ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 26, 2013

MPIGA BASS WA MSONDO AFARIKI


Mpiga bass wa bendi kongwe nchini Msondo Ngoma 'Baba y a Muziki' , Ismail Mapanga  amefariki dunia  siku ya jumatano ya wiki hii katika hospitali ya Temeke.

Kwa mujibu wa kipindi cha Saturday Bonanza cha Clouds fm watangazaji wakiwa ni Suzzy Bartazar na Ben Kinyaiya taarifa zinasema kuwa Mapanga alianza kuumwa wakati bendi ikiwa safarini katika safari yao mkoani Tabora iliyofanyika hivi karibuni, taratibu za mazishi tayari zimekwisha fanyika.
Bofya play Sikiliza 
 

Mwenyezi Mungu ilaze mahali pema peponi roho ya marehemu, Amina. 

TAMKO LA WACHUNGAJI KUHUSU WAKRISTU KUCHINJA LAOTA MBAWA MWANZA.

Baadhi ya Maaskofu na wachungaji wa madhehebu ya kikristo mkoani Mwanza leo wameshindwa kutoa tamko juu ya maamuzi ya waziri wa nchi Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu Steven Wassira aliyoyasema juu ya habari ya uchinjaji wanyama, jambo ambalo lilianza baada ya mchungaji kukamatwa akishitakiwa kutokana na malalamiko ya baadhi ya waumini wakislamu kuwa amewalisha kibudu baada ya mchungaji huyo kuchinja mnyama kwenye msiba wa muumini wake huko katika kijiji cha Nyehunge wilayani Sengerema... Pichani ni mmoja wa wachungaji kutoka Nyehunge akihadithia katika kanisa la Anglikana Mwanza lililopo barabara ya posta ya zamani kuelekea Kamanga Ferry na Capripoint..  
Baadhi ya waumini waliojitokeza leo kwenye kanisa la Anglikana jijini Mwanza kusikiliza tamko la baadhi ya maaskofu na wachungaji wa madhehebu ya kikristo wakifuatilia kwa makini maneno yaliyokuwa yakisemwa na mmoja wa wachungaji.
Mchungaji akihubiri kwa kutumia vifungu kadhaa vya Biblia kwenye kusanyiko hilo la Tamko lililofanyika katika kanisa la Anglikana Mwanza, hata hivyo wachungaji hao na maaskofu walishindwa kutimiza adhma ya kutoa tamko juu ya maamuzi ya waziri wa nchi Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu Steven Wassira aliyoyasema juu ya habari ya uchinjaji wanyama.


Viongozi hao wa madhehebu ya makanisa ya Kikristo juzi walipinga maamuzi ya waziri Wassira aliyetinga jijini Mwanza kusuluhisha mgogoro huo, ya Kwamba mwenye haki ya kuchinja ni mwislam kwa nyama ya biashara, kwenye kikao chao leo walichoketi wameshindwa kutoa tamko lao wakipata kigugumizi huku baadhi ya waumini waliofurika kanisani hapo wakipaza sauti zao wakiwatuhumu kuwa wawakilishi wao hao wamehongwa kusitisha utoaji wa tamko hilo.
Baadhi ya wachungaji na maaskofu wakifuatilia yanayojiri ndani ya kanisa.


Baadhi ya wachungaji na maaskofu wakifuatilia yanayojiri ndani ya kanisa, kwa mujibu wa mmoja wa wasemaji wao alitanabaisha kuwa wameahirisha kutoa tamko lao mpaka siku ya jumatatu. 

"BILA UMOJA VYAMA VYA UPINZANI HAVITAINGIA IKULU KUSHIKA DOLA" ASEMA JUMA DUNI HAJI: CUF KUFANYA MKUTANO KESHO JIJINI MWANZA.

Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Taifa ambaye pia ni Waziri wa Afya  wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar Juma Duni Haji akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza hii leo asubuhi.
 CHAMA cha Wananchi CUF kesho kitafanya Mkutano wake wa hadhara ikiwemo kuwakumbuka wahanga waliofarikidunia kwenye vurugu zilizotokea Zanzibar na jijini Dar es salaam mnamo mwaka 2001 wakitetea haki.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za CUF wilaya ya Nyamagana Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Taifa ambaye pia ni Waziri wa Afya  wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar Juma Duni Haji alisema kwamba vyama vya siasa vilivyopo nchini havina budi kushirikiana ili kuiondoa CCM madarakani.

"Bila kushirikiana hivi vyama vya upinzani na ikiwa kila kimoja ni kutaka kuingia ikulu kivyake basi itakuwa ni ndoto ya kukiondoa madarakani chama tawala (CCM) ambacho kinashikilia dola" alisema mjumbe huyo. Bofya Play msikilize...

