ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 12, 2013

TAMAA ZA MALI NA UMASIKINI ZASABABISHA WAZAZI KUOZESHA MABINTI ZAO MAPEMA KATIKA KIJIJI CHA DODOMA MKOANI SIMIYU.

Mratibu wa safari ya uelimishaji toka Shirika la KIVULINI iliyopewa jina la 'Caravan Route' Bi. Hadija Liganga akitoa uelimishaji kwa wanakijiji wa Dodoma wilayani Bariadi mkoani Simiyu ambapo katika kijiji hiki baadhi ya wazazi walikiri kuwalazimisha kuwaozesha mabinti zao katika umri mdogo ili wajipatie mali.
Kundi la sanaa la Babatan toka jijini Mwanza lilikuwa chachu katika kutoa elimu kupitia sanaa ya maigizo ambapo lililenga changamoto kubwa zilizopo katika eneo husika na kuigiza yanayojiri kisha kuchanganua nini kifanyike kuleta mabadiliko. 
Macho mbele huku wengine wakirekodi yanayojiri... watoto sanjali na wazazi wao katika kijiji hiki cha Dodoma kilichopo wilayani Bariadi mkoani Simiyu wamevutiwa sana na elimu inayotolewa na Caravan Route kuhusu masuala ya elimu ya kijinsia.  
Igizo lililo sisimua toka kwao BABATAN.
Mabinti wanaoolewa katika umri mdogo wamejikuta katika manyanyaso kutoka kwa waume zao kutokana na  ukosefu wa elimu ya kujitambua na uelewa mdogo wa haki zao hivyo wamekuwa wakikubali kutii hata yale yaliyo wazi yenye unyanyasaji wakidhani kuwa wao ni watu wa chini na ni haki yao kufanyiwa matendo hayo mabaya. alifunguka mwanamama Veronica Stephen. 
Baadhi ya wazazi wa kijiji cha Dodoma wameshindwa kutimiza wajibu wao wa kusaka mali na chakula kwaajili ya kuzilisha familia zao, kwa maana hiyo basi wengi hukimbilia kuwaoza mabinti zao mara tu wanapomaliza darasa la saba kama njia mbadala ya kujipatia mali kama ng'ombe na nafaka za chakula ambazo hutolewa kama sehemu ya mahali. Afunguka Bi. Maria.
Mzee Matius Doto asema mfumo dume ndiyo chanzo cha unyanyasaji kwa jiamii nyingi kijiji cha Dodoma kilichopo wilayani Bariadi mkoani Simiyu. Amekiri kuozesha binti yake akiwa na umri wa miaka 16 kutokana na hali ya uchumi wa familia yake, kitendo ambacho kwa sasa anakijutia. (MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY)
Joseph Sayayi naye alikiri kumwachisha mwanae shule na kumwozesha kutokana na kutojua umuhimu wa elimu kwani naye hakusoma. 
Wazee wa kijiji cha Dodoma kilichopo wilayani Bariadi mkoa mpya wa Simiyu wakisikiliza kwa makini kilichokuwa kikiendelea toka kwa timu ya wadau wa Caravan Route waliojikita katika mpango wa kutoa elimu kwa vijiji, kata na wilaya zilizo athiriwa na ukatili pamoja na unyanyasaji wa kijinsia Kanda ya ziwa.
Hakika wananchi wa kijiji hiki walivutiwa sana na masomo na ushauri uliokuwa ukitolewa na timu Caravan Route.
Mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo safari kuelekea kijiji kingine iliwadia, ambapo njiani changanoto za barabara kujaa maji na njia kutopitika ziliikabili timu ya waelimishaji Caravan Route, na hapa ilibidi chombo chetu cha usafiri kipige STOP kuyapisha maji.
Barabara ilikuwa haionekani...Hata hivyo daadaye safari iliendelea...kukifikia kijiji kingine kujionea changamoto...ITAENDELEA.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.