ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 31, 2013

BANDARI ZA MWANZA KASKAZINI NA KUSINI ZACHAFULIWA NA MGOMO WA MAKULI WADUMU KWA MASAA 7 WAFANYABIASHARA WALAANI

Nje ya lango kuu la Bandari ya Kaskazini jijini Mwanza ambapo lango hilo lilifungwa kwasababu za usalama.
 BANDARI ya Mwanza Kaskazini na Kusini yachafuka ni kutokana na mgomo wa wafanyabiashara na watu wanaofanya shughuli za kubeba mizigo (Makuli)  kugomea kutozwa VAT mala mbili ya kupakia na kupakua mizigo yao, ushuru na makato mengine na kusababisha shehena ya mizigo kutoka Bukoba kukaa ndani ya meli kwa masaa 7 Bandarini hapo Jijini Mwanza.

Sakata hilo lilitokea jana kuanzia majira ya saa12:30 na kudumu hadi saa 7:00 mchana baada ya Meli ya Mv Victoria kuweka Nanga  kwenye Bandari ya Mwanza Kaskazini kufatia Mamlaka ya Bandari nchini( TPA) kutoa maelekezo kwa uongozi wa TPA Mwanza kuwa muda wa mzabuni aliyekuwa akifanya kazi za kupakia, kupakua na kutoza ushuru wa mizigo kumaliza muda wake na kazi hiyo kufanywa na Mamlaka hiyo.
Askari wamezingira lango kuu la Bandari ya Kaskazini jijini Mwanza ambapo lango hilo lilifungwa kwasababu za usalama.

Askari akilinda lango kuu kuzuia watu wasitinge bandarini ambapo shughuli zote za huduma na biashara zimesimama.

 Akizungumza wakati wa kutekeleza mgomo huo Mwenyekiti wa Ushirika wa Wahudumu wa Bandari ya Mwanza Kaskazini na Kusini Rajabu Said alisema kuwa wao waliokuwa wazabuni wa kufanya shughuli za kupakia, kupakua na kutoza ushuru wa mizigo Bandarini hapo kugomea  na TPA kuendelea na kazi hizo kutokana na muda wa miaka miwili waliokuwa wamepewa kumalizika na kutakiwa kutjishughulisha tena.

Mwenyekiti Said alieleza kuwa kutokana na Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) kutoa mwongozo wa ukusanyaji mapato na ushuru baada ya kumalizika kwa muda wa USHIRIKA wa miaka miwili uliokuwa umetolewa kwa zabuni ambayo walishinda mwaka 2011 hadi kumalizika Agosti 30 mwaka huu aligubikwa na mizengwe na kuwa na usiri na kutowekwa bayana na viongozi wa TPA Mwanza.

Mwenyekiti Said akizungumza na chombo cha habari.
 “Muda wetu umekisha kama mzabuni aliyekuwa na tenda ya kufanya kazi Bandari ya Mwanza Kaskazini na Kusini lakini TPA hawajatangaza Tenda upya na walipotuita viongozi wa Ushirika na TPA kwenye kikao cha pamoja walidai kutupatia muda wa mwezi mmoja zaidi ili kutangazwa Tenda upya kumpata mzabuni atakayeshinda kufanya kazi hizo” alisema Said na kuongeza kuwa.


Baada ya Kikao hicho kumalizika kwa makubaliano yaliyoafikiwa  jambo la kushangaza asubuhi ya leo Agosti 31 mwaka huu wakati tulipofika Bandarini Mwanza Kaskazini tulikuta utaratibu mpya kwa walinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya SUPREM na kuteleleza kuwa haturuhusiwi kufanya shughuli za kutoza ushuru, kutoza mizigo tutakayo pakua leo Jumamosi (Jana) na kupakia Jumapili na kazi hiyo iko chini ya TPA kuanzia sasa.

Said alisema baada ya taarifa hiyo tulipinga na kuwataka wafanyabiashara wa kutoka Mjini Bukoba kuacha kushusha mizigo hiyo hadi muafaka upatikane na wao waliafiki kwa kutuunga mkono kutokubaliana na uongozi wa TPA kwa vile ulilenga kuwatoza fedha zaidi kwa kulipia VAT mala tano kwa mizigo yao ikiwa ni kupakia kulipa VAT asilimia 18 kwa Marine na TPA ikiwa na kushusha na tozo la fedha za Makuli hao.