Haji 'Babu' alisema kwamba Chama kinachohamasisha na kuchochea vurugu kitambue kuwa siyo  njia ya kukiwezesha chama hicho cha siasa (Upinzani) kuingia ikulu pia hakitaungwa mkono na wananchi kwani kwa kufanya hivyo wananchi hawatapata ujumbe na sera nzuri wanazopaswa kuzisikiliza kwenya mikutano ya hadahra ili kufanya uamuzi sahihi wa nani wachaguliwe kuwaongoza kupitia chaguzi mbalimbali. 

Hata hivyo ameonya kuwa hatopenda kuona wafuasi wa vyama vingine watakao fika kwenye mkutano huo wa hadhara na kufanya fujo, watambuwe kuwa CUF ni chama makini kilicho na ujasiri wa vurugu lakini kwa sasa hakikusudii kufanya vurugu bali kiko kwaajili ya kuzitangaza sera na mikakati madhubuti ambayo itakiwezesha chama hicho kuungwa mkono kwa kupata wanachama wapya ili kuweza kushinda uchaguzi 2015.

Aidha Chama  cha CUF kimejipanga kujiimarisha zaidi kwa kupata wabunge wengi kwenye uchaguzi ujao nchini ili kuwezesha kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa kama ilivyo Zanzibar.

Juma Duni Haji  ametoa wito kwa wananchi kufika kwa wingi kwenye mkutano huo utakaofanyika katika viwanja vya Nghokozi al-maarufu 'Dampo' vilivyopo barabara ya Uhuru jijini Mwanza.
Sehemu ya wandishi wa habari waliohudhuria kikao cha mazungumzo na Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Taifa.

Na ujumbe ulihusishwa.

Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Taifa ambaye pia ni Waziri wa Afya  wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar Juma Duni Haji akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza hii leo asubuhi.

Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Taifa ambaye pia ni Waziri wa Afya  wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar Juma Duni Haji akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza hii leo asubuhi.

MABONDIA WAPIMA UZITO KWA AJILI YA MPAMBANO WA KESHO


Bondia Antony Mathias (kushoto) akitunishiana misuri na Fadhili Majia baada ya kupima uzito, Dar es salaam  kwa ajili ya mpambo wao kesho utakaofanyika katika ukumbi wa CCM Tandare.
(Picha na 
www.superdboxingcoach.blogspot.com)

   

Mabondia Hassan Mandulla na Jems Martin wanatarajia kupanda ulingoni  Kesho jumapili Janual 27 katika ukumbi wa wa CCM Tandare Dar es salaam akizungumza mpambano huo mwandaaji Waziri Rosta amesema  wamepima uzito leo pamoja na kujua Afya zao mabondia wote watakaocheza kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi yakiwemo ya mabondia maarufu na chipkizi alisema mapambano ya utangulizi ni Fadhiri Majia na Anton Matiasi mpambano mwingine


Utamkutanisha Kalama Nyilawila atakaezidunda na Athumani Pendeza mpambano wa raundi nane kalama anapanda ulingoni baada ya mpambano wake wa mwisho kupondeza kwa K,O raundi ya sita na Francis Cheka 

michezo mingine ni  Shabani Kilumbelumbe na Mwaite Juma na Chaeles Mashali atavaana na Adam Ngange, Julias Noro atapambana na Abdallah Luwajempambano mwingine utawakutanisha Rajabu Tumaini na Daudi Anton na Rashid Mohamed Atavaana na Eliman Richard wakati Rashid Hamisi atamvaa Omary Shabani
 

Super D, alisema katika mpambano huo atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio, Juan Emanuel Marquez, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina 
michezo ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema. 

 Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia  hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo.   

Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana

Friday, January 25, 2013

HII NI WIKI ALIYOAPISHWA RAIS OBAMA KWA MUHULA WA PILI.

Obama akiapishwa aliwaambia wamarekani kuwa huu ndio wakati wa kijiimarisha kama nchi hasa baada ya kukabiliana na changamoto kama za kiuchumi na afya

Obama na makamu wake wa rais Joe Biden

Sasha na Malia Obama nao hawakuachwa nyuma wakati wa sherehe hizo.

Wakati wa densi.

Baada ya sherehe wageni walitumbuizwa lakini hapa Obama na mkewe walipata fursa ya kucheza densi na wanajeshi.

Beyonce alikuwepo pia kuwatumbuiza watu waliofika kumpongeza Obama.

Mamia walijitokeza ili wasikose fursa ya kushuhudia jambo la kihistoria la kuapishwa kwa rais mweusi mara ya pili.
Obama na mkewe Michelle wakiwaamkua wananchi waliofika kumpongeza.

Obama na mkewe waliandaliwa dhifa ya jioni baada ya shereh hizo.

Gwaride la jeshi.

