ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 6, 2013

SAKATA LA ZITTO LAWACHOMOA VIJANA 200 CHADEMA MWANZA

Na Peter Fabian.                                    
MWANZA. 

UMOJA wa Vijana wa Kata ya Mahina Wawapongeza Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa Wilaya ya Nzega Hessein Bashe na aliyekuwa Mjumbe wa Baraza kuu UVCCM Taifa toka Mkoa wa Mwanza Barnabas Mathayo kwa kufanikisha harambee yao na kupata kiasi cha milioni 10.7 Wilayani Nyamagana.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa UVCCM Gwalis Ahamada baada ya kumalizika kwa zoezi la harambee lililotanguliwa na ufunguzi wa mashina matano ya  vijana katika mitaa ya Bugarika (Shina la Igelegele), Buzuruga (Shina la Mwananchi), Nyakato (Shina la Isegenge ), Igoma (Shina la Machinjioni) na Mahina (Shina la Nyangulugulu) ambapo yalipatiwa fedha kiasi cha milioni 1.8 kwa yote.

Akizungumza kabla ya kuanza kuchangisha waalikwa na wananchi mgeni rasimi Mathayo aliyeongoza harambee hiyo kutokana na Bashe kuwa na majukumu mengine ya kikazi aliwaeleza vijana kuwa wajibu wao ni kuitumikia jumuia hiyo kwa kila hali na kuhakikisha Chama cha Mapinduzi kinazidi kuongoza na kuunda serikali pamoja na kutekeleza Ilani yake kwa vitendo.

Mathayo ambaye alipokea vijana 200 walioamua kujiunga kuwa wanachama wapya wa  UVCCM  na CCM Kata ya Mahina kwa madai kuwa wamechoshwa na hila na vurugu zinazoendelea kwenye Chama cha Demkrasia na Maendeleo (CHADEMA) na hivyo kuamua kukitosa chama hicho na kujiunga kwenye jumuiya hiyo na CCM Katani humo.

Mjumbe huyo mstaafu aliwakumbusha vijana hao kanuni na taratibu za jumuiya na CCM ambapo inawataka kuwa wanachama waaminifu na watiifu na kuachana na tabia yakuwa wanachama ndumilakuwili kwa kuwa na Kadi za Vyama vingine vya siasa kama ilivyo kwa wanasiasa wengine.

“Msiwe kama Yule Babu ambaye ni Katibu wa Chama fulani lakini anakadi ya CCM na amekuwa akiwajibu watu kuwa ni mali yake na ametunza kumbukumbu ya wajukuu zake hivyo nawahasa kuacha kufuata nyayo hizo kwa kuwa huo ni “umalaya” wa siasa na watu kama hao hawafai kuongoza Taifa letu kwa vile lengo lao ni uchu wa madaraka tu na si kuwatumikia wanachama”alisisitiza.

Mathayo alisema kwamba wanachama wa UVCCM na CCM wakiwa na umoja na kufuata kanuni na taratibu zilizopo za Katiba hakuna chama ambacho kitaweza kuishinda CCM katika chaguzi zijazo kwa kuwa chama kitakuwa na mvuto na ukizingatia nyinyi ni vijana mliokubali kwa ihali yenu kujiunga .

“Niwapongezeni sana kwa uamuzi wenu sahihi na kwa wakati sahihi kutaongeza ari ya vijana wengine kujiunga na jumuiya na Chama kwa kuwa ndicho chama pekee kimbilio la wengi chenyekuwajali vijana na watanzania kwa kuhakikisha usawa na demkrasia inaendelea kuwa imara ndani ya chama hiki kikongwe Barani Afrika ” alisisitiza.

Mmoja ya wanacha wapya aliyejiunga na CCM katika Kata hiyo ambaye alikuwa Katibu wa Shina la CHADEMA eneo la Buzuruga William Mahene alipopatiwa nafasi ya kusalimia alisema kuwa CCM ni chama bora afrika kitaendela kutawala kutokana na kufuata vyema kanuni na taratibu za Katiba yao na si CHADEMa kila siku ni kufukuzana hakina dira bali ni kuwahamasisha vijana ili kupata umaarufu tu si kushika dola.

“Nilikuwa huko lakini kitendo walichofanyiwa wanasiasa na wengine kuenguliwa kwa hila akitolea mfano wa Dr. World Kaburu (Kigoma) , David Kafurila (Mbunge) na sasa Mbunge Zitto Kabwe (Naibu Katibu Mkuu), Dr Kitilya Mkombo (Mjumbe Kamati Kuu) kwa hila na njama za kina Godbless Lema (Mbunge-Arusha) John Mnyika (Mbunge-Ubungo) , Freeman Mbowe (Mwenyekiti) na Dr. Wilbroad Silaa (Katibu Mkuu)” alisema.

Wachangiaji wa Harambe hiyo ni Bashe (laki tano), Mathayo (milioni 3), Meya wa Jiji la Mwanza Stanislaus Mabula (milioni 3), Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mahina James Bwire (milioni 2) walioongoza waalikwa wengine kuwachangia na kufikia lengo lililokusudiwa katika harambee hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.