“Hatukubaliani na kabisa na kilichofanywa na uongozi wa TPA kwani zabuni haijatangazwa nasi tukapata kutuma maombi yetu lakini imedaiwa kuwa kuna Chama cha Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo (TPA) Mwanza (DOWUTA) wamekisajili ili kuchukua nafasi ya Ushirika kufanya kazi hiyo na ndiyo maana Tenda hawajaitangaza na tumeelezwa na uongozi kuna mzabuni tayari nasi tumepinga na kugomea kukubaliana na utaratibu huo hivyo Bandari zote Makuli tumeomba uwazi uwepo na tenda zitangazwe” alisisitiza.

Ushirika huo wenye jumla ya wanachama 3000 na ulisajiliwa na kufanya kazi hizo Bandari za Mwanza Kaskazini na Kusini baada ya kushinda zabuni hiyo mwaka 2011 ulipunguza tatizo la ajira na kuwafanya wanachama hao ambao ni wafanyakazi wa kubeba mizigo wamekuwa na utaratibu wa kukopeshana, kuchaniana kwa matatizo ya ugonjwa na kutoa fedha kwa mwanachama anayefariki na wanaositaafu kubeba mizigo hulipwa milioni 1.5 ikiwa na hisa yake ya uanachama hivyo kutopewa kazi hiyo imedaiwa kuongeza watu kujihusisha na uhalifu mitaani na kuweka mashaka kwa wasafiri na mizigo yao kuanza kuibiwa na watu kwa kukabwa nakati za usiku na asubuhi.

Mizigo imedoda melini hakuna wapakuaji.

Ile hali meli ikiwa imejaa mizigo na bidhaa za ndizi baadhi ya wafanyabiashara waliamua wenyewe kupakua mizigo.


Vuta nikuvute nje ya lango la Mamlaka ya Bandari.

Baada ya vuta ni kuvute kutoka kwa wafanyabiashara na uongozi wa TPA Mwanza na Makao Makuu iliyotuma wawakilishi wake kujadiliana na kuona jinsi ya kumaliza mvutano huo na kumaliza mgomo wa Makuli hao na kupelekea kuibuka Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Huduma wa TPA Clementi Kiloyavaha na kueleza kuwa utaratibu uendelee kwa leo kama ilivyokuwa wakati wakianda Kikao cha pamoja.

Kiloyavaha alisema kwamba kutokana na maelekezo kutoka kwa Waziri wa Uchukuzi Dr.Harison Mwakyembe kwa Mamlaka hiyo ya TPA wamepewa utaratibu na hivyo utaanza kutekelezwa kuanzia Septemba mosi na kunachotakiwa kufanyika ni kikao cha pamoja baina ya wadau wa TPA na Wafayabiashara wanaotumia Bandari za Mwanza Kaskazini na Kusini kuwapa utaratibu mpya.

Kwa upande wa wafanyabiashara baadhi yao waliozungumizia sakata hilo na kukataa kutajwa majina yao walisema kuwa wao wanapinga kutozwa VAT asilimia 18 kwa kila tani moja na vifurushi wakati wa kupakia na kupakua mala mbili ikiwa ni kwa Kampuni ya Meli ya Marine na Mamlaka ya Babdari TPA pamoja na kutozwa VAT ya fedha za vibarua wa kupakia na kupakuwa wanayolipia kuwa ni kero kubwa kwao.

“Hili litatufanya kuacha kupitisha mizigo yetu katika Bandari hizi za TPA kwa vile utaratibu huu umelenga kuturudisha nyuma na kutukamua zaidi na kukosa faida kabisa na leo tumepoteza wateja na tutauza ndizi,mihogo na matunda kwa bei ya hasara na hili limetukera sana nibora wangetuarifu kwa matangazo badala ya kukurupuka na kuamua hata kama ni maagizo ya Waziri Mwakyembe” walisema .


Hali ililejea majira ya saa 7:00 mchana makuli na wafanyabiashara kuendelea na utoaji wa bidhaa zao na kupakia baada ya kuishusha ili iliyotoka Mji wa Bukoba na kusababisha mgomo wa masaa 7 na kuasilika kwa makundi ya wafanyabiashara wa ndizi mbivu na mbichi, matunda na mihogo katika masoka mbalimbali ya Jiji la Mwanza kama ilivyozoeleka Meli ya Mv Victoria inapofika Jijini Mwanza toka Mjini Bukoba.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.