ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 2, 2013

UCHAGUZI ZIMBABWE ULIKUWA HURU ASEMA OBASANJO

Upigaji kura kumchagua rais kati ya Robert mugabe na hasimu wake Morgan Tsvangarai.

Daftari hili lima majina ya wapiga kura waliofariki huku wengine wakiwa wamesajiliwa zaidi ya mara mbili na namba zao za vitambulisho zikiwa zimetofautiana.

Ingawa ni msimu wa baridi kali lakini nchini Zimbabwe lakini licha ya hayo wengi walijitokeza kupiga kura na pia kulikuwa namadai kuwa tayari kumetokea visa vya wizi wa kura hasa kwa daftari la wapiga kura lililotoka mkesha wa kupiga kura.

'Uchaguzi Zimbabwe ulikuwa huru'Obasanjo

Mkuu wa ujumbe wa uangalizi kutoka Muungano wa Afrika nchini Zimbabwe, Olusegun Obasanjo amesema uchaguzi mkuu wa hapo Jumatano ulikua huru na haki. Matokeo ya awali yanaoyesha Rais Robert Mugabe na chama tawala cha Zanu PF wakiongoza kwa kura nyingi
Chama hicho tayari kimedai ushindi. Msemaji wa chama hicho Rugare Gumbo alisema chama hicho kilitarajiwa kushinda kiasi ya asilimia 70 ya kura hizo.

Lakini mpinzani wa Mugabe, Morgan Tsvangirai, amesema uchaguzi huo ni wa uongo na kusema udanganyifu uliofanyika una maana uchaguzi huo haukubaliki.

Waangalizi kutoka Umoja wa Afrika na jumuia ya maendeleo kusini mwa Afrika wanatarajiwa kutoa tamko rasmi hii leo kuhusu uchaguzi huo.

Bw. Obasanjo amesema kulikua na visa kadhaa wakati wa shughuli ya kupiga kura. Hata hivyo amesema visa hivyo haviwezi kutajwa kuwa na uzito wa kubatilisha au kufuta matokeo ya kura.
Msimamo wa Muungano wa Afrika unatofautiana na ule wa kundi la uangalizi la Zimbabwe Election Support Network.

Kundi hilo ambalo ndilo kubwa zaidi linalochunguza kura ya Zimbabwe limekashifu uchaguzi mkuu na kusema ulikuwa na dosari nyingi. Hii ni kwa sababu watu milioni moja walizuiwa kupiga kura.

Huku upande wa Rais Mugabe ulitangaza kushinda uchaguzi na Morgan Tsvangirai akipinga ni dhahiri kwamba Zimbabwe ingali na mgawanyiko mkubwa wa kisiasa..
SHUKURANI BBC Swahili.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.