CLOUDS MEDIA GROUP YAUKARIBISHA MWAKA KWA HAFLA YA KUKATA NA SHOKA USIKU HUU

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group,Bwa.Joseph Kusaga akiwa sambamba na mke wake,ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni bingwa ya burudani hapa nchini,ya Prime Time Promotions Ltd,Johayna Kusaga,akizungumza mbele ya wafanyakazi mbalimbali wa kampuni hiyo waliokutana usiku huu kwenye hafla fupi (hawapo pichani) ya kuukaribisha mwaka na kuzungmza mambo mbalimbali ikiwemo na mafanikio yaliyopatikana mwaka jana,pia kuwashukuru kwa ushirikiano wao mkubwa ambao wamekuwa wakionesha kwenye kampuni hiyo kwa ammoja.

Boss Joe akiwaomba wafanyakazi wote wazinyanyue glassi zao za vinywaji juu na kuzigonganisha kwa pamoja kuonesha upendo,mshikamano na ushirikiano.Baada ya hapo Wafanyakazi walipewa ruksa ya kula kunywa na kujimwaya mwaya.

 Shampeni ikimiminwa baada ya kufunguliwa.

Eprahim Kibonde akimminia kinywaji aina ya Shampeni meneja wa vipindi Sebastian Maganga baada ya kufunguliwa,ikiashiria kuwa hafla ya kunywa,kula imefunguliwa rasmi usiku huu huku baadhi ya wafanyakazi wa Clouds Media wakishuhudia tukio hilo.

Mtangazaji wa kipindi cha power breakfast,Gerald Hando akizungumza jambo mbele ya Wafanyakazi wenzake usiku huu kabla ya kufungua shampeni,wa pili kulia ni Barbra Hassan,B Dozen,Eprahim Kibonde,Millard Ayo pamoja na Dina Marious.

Dj Zero akiangusha ngoma live ndani ya kiota cha maraha cha Escape 2 usiku huu.





Baadae wafanyakazi wa Clouds Media Group walianza kupata chakula cha pamoja kama uonavyo pichani.

Kulia ni Paul James a.k.a PJ,Suka,Dj Steve B pamoja na Dj Peter Mo wakipata msosi huku wakibadilisha mawazo usiku huu ndani ya kiota cha Escape 2
  
Dj Mayanga akiangusha ngoma za kufa mtu usiku huu ndani ya Escape 2 
Pichani kulia ni Dj Venture,Gerald Hando pamoja na Mdau mwingine.
Kulia ni Dj Too Shot,Dj Bulla akiw ana Mdau kimapozi ndani ya picha.
 Mmoja wa watangazaji wa kipindi cha Power Breakfast,Paul James a.k.a PJ akifurahia jambo na Meneja vipindi wa clouds FM,Sebastian Maganga usiku huu ndani ya kiota cha maraha cha Escape 2.
Dj PQ aliyekaa wakipiga stori na sebastian Maganga pamoja na PJ.
Mzee wa Kipindi Cha Jahazi,Eprahim Kibonde na mdau mwingine wakipata vitu laini laini safi kabisa.

Ilikuwa ni full kujichana, kula kunywa na kufurahi pamoja ikiwa ni sehemu ya hafla usikuu huu ndani ya Escape 2.
 Dada Regina Mwalekwa akiwa amepozi na Bonge Barabarani.

Cheersssss..
Pichani kulia ni mdau mkubwa wa Clouds Media Group,Dauda wa Kota akifurahia jambo na Dada Regina Mwalekwa.
Sehemu ya kikosi kazi cha Clouds Tv wakishangilia jambo.

Thursday, January 24, 2013

WASIRA AKWAMA KUSURUHISHA MGOGORO WA KUCHINJA BAINA YA WAISLAMU NA WAKRISTU


Leo kutwa nzima Wasira alikuwa akikutana na pande mbili baina ya Waislamu na Wakristu kuhusu nani mwenye haki ya Kuchinja.

Wasira alianza kwa kuzungumza na viongozi wote kicha kuzungumza na Waislamu pekee na baadaye Wakristo, lakini katika majumuisho alipowakutanisha wote alieleza kwamba msimano wa serikali waendelee kuchinja Waislamu lakini na Wakristu wachinje majumbani kwao.

Uamuzi huo umepingwa na Wakristu na kusema suala la kuchinja Waislamu nyama ya Bucha lilikuwa ni ustarabu na siyo sheria hivyo kugomea maamuzi waziri Wasira wakieleza hata wakristu wanayo haki ya kuchinza.

Sijui tunaelekea wapi, serikali imefumbia macho mgogoro huu na sasa umefikia kubaya.


MAONI YANGU NI:-

AIRTEL NGOMA MPETO, SASA KULONGA SENTI KUMI TU KWA SEKUNDE BAADA YA DAKIKA YA PILI.

Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Tanzania akifafanua jambo jinsi wateja wa Airtel watakavyofaidika na huduma ya punguzo la gharama za maongezi hadi senti 10 kwa sekunde

Wateja wa airtel sasa kupeta kwa senti 10 kwa kupiga simu baada ya dakika ya pili ya maongezi. Huduma hizo imezinduliwa leo makao makuu ya Airtel Tanzania

Meneja Masoko wa Airtel Tanzania Rwebugisa Mutahaba akifafanua  jambo jinsi wateja wa airtel watakavyoweza kufurahia punguzo nafuu ya la senti10 kwa sekunde baada ya dakika ya pili kuanzia leo


Wataalamu wa Airtel kitengo cha masoko na Mawasiliano wakionyesha vipeperushi vitakavyotumiwa kuelimisha jamii juu ya punguzo hilo wakiwa kwenye bonge la pozi.

Baadhi ya wafanyakazi wa airtel wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa punguzo gharama za huduma ya kuongea yaa Airtel-airte hadi senti 10 kwa sekunde baada ya dakika ya pili

Mfanyakazi wa Airtel kitengo cha ugavi akielezea kufuruahishwa na punguzo la kupiga simu kwa senti 10 baada ya dakika ya pili wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma hiyo leo ktk ofisi za Airtel dar

Airtel yapunguza gharama za kupiga simu hadi senti 10 kwa sekunde

*       Wateja kufurahia punguzo la asilimia 70 kupiga simu Airtel kwenda Airtel
*       Wateja wa Airtel kupiga simu kwa senti 10 tu kwa sekunde baada ya dakika mbili
*       Hakuna kujiunga, kila mteja wa malipo kabla ameunganishwa kufurahia viwango hivyo.

K
ampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea na dhamira yake ya kutoa mawasiliano nafuu nchini kwa kutangaza punguzo la gharama za kupiga simu kwa lengo la kutoa fulsa zaidi kwa wateja wa Airtel wa malipo ya kabla kuendelea kufurahia huduma za Airtel

Sasa wateja wa Airtel watatozwa senti 10 kwa sekunde baada ya dakika ya pili ya maongezi kwa kupiga simu Airtel kwa Airtel.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo, Mkurugenzi wa Airtel Bw Sam Ellangallor alisema" tumepunguza gharama zetu za kupiga simu kwa asilimia 70 ili kuendelela kutoa huduma za kisasa, rahis na  za bei nafuu kuweza kukidhi mahitaji ya wateja wetu  sasa kupiga simu Airtel kwenda Airtel  ni kwa bei nafuu zaidi ambapo wateja wa Airtel watatozwa senti 10 kwa sekundi baada ya dakika mbili za awali pale watakapopiga simu Airtel kwenda Airtel. Hakuna sababu ya kushindwa kuwasiliana kwani Airtel inakuwezesha kuongea na familia na marafiki zako siku nzima bila kikomo kwa gharama nafuu ya senti 10 kwa sekunde"

"Tunafahamu huduma ya mawasiliano ni nyenzo kubwa kwenye shughuli za kiuchumi na kijamii kwa wateja wetu, Hivyo ndio maana Airtel tunajitahidi sana kuwaletea wateja huduma zenye ubunifu wa hali ya juu ili kutoa unafuu wa mawasiliano zaidi.

Airtel bado tunaendlelea na mkakati wetu wa kupunguza gharama za mawasiliano ili kutimiza dhamira yetu ya kutoa huduma bora".aliongeza Elangallor.

Airtel hivi karibuni imepunguza gharama za kutuma sms kwa kupitia huduma yake ya SMS Kichizi ambapo ujumbe mfupi wa maneno kwenda mtandao wowote unatozwa shilingi moja mara baada ya kutuma ujumbe mfupi wa kwanza kwa shilingi 125 tu.


Akitoa maelezo zaidi ya huduma hiyo ya ya punguzo la gharama za mawasiliano Mkurugenzi  wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya "leo tumewawezesha wateja wake kuongea kwa senti 10 tu kwa sekundu na kutoa uhuru zaidi wa kuongea.Hakuna haja kwa mteja wa Airtel kujiunga na gharama hizi mpya nafuu, ukiwa unatumia Airtel tu moja kwa moja utakuwa umeunganishwa na huduma hii nafuu.

Akizungumza juu ya muda Mallya aliongeza hizi ni gharma za kudumu  zitakazopatikana nchi nzima

Airtel Tanzania ni kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma bora na nafuu kama Airtel money na huduma ya internet ya kasi ya 3.75G. Mwanzoni mwa mwaka huu Airtel  imetoa punguzo la gharama za ujumbe mfupi (SMS) ijulikanayo kama  SMS kichizi inayowawezesha wateja wakel kutuma kila SMS kwa shilingi 1 kwa siku