ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 5, 2013

MBINU YA MUUZA MAGAZETI NI 'CHIBOKO'

Kwa wale wanao 'peruzi na kudadisi' kisha wanasepa bila kununua magazeti hapa wamekomeshwaje...!?
Kabla ya mbinu hii, ilikuwa desturi ya wakazi wa eneo la Lamadi mkoani Simiyu kufika kwenye kiota hiki cha mchuuzaji magazeti, mara tu magazeti ya siku yanapotinga, watu walikuwa wanayasoma yakiwa mezani wakidai kwamba wanatizama yaliyomo kisha watanunua na mwisho wa siku wasinunue kwa madai kuwa hawajakuta habari wazitakazo, hali ambayo imekuwa ni hasara kwa muuzaji, mtu anapitia taarifa zote muhimu za gazeti kisha anasepa, wakiyaacha magazeti yamechakaa na kutota mafuta kutokana na kupitiwa na kila mkono wa msomaji. 
Magazeti yakawa yanamdodea sana jamaa na kila siku akiyarudisha kwa wakalawake, kuona hivyo ndipo alipokuja na mbinu hii ya kuweka wavu, kwamba gazeti unalitizama kwa mbaaaaaali kama kuku bandani.
Na imekuwa suluhu jamaa sasa anafanya biashara.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.