kusanyiko la Pasaka Gospel Festival 2013 lililofanyika jumatatu ya tarehe 1 april 2013.


Kama kawaida yake mwimbaji Nesta Sanga ameendeleza wimbi lake la kufanya vyema kwenye kila kusanyiko alilohusika nalo kanda ya ziwa.


Uwanja huu hauna majukwaa hivyo wananchi hukusanyika popote wanapoweza yote kwa yote huu ni moja kati ya utalii.


Ni mwimbaji mpya kabisa kwa masikio ya wengi mijini lakini ndani ya himaya ya Geita yu msanii mkubwa na ana nyimbo nzuri za kusikilizwa na hata kuchezeka.


Macho mbele kwenye mashughuli.


Ni raha ni kucheza kwa furaha.
Kwaya ya Katoro Geita.


Lango kuu la uwanja wa CCM Katoro kama ni tiketi hiyo hiace hapo pembezoni...


Ni producer wa COSU Studio ambaye vilevile yu mkali katika mavideo..


Alikuwa paleeeee.....!!!


Picha toka kwenye kamera ya producer wa COSU.



Ilifika kipindi waimbaji wakawa katikati  ya umati  nayo shughuli ikaendelea kama ilivyopangwa.
Watangazaji wa Radio Kwaneema Fm Mwanza kutoka kushoto ni Jackline na Florida.